Hamia kwenye habari

NOVEMBA 18, 2016
URUSI

SEHEMU YA 2 Nyongeza

Mahojiano ya Pekee—Wataalamu Wapinga Tishio la Urusi la Kupiga Marufuku Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Mahojiano ya Pekee—Wataalamu Wapinga Tishio la Urusi la Kupiga Marufuku Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hii ni Sehemu ya 2 ya mfuatano wa mahojiano yaliyo na sehemu tatu.

Licha ya kuwa rais Vladimir Putin karibuni alipitisha marekebisho kwenye katiba yaliyopinga kupiga marufuku maandishi matakatifu, wenye mamlaka nchini Urusi wanajaribu kupiga marufuku Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya iliyochapishwa na Mashahidi wa Yehova, na kuiita yenye “msimamo mkali.” Wanaposubiri kesi hiyo iendelee, baada ya mahakama kuagiza Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ichunguzwe na Kituo cha Mafunzo ya Utaalamu wa Masuala ya Utamaduni na Jamii cha Moscow, tulifanya mahojiano na wasomi wa dini, siasa, na sosholojia, na vilevile wataalamu wa masomo kuhusu Muungano wa Sovieti na baada ya muungano huo.

Wasomi wa Biblia wana maoni gani kuhusu Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya na kuhusu kazi ya utafsiri ya Mashahidi wa Yehova?

  • Dakt. Ringo Ringvee

    Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ni kama tafsiri zote zinazojitahidi kuelewa na kufafanua maana kwa kushikamana kabisa na lugha ya awali. Tafsiri zote zinazochapishwa na mashirika ya kidini yanafuata mtindo fulani wa imani yao, na Tafsiri ya Ulimwengu Mpya inafanya hivyo pia, kwa mfano inatumia jina “Yehova” kila mahali, lakini hilo halimaanishi kwamba ni tafsiri mbaya. Katika mwaka wa 2014, Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ilichapishwa katika Kiestonia. Ilizungumziwa sana na watafsiri wengine wa Biblia katika Kiestonia. Walioichunguza walitoka dini mbalimbali za Kikristo na kiwango tofauti cha elimu, na ilionwa inaeleza mambo wazi na inaburudisha. Mwishowe, Tafsiri ya Ulimwengu Mpya katika Kiestonia ilipewa tuzo ya tatu katika kura iliyopigwa mwaka wa 2014 Tuzo la Mwaka Kuhusu Lugha, iliyotolewa na Wizara ya Utafiti na Elimu.”—Dakt. Ringo Ringvee, mshauri, Masuala ya Kidini, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Estonia; profesa wa extraordinarius of comparative religion, Theological Institute of the Estonian Evangelical Lutheran Church, Estonia  

  • Dakt. Roman Lunkin

    “Kati ya wasomi wa masomo ya kidini, hakuna shaka kwamba Mashahidi wa Yehova wanatangaza viwango na kanuni zilizo katika Biblia. Mashahidi wa Yehova wanajulikana kuwa watafsiri wazuri wa Biblia.”—Dakt. Roman Lunkin, mkuu wa Kituo cha Dini na Jamii katika Taasisi ya Ulaya, Chuo cha Sayansi cha Moscow; rais wa Muungano wa Wataalamu wa Dini na Sheria, Urusi

  • Dakt. Ekaterina Elbakyan

    “Inajulikana wazi kwamba leo kuna tafsiri nyingi za Biblia, kuanzia tafsiri ya Agano la Kale ya Septuajinti katika Kigiriki na kufikia tafsiri za Biblia katika lugha za kisasa kutia ndani Kirusi. Bila shaka, kila tafsiri ina ladha yake kwa sababu ya matumizi ya kila lugha. Hata hivyo, jambo kuu ni kwamba maana ya lugha ya awali haipaswi kubadilika katika kila tafsiri ya Biblia, haidhuru imetafsiriwa jinsi gani. Kwa maoni yangu, Tafsiri ya Ulimwengu Mpya imetafsiriwa hivyo.”—Dakt. Ekaterina Elbakyan, profesa wa sosholojia na masuala ya kijamii, Chuo cha Kazi na Mahusiano na Jamii cha Moscow; mshiriki wa Shirika la Ulaya la Masomo ya Dini; mhariri mkuu wa vitabu Westminster Dictionary of Theological Terms, Study of Religion, na Encyclopedia of Religions, Urusi

  • Dakt. Gerhard Besier

    “Tafsiri ya Ulimwengu Mpya imesifiwa ulimwenguni pote na wasomi wa Biblia kutoka jamii mbalimbali za kidini.”—Dakt. Gerhard Besier, profesa aliyestaafu, masomo ya Ulaya, Technische Universität Dresden; mhadhiri, Chuo Kikuu cha Stanford; mkurugenzi, Taasisi ya Sigmund Neumann ya Utafiti Kuhusu Uhuru na Demokrasia, Ujerumani

  • Dakt. Liudmyla Fylypovych

    “Kazi ya kutafsiri Biblia ya Mashahidi wa Yehova si kazi ya waumini wasio na ustadi. Ni kazi kubwa iliyofanywa na watafsiri stadi kwa miaka mingi, wakiomba msaada wa wataalamu bora zaidi wa lugha za awali wanaojulikana. Wataalamu, hasa wasomi wa Biblia, wanaochunguza tafsiri mpya ya Mashahidi wamekata kauli kwamba hakuna tofauti ya maana kati ya tafsiri mpya na za zamani na hawajagundua mambo yoyote mapya yaliyoanzishwa na Mashahidi wa Yehova. Maneno na mawazo magumu au ambayo hayatumiki tena yametafsiriwa katika lugha ya kisasa. Waprotestanti wamekubali tafsiri hiyo bila vipingamizi vyovyote, na kuiona kuwa sehemu ya kazi ya elimu ya Biblia ya ulimwenguni pote.”—Dakt. Liudmyla Fylypovych, profesa, mkurugenzi, Idara ya Historia ya Dini na Practical Studies, Philosophy Institute of the National Academy of Sciences; makamu rais, Muungano wa Ukrainia wa Watafiti wa Dini, Ukrainia

  • Dakt. George D. Chryssides

    “Ni sahihi kusema kwamba Tafsiri ya Ulimwengu Mpya imechambuliwa na wasomi. Hata hivyo, imechambuliwa kwa sababu ya mambo machache kuhusu mafundisho yanayotumiwa katika maandiko kadhaa makuu. Mashahidi wa Yehova hawajaongeza chochote katika Biblia ambacho kitawachochea watu wawe na msimamo mkali au wajeuri. Kinyume cha hilo, sikuzote Mashahidi wameitumia Biblia kuendeleza amani na kupinga jeuri.”—Dakt. George D. Chryssides, mkurugenzi wa zamani wa masomo ya dini, Chuo Kikuu cha Wolverhampton; honorary research fellow in contemporary religion Chuo Kikuu cha York St. John na Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza

  • Prof. Frank Ravitch

    “Naamini kabisa kwamba Biblia hiyo haina ‘msimamo mkali,’ ni tafsiri nzuri. Kwa kuwa ninazungumza lugha kadhaa—Kiingereza, Kijapani, na Kiebrania—ninaelewa jinsi ilivyo vigumu kutafsiri, lakini Tafsiri ya Ulimwengu Mpya haina matatizo mengi ya utafsiri ikilinganishwa na tafsiri nyingine nzuri au machache ikilinganishwa na tafsiri ya kwanza ya King James.”—Profesa Frank Ravitch, profesa wa sheria, mwenyekiti wa Walter H. Stowers ya Sheria na Dini, Chuo Kikuu cha Michigan State, Marekani

  • Dakt. Ain Riistan

    “Hakuna tafsiri kamilifu ya Biblia. Mambo mengi yanasababisha hali iwe hivyo. Kuna maandiko fulani katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ambayo mimi ningetafsiri kwa njia tofauti. Ndivyo ilivyo na tafsiri nyingine zote. Mimi si mtaalamu wa lugha ya Kirusi (ingawa naielewa), hivyo siwezi kuchunguza ubora wa lugha wa tafsiri ya Kirusi. Tafsiri ya Ulimwengu Mpya katika Kiestonia ilipochapishwa mwaka wa 2014, ilipokelewa vizuri na watu kwa ujumla. Hata iliitwa ‘tukio la fasihi la mwaka’ kwa sababu ya ubora na jinsi inavyoeleza mambo wazi katika Kiestonia. Ukifikiria jinsi wanavyotafsiri kwa njia ileile Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ulimwenguni, mwishowe utapata ujumbe uleule kukiwa na tofauti chache tu kwa sababu ya njia ya kila lugha ya kutafsiri. Sidhani kama kuna tofauti kubwa kati ya tafsiri ya Kirusi na Kiestonia. Kwa hiyo, ninaweza kusema kwa uhakika kwamba ni tafsiri nzuri na si hatari au yenye ‘msimamo mkali.’”—Dakt. Ain Riistan, mhadhiri wa Agano Jipya, Shule ya Theolojia na Masomo ya Dini, Chuo Kikuu; profesa mshiriki wa theolojia ya makanisa huru na historia ya dini, Seminari ya Theolojia ya Tartu, Estonia

  • Dakt. Basilius J. Groen

    “Inasikitisha kwamba wengi walio na mamlaka ambao wanaamua kuharibu Biblia za Mashahidi hawajui lolote kuhusu imani wala Maandiko Matakatifu. Bila shaka, Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ni nzuri na bila shaka pia baadhi ya mambo yaliyotafsiriwa yanaweza kubishaniwa, lakini ndivyo ilivyo na tafsiri nyingine pia (kutia ndani tafsiri ya dini yangu, Katoliki).”—Dakt. Basilius J. Groen, UNESCO (Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi, na Tamaduni) Mwenyekiti wa Mawasiliano ya Tamaduni na Dini Mbalimbali ya Ulaya Kusini Mashariki, Chuo Kikuu cha Karl-Franzens; profesa wa liturjia na theolojia takatifu, mkurugenzi wa Taasisi ya Liturjia, Sanaa na Nyimbo za Kikristo, Chuo Kikuu cha Graz, Austria

  • Dakt. Hocine Sadok

    “Kwa maoni yangu nikiwa msomi, wenye mamlaka hawahitaji kuchunguza Tafsiri ya Ulimwengu Mpya. Ni kitabu cha kidini, na wenye mamlaka wa nchi ya kidemokrasia hawapaswi kuingilia. Kudai kwamba Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ni hatari na yenye msimamo mkali ni upuuzi.”—Dakt. Hocine Sadok, mhadhiri wa sheria, mkurugenzi, idara ya Uchumi wa Kijamii na Kisheria, Université de Haute Alsace, Ufaransa

  • Dakt. William Cavanaugh

    “Kwa ujumla, nafikiri wasomi wengi wanaheshimu tafsiri ya Mashahidi wa Yehova ya Biblia, ingawa huenda baadhi yao wakapinga jinsi maneno fulani yametafsiriwa.”—Dakt. William Cavanaugh, profesa wa masomo ya Kikatoliki, mkurugenzi, Kituo cha Ukatoliki Ulimwenguni na Intercultural Theology, Chuo Kikuu cha DePaul, Marekani

Una maoni gani kuhusu serikali ya Urusi kujaribu kupiga marufuku Biblia iliyotafsiriwa na Mashahidi wa Yehova kwa sababu inaonwa kuwa yenye “msimamo mkali”?

  • “Ninafikiri kwamba kupiga marufuku Tafsiri ya Ulimwengu Mpya nchini Urusi kunapingana na marekebisho ya Kifungu cha 3 cha Sheria kuhusu Msimamo Mkali iliyotiwa sahihi na Bw. Putin katika mwaka wa 2015, kwa sababu sheria hiyo haisemi chochote kuhusu tafsiri za maandishi matakatifu. Kama tujuavyo, hakuna kitabu chochote kitakatifu (Biblia, Kurani, Torati, na Kangyur) ambacho kiliandikwa katika Kirusi au katika Kislavoni cha kanisa, vitabu hivyo vinatafsiriwa ili vitumiwe nchini Urusi. Kuna tafsiri nyingi sana za vitabu hivyo. Sheria haitaji kihususa ni tafsiri zipi za vitabu vitakatifu ambazo zinaweza kutumiwa katika Jamhuri ya Urusi na zipi ambazo zimepigwa marufuku. Kwa hiyo, tafsiri yoyote inaweza kutumiwa, na kupiga marufuku tafsiri yoyote ni kinyume cha sheria.”—Dakt. Elbakyan, Urusi

  • Dakt. Derek H. Davis

    “Kupiga marufuku maandishi yoyote ya kidini ni jambo lisiloeleweka, lakini Biblia ina historia ndefu ya kutumiwa kwa makusudi matakatifu na vikundi vinavyojulikana na kuheshimiwa kama Mashahidi wa Yehova. Kuna tafsiri nyingi za Biblia zinazotumiwa na vikundi vingine vya Kikristo ambazo hazijapigwa marufuku; hivyo inaonekana wazi kwamba nchi ya Urusi inawashambulia Mashahidi wa Yehova bali si Biblia yao.”—Dakt. Derek H. Davis, wakili, mkurugenzi wa zamani wa Taasisi ya J.M. ya Masomo ya Kanisa na Dini, Chuo Kikuu cha Baylor, Marekani

  • Dakt. Jeffrey Haynes

    “Kwa kuwa nchi ya Urusi ni mshiriki wa ICCPR [Maagano ya Kimataifa ya Haki za Raia na Siasa], kujaribu kupiga marufuku Biblia kama hiyo ni kinyume cha uhuru wa ibada.”—Dakt. Jeffrey Haynes, profesa wa siasa, mkurugenzi wa Kituo cha Masomo ya Dini, Mizozo na Kushirikiana, Chuo Kikuu cha London Metropolitan; mwenyekiti, Muungano wa Ulaya wa Kikundi cha Utafiti wa Dini na Siasa, Uingereza

  • “Nchini Urusi, ambako maoni ya kidini yamekuwa sehemu kubwa ya utamaduni na ukuzi, wenye mamlaka wameanza kuona dini kuwa haitegemeki na wanaishuku. Ni nani ambaye angewazia kwamba kutunga sheria ya kulinda maandishi fulani matakatifu kungefanya maandishi mengine matakatifu yapigwe marufuku? Wakati huohuo, mbinu ya kutenganisha vitu vitakatifu na visivyo vitakatifu imebuniwa. Na watu wa kwanza kuathiriwa ni Mashahidi wa Yehova, pamoja na tafsiri yao ya Biblia, na hilo halishangazi kwa sababu kumekuwa na kampeni ya kisiasa dhidi yao tangu mwaka wa 2009.”—Dakt. Lunkin, Urusi

  • Prof. William S. B. Bowring

    “Nina uhakika kwamba Urusi imekuwa tayari kupiga marufuku Tafsiri ya Ulimwengu Mpya kwa sababu imechapishwa na Mashahidi wa Yehova. Bila shaka, mtazamo huo haupatani na akili hata kidogo, kwa sababu Biblia ni Biblia, kama vile Kurani ni Kurani. Sina sababu yoyote ya kushuku kwamba Tafsiri ya Ulimwengu Mpya haijatayarishwa kwa uangalifu mwingi.”—Profesa William S. B. Bowring, profesa wa sheria, mkurugenzi wa Haki za Kibinadamu LLM/MA, Shule ya Sheria ya Birkbeck, Chuo kikuu cha London; mwanasheria wa Middle Temple and Gray’s Inn, Uingereza

  • Dakt. William Schmidt

    “Sijasadikishwa kwamba marekebisho ya sheria yaliyofanywa hayahusu Mashahidi wa Yehova na dini nyingine ndogo na mpya. Hali hiyo inaashiria kwamba kuna tatizo kati ya siasa na sheria, kukosa kuelewa na kuchunguza mahusiano kati ya dini na serikali na kuiona kuwa aina ya pekee ya sehemu ya kiraia na siasa. Katika nchi hii [Urusi] hakuna kanuni zilizowekwa wazi kuhusiana na sera za serikali (makubaliano, programu) katika mahusiano ya dini na serikali. Huko kutoeleweka kwa mahusiano ya siasa na sheria kunachochea kuingiliwa na serikali na kupotoshwa kwa sheria na pia kunadhuru masilahi ya dini na mahusiano ya dini kwa ujumla. Kila dini inaheshimu sana maandiko yake matakatifu. Maandishi hayo yanatokeza kanuni zao za kidini.”—Dakt. William Schmidt, mhariri mkuu, Eurasia: the spiritual traditions of the peoples; profesa, Mahusiano ya Taifa na Jamhuri, Chuo cha Urusi cha Rais cha Uchumi wa Kitaifa na Usimamizi wa Umma (RANEPA), Urusi

  • “Siwezi kufikiria sababu yoyote nzuri ambayo ingefanya wenye mamlaka nchini Urusi wabague Tafsiri ya Ulimwengu Mpya. Hakuna chochote chenye msimamo mkali katika tafsiri ya Biblia ya Mashahidi. Ni tafsiri inayolingana na maandishi ya Kiebrania na Kigiriki, na ina mambo yaleyale yaliyo katika tafsiri nyingine zinazokubaliwa.”—Dakt. Chryssides, Uingereza

  • Dakt. Thomas Bremer

    “Inaonekana kwamba wenye mamlaka nchini Urusi walipoamua kwamba Mashahidi wa Yehova ni tengenezo lenye msimamo mkali, wanafanya yote wawezayo kulingana na uamuzi huo—uamuzi ambao mtu anaweza na anapaswa kuuona kuwa kosa.”—Dakt. Thomas Bremer, mtafiti wa zamani wa sheria, Kituo cha Jordan cha Masomo ya Juu cha Urusi, Chuo Kikuu cha New York; profesa wa theolojia ya dini mbalimbali, masomo ya dini za mashariki na masomo ya amani, Chuo Kikuu cha Münster, Ujerumani

  • Dakt. Jim Beckford

    “Hilo halinishangazi. Inaambatana na sera na mazoea ya Muungano wa Sovieti dhidi ya vikundi vidogo vya kidini. Lakini badala ya kupiga marufuku utendaji mwingi wa kidini, nchi ya Urusi imechagua kuwadhibiti kwa sheria zinazosemwa kuwa zinalinda amani ya umma na kuzuia msimamo mkali.”—Dakt. Jim Beckford, mwanasheria katika Chuo cha Uingereza; profesa aliyestaafu wa sosholojia, Chuo Kikuu cha Warwick; rais wa zamani wa Jumuiya ya Uchunguzi wa Kisayansi wa Dini (Marekani), Uingereza

  • Dakt. Dmitry Uzlaner

    “Wazo la sheria hiyo mpya kuhusiana na dini ni hili: kuna dini kuu (nchini Urusi—kwanza kanisa la Othodoksi, lakini pia Uislamu, dini ya Kiyahudi, dini ya Budha) na dini ndogo (kwa mfano, Mashahidi wa Yehova). Kulingana na wazo hilo, dini kuu zinapata mapendeleo fulani kutoka serikalini kwa sababu zinaonwa kuwa zina matokeo mazuri katika jamii ya Urusi, kwa upande mwingine, dini ndogo zinapaswa kudhibitiwa kwa sababu zinaeneza viwango na mtindo mpya wa maisha katika jamii ya Urusi. Hiyo ndiyo sababu Mashahidi wa Yehova na dini nyingine ndogo hawatanufaika na sheria mpya zinazotetea hisia za waamini au zinazopinga kupigwa marufuku kwa vitabu vinne vitakatifu. Hata hivyo, ninaamini kwamba Mashahidi wa Yehova pamoja na dini nyingine ndogo wanapaswa kufurahia uhuru wa ibada kotekote katika Jamhuri ya Urusi.”—Dakt. Dmitry Uzlaner, mtafiti, Shule ya Moscow ya Jamii na Sayansi ya Uchumi; mhariri mkuu wa State, Religion and Church, Urusi

  • Bw. Eric Rassbach

    “Mashahidi wa Yehova wanapaswa kupewa haki kamili ya kutumia tafsiri yao ya Biblia. Kupata Maandiko ni sehemu muhimu ya haki ya uhuru wa kidini, na kuna tafsiri nyingi za Biblia zinazohusianishwa na imani mbalimbali. Kusema kwamba tafsiri ambayo Mashahidi wa Yehova wanapenda ina ‘msimamo mkali’ ni kuwakandamiza Mashahidi wa Yehova wasiishi kulingana na imani yao.”—Bw. Eric Rassbach, naibu wakili, Hazina ya Becket ya Uhuru wa Kidini, Marekani

  • Dakt. Emily B. Baran

    “Kupiga marufuku tafsiri yoyote ya Biblia ni kupinga uhuru wa kidini, hasa ikiwa unashambulia dini fulani ndogo na kuingilia ufafanuzi wao wa Maandiko. Haipaswi kuwa kazi ya serikali kushiriki mahojiano ya kidini kuhusu usahihi wa tafsiri fulani ya Biblia.”—Dakt. Emily B. Baran, profesa msaidizi wa historia ya Urusi na Ulaya Mashariki, Chuo Kikuu cha Jimbo la Middle Tennessee, Marekani

  • Sir Andrew Wood

    “Kwa sasa kuna uhusiano mkubwa kati ya serikali ya Urusi na Kanisa Othodoksi la Urusi (ROC)—ambayo kama vile nchi ya Urusi halikubaliani na Waothodoksi wa nchi nyingine. Ninadhani kwamba ROC haiwezi kukubali Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ya Mashahidi wa Yehova ihesabiwe kati ya vitabu vitakatifu vilivyokubalika vya dini kuu nne: dini ya Kiyahudi, Ukristo, Uislamu, na dini ya Budha. Njia ya kufikiri iliyokita mizizi ya wenye mamlaka ingemaanisha kwamba wao pia wangejaribu kudhibiti uvutano wa wale wanaotegemea maandishi na imani yao, na jitihada zao za kuwaeleza wengine maoni yao. Ukweli wa kwamba Mashahidi wa Yehova wamekuwepo nchini Urusi tangu siku za Maliki haungebadili mtazamo huo, kama tunavyoona waziwazi kulingana na jinsi ambavyo wamewanyanyasa kwa miaka mingi.”—Sir Andrew Wood, wakili wa programu ya Urusi na Eurasia, Chatham House, Taasisi ya Kifalme ya Masuala ya Kimataifa; balozi wa zamani wa Uingereza nchini Urusi (1995-2000), Uingereza

  • “Sababu ya kupiga marufuku Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya na pia vitabu vingine, ni kudhibiti maisha ya kiroho nchini Urusi na kutafsiriwa kwa Maandiko Matakatifu. Zaidi ya tafsiri hiyo ya Mashahidi wa Yehova, Kanisa Othodoksi la Urusi halitambui tafsiri nyingine, kutia ndani Vulgate, tafsiri ya Kilatini ya Wakatoliki. Nao Wakatoliki hawatambui Biblia ya Walutheri.”—Dakt. Fylypovych, Ukrainia

  • Dakt. Zoe Knox

    “Marekebisho ya sheria kuhusu msimamo mkali, yanaweza kuonekana kuwa yanalinda Biblia isipotoshwe au kupigwa marufuku. Inaonekana kuwa si maandiko matakatifu yaliyolindwa, bali ni tafsiri hususa. Tafsiri ya Ulimwengu Mpya zilichukuliwa si kwa sababu ya mambo yaliyomo bali kwa sababu ya chanzo chake, yaani, Mashahidi wa Yehova. Mashahidi wanaonwa kuwa tisho kwa dini kuu za Urusi kwa njia mbalimbali, kwanza kwa sababu ya jinsi wanavyoishi, mipango ya kutaniko, imani yao, na tafsiri yao ya Biblia. Isitoshe, wanaonwa kuwa wameathiriwa na Wamarekani. Kwa ujumla, wanaonwa kuwa hawana msingi wowote wa kisheria wa kuwa nchini Urusi.”—Dakt. Zoe Knox, profesa msaidizi wa historia ya kisasa ya Urusi, Chuo Kikuu cha Leicester, Uingereza

  • Bi. Catherine Cosman

    Kuchukuliwa kwa Biblia za Mashahidi wa Yehova kwa wingi kunaonyesha kwamba serikali ya Urusi inaona tafsiri fulani tu za Biblia kuwa ‘zinakubalika’ kisheria, jambo lingine linaloingilia uhuru wa ibada. Serikali ya Urusi inapaswa kurekebisha kabisa sheria yao kuhusu msimamo mkali, kama ambavyo Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu, Tume ya Venice, na Shirika la Usalama na Ushirikiano wa Ulaya zilipendekeza.”—Bi. Catherine Cosman, mchunguzi wa sera (Ulaya na nchi zilizokuwa sehemu ya Muungano wa Sovieti), Tume ya Marekani ya Uhuru wa Ibada wa Kimataifa (USCIRF), Marekani

  • “Siungi mkono kupigwa marufuku kwa tafsiri za vitabu vitakatifu. Kujaribu kudhibiti imani kunahusiana sana na uhusiano wa karibu uliopo kati ya Kanisa Othodoksi la Urusi na uzalendo wa nchi ya Urusi. Warusi wengi walihangaika walipoona ongezeko la watu waliotaka kuwageuza watu imani baada ya kuanguka kwa Muungano wa Sovieti. Wengi walihisi kwamba Kanisa Othodoksi la Urusi lilihitaji muda wa kupumua baada ya utawala wa Kikomunisti.”—Dakt. Cavanaugh, Marekani

  • Dakt. John A. Bernbaum

    “Ninatetea sana haki ya Mashahidi ya kuwa na tafsiri yao ya Biblia ikitegemea kujifunza neno la Mungu. Hakuna mamlaka inayopaswa kuingilia kutafsiriwa au kuchapishwa kwa machapisho ya kidini. Uhuru wa ibada ni haki ya msingi na wenye mamlaka wanapaswa kuunga mkono maoni tofauti-tofauti ya kidini.”—Dakt. John A. Bernbaum, rais, Taasisi ya Urusi na Marekani (Moscow), Marekani

  • Bw. Alexander Verkhovsky

    “Hakuna dalili zozote za msimamo mkali katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya. Tunaona mnyanyaso dhidi ya Mashahidi wa Yehova nchini Urusi na kupigwa marufuku kwa machapisho yao na jamii zao kuwa ubaguzi wa kidini.”—Alexander Verkhovsky, msimamizi, Kituo cha SOVA cha Habari na Utafiti (shirika la Kirusi jijini Moscow lisilo la kibiashara linalofanya utafiti kuhusu uzalendo, ubaguzi, mahusiano kati ya makanisa na jamii, na siasa zenye msimamo mkali), Urusi

  • Dakt. Régis Dericquebourg

    “Biblia iliyotafsiriwa na Mashahidi wa Yehova si kitabu kinachopingana kisiasa na jamii ya Urusi. Ni tafsiri kama nyingine tu ya Biblia. Sioni jinsi Biblia ya Mashahidi wa Yehova inaweza kuwa yenye ‘msimamo mkali.’ Ingekuwa yenye msimamo mkali, ingepigwa marufuku katika nchi nyingine zinazohofia msimamo mkali wa kisiasa. Lakini haijapigwa marufuku katika nchi nyingine za kidemokrasia.”—Dakt. Régis Dericquebourg, mwanasosholojia, profesa msaidizi wa dini za karibuni, Antwerp FVG, Belgium

  • Dakt. Mark R. Elliott

    “Inasikitisha kwamba mara nyingi nchi ya Urusi inapuuza haki za kibinadamu za kabila na dini ndogo. Ukweli ni kwamba ufafanuzi wa maofisa Warusi ambao ni wabaguzi kuhusu ‘msimamo mkali,’ unaweza kutumiwa kuhusiana na Biblia yoyote ya Kikristo, kutia ndani Tafsiri ya Othodoksi ya Synodal toleo la 1876.”—Dakt. Mark R. Elliott, mhariri mwanzilishi, East-West Church and Ministry Report, Chuo Kikuu cha Asbury, Kentucky, Marekani

  • “Urusi ingefurahi ikiwa Ukristo ungewakilishwa na Kanisa Othodoksi la Urusi na machapisho yake. Kwa sasa vikundi vingine vya kidini tofauti na Mashahidi wa Yehova wanasumbuliwa sana nchini Urusi—jambo ambalo linaturudisha katika enzi za maliki. Mashirika ya kidini hasa yaliyo na wafuasi wengi nchini Marekani hayakubaliwi nchini Urusi.”—Dakt. Besier, Ujerumani

  • Dakt. Silvio Ferrari

    “Kupiga marufuku Biblia ya Mashahidi wa Yehova ya Kirusi, ambayo ilisemekana kuwa yenye ‘msimamo mkali,’ ni jambo ambalo halijawahi kutokea barani Ulaya. Kwa upande mwingine, ingawa ni sawa kutopiga marufuku ‘Biblia, Kurani, Tanakh, na Kangyur, maandiko yaliyomo, na manukuu kutoka vitabu hivyo,’ inaonyesha ubaguzi kati ya vitabu hivyo vitakatifu na vitabu vya dini nyingine. Kwa kuwa hakuna uthibitisho wowote kwamba vitabu vingine vina ‘msimamo mkali’ kuliko vya kwanza vinne, ni wazi kwamba hakuna usawaziko.”—Dakt. Silvio Ferrari, rais, International Consortium for Law and Religious Studies; mhariri msaidizi, Oxford Journal of Law and Religion; co-founder, European Consortium for Church and State Research; profesa wa sheria na dini na kanuni za dini, Chuo Kikuu cha Milan, Italia

  • “Ni hatari sana serikali zinapoanza kuamua ni tafsiri zipi za maandishi ya kidini zilizo ‘sahihi’ au zinazoruhusika. Hilo si jukumu la serikali, bali ni jambo la kujadiliwa na kuzungumziwa kati ya waumini wa dini. Kuna tofauti nyingi na ufafanuzi mbalimbali wa vitabu vitakatifu, kutia ndani Biblia, na ni kuvunja kanuni za kimataifa za uhuru wa kidini kwa serikali kuwalazimishia waumini tafsiri fulani kuwa kweli ya kidini.”—Dakt. Carolyn Evans, mkuu wa Harrison Moore Chair of Law, Shule ya Sheria ya Melbourne; mhariri msaidizi, Religion and International Law; mhariri msaidizi, Law and Religion in Historical and Theoretical Perspectives, Australia

  • Dakt. Javier Martínez-Torrón

    “Sioni sababu yoyote katika sheria ya kimataifa ya Ulaya kupiga marufuku vitabu vitakatifu vya dini yoyote, ilimradi haienezi chuki au kuharibu amani. Kutoa hukumu juu ya usahihi wa dini au maandiko si kazi ya serikali.”—Dakt. Javier Martínez-Torrón, profesa wa sheria, msimamizi, Idara ya Sheria na Dini, Chuo Kikuu cha Complutense cha Sheria, Hispania

  • Prof. Robert C. Blitt

    “Kama ambavyo ICCPR imesema kwa muda mrefu, ukweli wa kwamba dini fulani ‘inaonwa kuwa kubwa. . . haupaswi kufanya haki za wengine zivunjwe.’ Kwa hiyo kupendelea dini fulani ‘kubwa’ na wakati huohuo kudhibiti dini nyingine ‘ndogo’ ni kubagua mtu kwa msingi wa dini au imani na ni kinyume cha uhakikisho wa ICCPR kwamba vikundi vyote vitalindwa kwa njia ileile.”—Profesa Robert C. Blitt, profesa wa sheria, Chuo Kikuu cha Tennessee; mtaalamu wa zamani wa sheria za kimataifa, Tume ya Marekani Kuhusu Uhuru wa Kidini Kote Duniani (USCIRF), Marekani

  • “Ikiwa dini kubwa hazibaguliwi na wenye mamlaka nchini Urusi, inaonekana inapambana dhidi ya uvutano wa nje ya nchi bali haipambani na dini. Hali ya sasa ya kisiasa nchini Urusi inachochea tofauti kati yao na maoni au vikundi vyovyote ambavyo vingeweza kuleta vurugu kwa njia yoyote, iwe ni vya kisiasa au kidini. Wenye mamlaka nchini Urusi wangependelea ikiwa hakungekuwa na uvutano wowote wa nchi za nje katika eneo lao. Wanaamini kwamba dini ndogo za hivi karibuni kama Mashahidi wa Yehova zinaendeleza uvutano wa nchi za nje nchini Urusi. Kwa maoni yao, Mashahidi wa Yehova wanaonwa na mamlaka za Urusi kuwa kikundi kutoka bara la Amerika Kaskazini, na hivyo kuwa na uvutano mbaya nchini humo. Hivyo, uhalali si ndilo suala kwa wenye mamlaka wa Urusi. Hatua ya kisheria iliyochukuliwa ni kama kifuniko tu.”—Dakt. Sadok, Ufaransa

  • Dakt. Marco Ventura

    “Serikali zimeingilia na kuathiri sana haki ya dini, taasisi, na mashirika kutokeza, kuingiza nchini, na kusambaza machapisho ya kidini, kwanza imeathiri vitabu vitakatifu, kama vile Biblia Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ya Mashahidi wa Yehova. Kuhusiana na hilo, marufuku hiyo ya wenye mamlaka imefikia kiwango cha kupinga haki ya msingi ya uhuru wa dini kuwa na tafsiri wanayopenda ya Maandiko, hasa kuhusiana na kutafsiri na kufafanua. Kwa kufanya hivyo, mamlaka nchini Urusi zimekosa kutimiza jukumu lao la kutounga mkono na kutobagua kuhusiana na masuala ya kweli na vitabu vya kidini.”—Dakt. Marco Ventura, profesa wa sheria na dini, Chuo Kikuu cha Siena; msimamizi, Kituo cha Masomo ya Kidini katika Taasisi ya Bruno Kessler; mtafiti, Kituo cha Droit, Religion, Entreprise et Société (DRES), Chuo Kikuu cha Strasbourg (Ufaransa), Italia

  • “Kwa maoni yangu, hilo limetokana na msimamo wenye mashaka wa uhuru wa ibada nchini Urusi. Si Mashahidi wa Yehova tu ambao wamesumbuliwa na wenye mamlaka nchini Urusi katika siku za karibuni. Hata hivyo, ninaona kwamba kupiga marufuku tafsiri ya Biblia ni jambo la kusikitisha sana. Ukipiga marufuku tafsiri moja, basi tafsiri nyingine zote ziko hatarini. Marekebisho yangetumiwa kuhusiana na maandishi katika lugha ya awali tu (kwa mfano, Biblia—Kiebrania, Kiaramu, Kigiriki). Pia, namna gani tafsiri za hati? Ukweli huo peke yake unaonyesha ubaguzi kuhusiana na marufuku hiyo.”—Dakt. Riistan, Estonia

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu, 1-718-560-5000

Urusi: Yaroslav Sivulskiy, simu, 7-812-702-2691