Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Aorta Ubuni wa Kustaajabisha

Aorta Ubuni wa Kustaajabisha

Aorta Ubuni wa Kustaajabisha

Aorta ni “bomba” tata zaidi kuliko wanasayansi walivyowazia mwanzoni. Mpindo wa aorta hushabihi mpini uliopindika wa mwavuli. Lakini sivyo ilivyo kikweli. Mpindo wa aorta si mpindo sahili wa nyuso mbili, bali una nyuso tatu, kama sehemu ya nusuduara iliyokatwa toka kwa springi iliyojikunja. Inapowekwa kwenye sehemu bapa, hujipindapinda na kuinuka.

Kwa nini ina umbo hilo? Kwa sababu badala ya kufanya damu itiririke tu palipopindika kama maji yanavyotiririka sehemu ambayo mto umepinda, umbo hilo hufanya damu izunguke-zunguke inapopita katika aorta. Maji hutiririka polepole sehemu ya ndani ya mpindo wa mto, na hivyo masimbi hurundamana. Lakini maji hutiririka kasi sana sehemu ya nje ya mpindo, na kumomonyoa ukingo wa mto. Mwendo wa damu kama huo katika aorta ungeweza kusababisha kurundamana kwa ukoga hatari damu inapotiririka polepole katika sehemu ya ndani ya mpindo. Hata hivyo, aorta hupunguza tatizo hilo kwa kulazimisha damu kutiririka kwa mzunguko na hivyo kusugua sawia kuta za ndani za mishipa.

Kwa kweli, aorta ni ubuni wa ajabu! Mtunga-zaburi wa Biblia alisema hivi kwa kufaa: “Nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha.”—Zaburi 139:14.

[Mchoro katika ukurasa wa 31]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

AORTA

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

Picha ya chembe za damu iliyo kwenye ukurasa wa 24-26, na 31: Lennart Nilsson