Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

JW LUGHA

Mambo Mbalimbali Kuhusu JW Lugha

Mambo Mbalimbali Kuhusu JW Lugha

Lugha Zinazopatikana

Kiarabu, Kiindonesia, Kirusi, Kibengali, Kiitaliano, Kihispania, Kichina cha Kikantoni (cha Kitamaduni), Kijapani, Kiswahili, Kichina cha Kimandarin (Sahili), Kikorea, Kitagalog, Kiingereza, Kijerumani cha Low, Kithai, Kifaransa, Kimalay, Kituruki, Kijerumani, Kimyanmar, Kivietnam, Kihindi, Kireno

 

Ina Habari Kuhusu Huduma

Maneno yaliyo katika programu ya JW Lugha yanahusu kuhubiri, kufundisha, na msamiati wa Biblia. Trakti kadhaa zilizopangwa zinapatikana ili uweze kulinganisha lugha yako na lugha unayojifunza.

Njia Mbalimbali za Kujifunza

 • Soma maneno na maelezo katika lugha yako, kisha ulinganishe na lugha unayojifunza

 • Msikilize mwenyeji akitamka neno mojamoja, fungu la maneno, au chapisho

 • Tazama video kuhusu huduma katika lugha unayojifunza

 • Jifunze ukitumia picha

 • Tambua jinsi maneno mbalimbali yanavyoathiri muundo wa sentensi katika kuonyesha Sarufi

 • Fanya mazoezi ukitumia mbinu mbalimbali za kujifunza

  • Tazama: Chagua tafsiri ya neno unaloona

  • Linganisha: Chagua maneno yanayofanana

  • Sikiliza: Chagua tafsiri ya neno unalosikia

  • Kadi za Kumbukumbu: Fikiria tafsiri ya neno unaloona

  • Somo la Kusikiliza: Sikiliza maneno yakisomwa kwa sauti katika rekodi ya kusikiliza yenye sehemu zinazosimama kwa muda ili ufanye mazoezi

Panga Habari Kulingana na Mapendezi Yako

 • Hifadhi picha na maneno unayopenda ili uyapate haraka

 • Ongeza au upunguze mwendo wa sehemu ya kusikiliza maneno

 • Kwa lugha ambazo hazitumii herufi za Kiroma, unaweza kuchagua kuona maneno yaliyotoholewa katika herufi za Kiroma

 • Pakua habari ili uzitumie bila Intaneti

 • Tumia nafasi kidogo kwenye kifaa chako kwa kupakua video zenye ubora mdogo

Kubadili Maandishi Yawe Katika Kiroma

Kwa lugha ambazo hazitumii mfumo wa maandishi ya Kiroma, maneno yanaonyeshwa katika Kiroma pia.

Utegemezo

Ukipata matatizo unapotumia JW Lugha, tafadhali jaza na utume fomu ya kutoa msaada inayopatikana katika Tovuti yetu.