Hamia kwenye habari

Tuzo ambayo Mashahidi wa Yehova walipokea katika shidano la Buildings of Excellence, ikiwa juu ya kigezo cha majengo ya Ramapo

MACHI 28, 2023
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE

Mradi wa Makao Makuu wa Ramapo

Jimbo la New York Lawapa Tuzo Mashahidi wa Yehova kwa Sababu ya Muundo wa Majengo ya Ramapo

Jimbo la New York Lawapa Tuzo Mashahidi wa Yehova kwa Sababu ya Muundo wa Majengo ya Ramapo

Mamlaka ya Utafiti na Maendeleo ya Nishati ya Jimbo la New York (NYSERDA) iliwapa Mashahidi wa Yehova tuzo ya dola milioni 1 (za Marekani) katika shindano la Buildings of Excellence Competition. Tuzo hiyo ilitolewa kwa sababu muundo wa majengo ya Ramapo hautahatarisha mazingira. a Hii ni mara ya kwanza kwa jengo lolote katika mji wa Ramapo au katika Jimbo la Rockland kushinda tuzo hiyo.

Keith Cady, ambaye anatumikia kwenye Halmashauri ya Mradi wa Ujenzi wa Ramapo anasema hivi: “Lengo letu lilikuwa kubuni muundo wa majengo ambayo yanatumia vizuri nishati inayopatikana bila kuchafua mazingira. Tunafurahi sana kwamba wenye mamlaka wameona jitihada zetu na kutupatia tuzo hiyo hata kabla ya ujenzi wenyewe kuanza. Fedha hizo pamoja na michango ya hiari ya Mashahidi wa Yehova zitatumiwa vizuri.”

Shindano la Buildings of Excellence Competition ndilo shindano pekee la aina yake nchini Marekani. Lilianzishwa Machi 2019 na kufikia sasa limetoa tuzo kwa miradi 63. Tovuti rasmi ya NYSERDA inasema kwamba miradi iliyopewa tuzo “inawahimiza wadau wa ujenzi kufuata mfano mzuri wa miradi hiyo, lengo likiwa kupunguza kaboni-dioksidi inayotokezwa duniani.”

Tunathamini kwamba wenye mamlaka wametambua ubora wa muundo wa majengo yetu na hilo linamletea Yehova utukufu.​—Mathayo 5:16.

a Jina tulilotumia kwenye shindano hilo lilikuwa “Makazi ya Sterlington.”