Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

2 Je, Tunapaswa Kujilaumu Tunapoteseka?

2 Je, Tunapaswa Kujilaumu Tunapoteseka?

Kwa Nini ni Muhimu Kupata Jibu la Swali Hilo?

Ikiwa jibu ni ndiyo, basi huenda tunaweza kupunguza matatizo tunayokabili.

Jambo la Kufikiria

Wanadamu wamechangia kwa kiasi gani kuwepo kwa matatizo yafuatayo?

  • Kutendewa Vibaya.

    Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kwamba mtu mmoja kati ya watu wanne aliwahi kutendewa vibaya alipokuwa mtoto na mwanamke mmoja kati ya watatu hutendewa vibaya kimwili au kingono (au yote mawili) katika maisha yake.

  • Vifo.

    Takwimu ya Afya ya mwaka 2018 iliyochapishwa na Shirika la Afya Duniani inasema hivi; “Inakadiriwa kwamba watu 477,000 waliuawa duniani kote mwaka wa 2016.” Idadi hiyo inatia ndani watu 180,000 hivi ambao inawezekana waliuawa kwenye vita au vurugu zilizotokea mwaka huo.

  • Matatizo ya Afya.

    Makala iliyochapishwa kwenye jarida la National Geographic ya Fran Smith ilisema kwamba watu zaidi ya bilioni moja huvuta sigara na inasemekana kwamba sigara ni mojawapo ya chanzo cha magonjwa yanayosababisha vifo vya watu wengi kama vile magonjwa ya moyo, kiharusi na kansa ya mapafu.

  • Kutokuwa na Usawa Katika Jamii.

    Mwanasaikolojia Jay Watts anasema hivi: “Umaskini, kutokuwa na usawa katika jamii, kubaguliwa kwa sababu ya rangi, ubaguzi wa kijinsia, kulazimishwa kuhama eneo unaloishi au kuishi katika jamii yenye mashindano husababisha mkazo, kushuka moyo, mahangaiko na hofu.”

    JIFUNZE MENGI ZAIDI

    Tazama video Kwa Nini Mungu Aliiumba Dunia? kwenye jw.org/sw.

Mambo Ambayo Biblia Inafundisha

Matatizo mengi yaliyopo ulimwenguni leo yamesababishwa na wanadamu.

Matatizo mengi yamesababishwa na serikali zenye ukandamizaji zinazodai kuhangaikia masilahi ya raia wake na hivyo kufanya maisha yawe magumu kwa wanadamu.

“Mwanadamu amemtawala mwanadamu mwenzake kwa kumuumiza.”​MHUBIRI 8:9.

Tunaweza kupunguza matatizo.

Kanuni za Biblia zinatutia moyo tuwe na afya nzuri na uhusiano mzuri pamoja na wengine.

“Moyo mtulivu huupa mwili uzima, lakini wivu huozesha mifupa.”​METHALI 14:30.

“Acheni kabisa kila aina ya chuki yenye uhasama, hasira, ghadhabu, kufoka, matusi, na mambo yote yanayodhuru.”​WAEFESO 4:31.