SEPTEMBA 18, 2019
KOREA KUSINI
Msimamo wa Kikristo wa Kutounga Mkono Upande Wowote Nchini Korea Kusini—Historia ya Imani na Ujasiri
Tangu mwaka wa 1953, akina ndugu vijana nchini Korea wamefungwa gerezani kwa sababu ya kukataa utumishi wa kijeshi. Zaidi ya ndugu 19,000 waliokataa kukana imani yao walifungwa jumla ya miaka 36,000 gerezani. Hata hivyo, mnamo Februari 28, 2019, ndugu wa mwisho aliyekuwa gerezani aliachiliwa. Ni nini kilichoongoza kwenye tukio hilo la kihistoria? Acheni tuchunguze rekodi ya akina ndugu nchini Korea inayoonyesha imani yenye nguvu na ujasiri thabiti.