MEI 7, 2024
URUSI
Ndugu Anton Virich Amehukumiwa Kifungo cha Miaka Sita na Miezi Miwili Gerezani
Aprili 25, 2024, Mahakama ya Wilaya ya Pozharskiy iliyo katika Eneo la Primorye ilimhukumu Ndugu Anton Virich kifungo cha miaka sita na miezi miwili gerezani. Amekuwa gerezani tangu Julai 11, 2023, naye atabaki kizuizini.
Maelezo Mafupi Kumhusu
Tunafarijika kujua kwamba kadiri tunavyoimarisha upendo wetu kwa Yehova kwa kuvumilia majaribu, tunapata kibali na baraka kutoka kwake.—Yakobo 1:12.
Mfuatano wa Matukio
Februari 11, 2021
Kesi ya uhalifu ilianzishwa
Novemba 9, 2021
Bila hata kumjulisha, Anton alifunguliwa mashtaka ya uhalifu na akawekewa vizuizi vya kusafiri
Julai 11, 2023
Alipokuwa akiendesha gari katika jiji la Uzhur maofisa wa polisi walimjulisha Anton kwamba alikuwa mkimbizi na wakamkamata na kumweka mahabusu kwa siku kadhaa
Julai 15, 2023
Alisafirishwa kwa ndege hadi kwenye mahabusu ya Luchegorsk, umbali wa kilometa 4,700 hivi
Novemba 7, 2023
Kesi ya uhalifu ilianza
Aprili 25, 2024
Alihukumiwa kifungo cha miaka sita na miezi miwili gerezani