Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kuutazama Ulimwengu

Kuutazama Ulimwengu

Ulimwengu

Kumaliza njaa ni suala linalohusisha mengi zaidi ya uzalishaji wa chakula tu. Inakadiriwa kwamba kwa sasa wakulima wanazalisha chakula cha kutosha kulisha watu bilioni 12—zaidi ya watu bilioni 5 ukilinganisha na idadi ya sasa ya watu katika sayari yetu. Visababishi vikuu vya tatizo hilo ni ukosefu wa usawa katika uchumi na usambazaji wa chakula, na pia utupaji wa chakula.

Uingereza na Marekani

Karibu robo (asilimia 24) ya wafanyakazi wa mashirika ya kifedha waliofanyiwa uchunguzi walisema kwamba “huenda wakalazimika kujihusisha katika mwenendo ulio kinyume cha maadili au wavunje sheria ili wafanikiwe.” Asilimia 16 walikiri kwamba wangefanya uhalifu “ikiwa wangeweza kuepuka kukamatwa.”

Argentina

Nchini Argentina, walimu watatu kati ya watano huomba likizo kazini kwa sababu ya mkazo au jeuri kazini.

Korea Kusini

Nchini Korea Kusini, karibuni itakuwa ni jambo la kawaida kwa watu kuishi peke yao kuliko kuishi na mtu mwingine.

China

Inadhaniwa kwamba asilimia 66 ya majiji ya China yatashindwa kufikia viwango vipya vya kupunguza uchafuzi wa hewa vilivyowekwa na serikali vitakavyoanza kutumika mwaka wa 2016. Kwa kuongezea, maji mengi yanayopatikana chini ya ardhi yamesemekana kuwa “machafu au machafu kupindukia.”