Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Utangulizi na Muhtasari wa Yaliyomo

Utangulizi na Muhtasari wa Yaliyomo

Baadhi ya mafundisho bora zaidi yanayojulikana ya Yesu yanapatikana katika hotuba aliyoitoa mlimani karibu na jiji la Kapernaumu, lililokuwa kwenye ufuo wa Bahari ya Galilaya. Hotuba hiyo inayojulikana kama Mahubiri ya Mlimani, inapatikana katika sura ya 5 hadi 7 ya kitabu cha Biblia cha Mathayo. Mafundisho hayo yanazungumziwa kwenye broshua hii ili uweze kunufaika na hekima ya Yesu.

  • SURA YA 5

    • Yesu aanza kufundisha mlimani (1, 2)

    • Mambo tisa yanayoleta furaha (3-12)

    • Chumvi na nuru (13-16)

    • Yesu alikuja kutimiza Sheria (17-20)

    • Mashauri kuhusu hasira (21-26), uzinzi (27-30), talaka (31, 32), viapo (33-37), kulipiza kisasi (38-42), kupenda adui (43-48)

  • SURA YA 6

    • Msijionyeshe kuwa waadilifu (1-4)

    • Jinsi ya kusali (5-15)

      • Sala ya mfano (9-13)

    • Kufunga (16-18)

    • Hazina duniani na mbinguni (19-24)

    • Acheni kuhangaika (25-34)

      • Endeleeni kuutafuta kwanza Ufalme (33)

  • SURA YA 7

    • Acheni kuhukumu (1-6)

    • Endeleeni kuomba, kutafuta, kupiga hodi (7-11)

    • Kanuni Bora (12)

    • Lango jembamba (13, 14)

    • Watajulikana kwa matunda yao (15-23)

    • Nyumba iliyo juu ya mwamba, nyumba iliyo juu ya mchanga (24-27)

    • Umati washangazwa na njia ya Yesu ya kufundisha (28, 29)