Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

JW Lugha

JW Lugha ni programu rasmi iliyobuniwa na Mashahidi wa Yehova ya kuwasaidia wanaotaka kujifunza lugha kuboresha msamiati wao na ustadi wao wa kuzungumza na wengine katika huduma na katika mikutano ya kutaniko.

Inatia Ndani Lugha Nyingi

Chagua lugha moja ya kigeni unayotaka kujifunza kati ya lugha 22 zinazopatikana. Kati ya kiarabu, Kibengali, Kichina cha Kikantoni (cha Kitamaduni), Kichina cha Kimandarin (Sahili), Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, Kihindi, Kiindonesia, Kiitaliano, Kijapani, Kikorea, Kimalay, Kimyanmar, Kireno, Kirusi, Kihispania, Kiswahili, Kitagalogi, Kithai, Kituruki na Kivietinam.

 

Ina Habari Kuhusu Huduma

Maneno yaliyo katika programu ya JW Lugha yanahusu kuhubiri, kufundisha, na msamiati wa Biblia. Trakti kadhaa zilizopangwa zinapatikana ili uweze kulinganisha lugha yako na lugha unayojifunza.

Njia Mbalimbali za Kujifunza

  • Soma: Linganisha lugha yako upande mmoja na lugha unayojifunza upande wa pili

  • Sikiliza: Rekodi za mwenyeji akitamka neno mojamoja, mafungu ya maneno, na chapisho

  • Tazama: Kwa Nini Ujifunze Biblia? na Ni Nini Hutendeka Kwenye Funzo la Biblia? katika lugha yako na lugha unayojifunza

  • Mazoezi: Katika mfumo wa Kadi za Kumbukumbu

Vipendwa Ulivyochagua

Tengeneza sehemu kadhaa za kutunza Vitu Ulivyokusanya na uhifadhi misemo unayotumia mara nyingi au inayokutatiza ili uipate kwa njia ya haraka. Unaweza pia kutazama vitu ulivyokusanya katika mfumo wa Kadi za Kumbukumbu.

Kubadili Maandishi Yawe Katika Kiroma

Kwa lugha ambazo hazitumii mfumo wa maandishi ya Kiroma, maneno yanaonyeshwa katika Kiroma pia.

Utegemezo

Ukipata matatizo unapotumia JW Lugha, tafadhali jaza na utume fomu ya kutoa msaada inayopatikana katika Tovuti yetu.