JANUARI 24, 2020
URUSI
Mahakama ya Urusi Yawatoza Faini Ndugu Markin na Ndugu Trofimov. Hawataenda Gerezani
Ijumaa, Januari 24, 2020, Mahakama ya Wilaya ya Polyarny huko Murmansk iliwahukumu Ndugu Roman Markin na Viktor Trofimov. Ndugu Markin alitozwa faini ya rubo 300,000 (dola 4,858 za Marekani), na Ndugu Trofimov, rubo 350,000 (dola 5,668 za Marekani). Ingawa hatufurahi kwamba ndugu zetu wapendwa wamehukumiwa, tunashukuru kwamba hawatatumikia kifungo cha gerezani.