Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 39

Jifanyie Jina Zuri Mbele za Mungu

Jifanyie Jina Zuri Mbele za Mungu

(Mhubiri 7:1)

  1. 1. Tunatamani kupendeza Mungu.

    Tuwe na jina zuri mbele zake.

    Tukifanya mambo yampendezayo,

    Twafurahisha moyo wake.

  2. 2. Ulimwenguni watu hutafuta,

    Kujifanyia jina mashuhuri.

    Tukifuatia ulimwengu huu,

    Kibali cha Yah, tutakosa.

  3. 3. Twataka jina, libaki katika

    Kumbukumbu ya Yehova milele.

    Basi sikuzote tumtii Mungu,

    Na tudumishe jina zuri.