Masharti ya Utumiaji
Programu hii imekusudiwa kukusaidia kujifunza mengi zaidi kumhusu Mungu, Biblia, na Mashahidi wa Yehova. Unaweza kusoma, kutazama, na kupakua habari zinazokuvutia. Tungependa wote wanufaike kutokana na programu hii, ila hakuna mtu yeyote anayeidhinishwa kuchukua habari zozote na kuziweka katika programu au tovuti nyingine. Unaruhusiwa kuwaonyesha wengine mambo uliyojifunza kwa kuwaelekeza jinsi ya kupakua Programu hii.
Masharti haya ya Utumiaji (“Mkataba”) yanatambulika kisheria kama mkataba kati ya Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc., ambayo ni shirika lisilo na kusudi la kutengeneza faida (“Watchtower,” “sisi,” au “yetu”) na wewe (“wewe”) ambaye ni mtumiaji wa programu hii.
Ikiwa kutakuwa na habari zilizoongezwa, zilizoboreshwa, mambo mapya, na/au mabadiliko fulani katika Programu hii, yote hayo yatakuwa chini ya Mkataba huu. Tuna uwezo wa kufanya mabadiliko, kurekebisha, au kufuta Mkataba huu muda wowote ule. Katika Mkataba huu unakubali kwamba marekebisho hayo, mabadiliko yoyote, au Mkataba unapovunjwa kutaathiri jinsi unavyotumia programu hii. Ikiwa utaendelea kutumia na/au kuwa na programu hii baada ya mabadiliko ya aina hiyo itaashiria kwamba unakubaliana na marekebisho yaliyofanywa.
Ikiwa hutendi kupatana na Mkataba huu hata iwe ni kwa sehemu tu basi tunaweza kuubatilisha (bila kukupatia taarifa). Hutaweza kufungua na/au hutakuwa na kibali cha kutumia Programu hii. Hivyo, unakubali kwamba tunaweza kukufungia na/au kufuta kibali chako cha kufungua Programu hii bila kukupatia taarifa, kwa sababu yoyote au bila sababu yoyote.
UNAKUBALI KUTENDA KUPATANA NA MKATABA HUU UNAPOBOFYA “KUBALI” KATIKA MKATABA HUU AU KWA KUPAKUA, KUSAKINISHA, KUNAKILI, AU KWA KUTUMIA PROGRAMU HII. ILI UPATE KIBALI CHA KUITUMIA NI LAZIMA UKUBALIANE NA MKATABA HUU. IKIWA HUTAKUBALI KUTENDA KUPATANA NA MASHARTI YALIYO KATIKA MKATABA HUU, HUPASWI KUSAKINISHA, KUNAKILI, AU KUTUMIA PROGRAMU HII NA NI LAZIMA UFUTE NAKALA ZOTE ZA PROGRAMU HII KATIKA KIFAA CHAKO MARA MOJA.
1. KUPEWA KIBALI. Programu hii haiuzwi, tunakupa kibali ili uitumie kupatana na masharti yaliyo katika Mkataba huu. Maadamu ulitenda kupatana na masharti yote yaliyomo, na unaendelea kufanya hivyo, sasa Watchtower inakupa kibali kinachoweza kubatilishwa wakati wowote, chenye mipaka, ambacho huwezi kumhamishia mtu mwingine, ambacho huwezi kumpa mtu mwingine leseni atumie, na tunakupa idhini bila ubaguzi ya kuifungua, kuitumia, kuisakinisha, kuitekeleza, kuihifadhi, kuionyesha, kuwa na Programu hii katika vifaa unavyomiliki au unavyotumia kwa kufanya mambo yaliyoidhinishwa katika Mkataba huu au kupatana na maagizo yanayotoka Watchtower katika maandishi. Masharti yaliyo katika Mkataba huu yataendelea kutumika hata Programu hii inapoboreshwa na Watchtower na kuchukua nafasi ya toleo hili na/au ili kuongezea mambo ambayo hayapo kwa sasa, isipokuwa tu ikiwa toleo la aina hiyo litakuwa na masharti na kibali tofauti. Baadhi ya sehemu katika Programu zina kibali inayomruhusu mtumiaji kufanya marekebisho au zina vibali kutoka kwa mtu wa tatu. Ikiwa masharti ya sehemu hizo yanatofautiana na masharti yaliyo katika Mkataba huu basi vibali hivyo vitatumika kuhusiana na sehemu husika tu.
2. KUIDHINISHA MATUMIZI NA UMILIKI; HABARI ZINAZOANDALIWA NA MTU WA TATU, ALAMA ZA USAJILI. Watchtower inamiliki Programu hii na ina haki ya kuamua jinsi inavyotumiwa hata inapohusu mambo ambayo hayajatajwa katika Mkataba. Mkataba huu unalindwa na haki miliki (copyright) pamoja na sheria nyingine za mali miliki na mikataba mingine. Inapohusu Mkataba huu kati yako na Watchtower, Watchtower inamiliki haki ya kuidhinisha matumizi yako, hati, na ina haki zote juu ya programu hii. Isipokuwa iwe imeonyeshwa (i) habari zote zinazopatikana katika Programu hii na (ii) alama zinazotumiwa na Watchtower katika Programu hii ni mali ya Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania (“Watch Tower”). Ili kusiwe na shaka, mali zote za kitaaluma za na mtu wa tatu na zinazopatikana katika programu yetu zinaendelea kuwa mali ya mtu huyo wa tatu na si za Watchtower au Watch Tower. Hivyo, unakubali kwamba hutaondoa, hutaficha, au kubadilisha haki miliki, alama zinazotumiwa na Watchtower, au mali yoyote ya kitaalumu au kitambulisho cha chanzo (source identifier) iliyo katika Programu (kutia ndani zilizoorodheshwa kwenye sifa za leseni huria) (“Sifa”). Sisi hatuna mamlaka juu ya habari yoyote ambazo ni mali ya mtu yeyote wa tatu (ikiwa ipo) katika programu hii.
Adobe, nembo ya Adobe, Acrobat, na nembo ya Acrobat ni alama za kibiashara zinazomilikiwa na Adobe Systems Incorporated. iTunes na iPod ni nembo za kibiashara zinazomilikiwa na Apple Inc. Microsoft, nembo ya Microsoft, na programu zinazotoka Microsoft kama vile Microsoft Office na Microsoft Office 365, ni nembo za kibiashara zinazomilikiwa na Microsoft Inc. Android ni nembo ya kibiashara ya Google LLC. Roboti ya Android inatokezwa upya au kurekebishwa na Google kutokana na ubunifu na usambazaji wa Google kwa kutumia masharti yaliyofafanuliwa kwenye Creative Commons 3.0 Attribution License (https://creativecommons.org/licenses/by/3.0/us/). Alama nyingine zote za usajili na alama za usajili zilizosajiliwa zinawakilisha kampuni inayozimiliki.
3. MIPAKA YA UTUMIAJI. Programu hii imebuniwa kwa kusudi la kutumiwa na mtu binafsi kama Mkataba huu unavyoonyesha isipokuwa tu mtu aruhusiwe na Watchtower katika maandishi. Unakubali kwamba wewe binafsi hutafanya mambo yafuatayo na wewe hutaruhusu mtu mwingine yeyote iwe moja kwa moja au la, kufanya mambo yafuatayo: (a) kukodisha, kukopa, kuuza, kuhamisha, kukabidhi, kusambaza, kutokeza upya, kunakali, kuchapisha, kugawa haki za kuitumia, kuiga au kueneza ustadi uliotumiwa, kuchukua sehemu za Programu au Programu nzima, (b) kubadili uhandisi uliotumiwa, kutoa kodi tofauti, kubadili, kuiga, kutafsiri au kuchanganua sehemu yoyote ya Programu kutia ndani ubuni uliotumika, mfumo na muundo, au kutokeza Programu nyingine kwa kutumia Programu hii, bidhaa au huduma zilizomo (isipokuwa tu ikiwa vizuizi hivi vimebatilishwa na sheria au ikiwa kibali kinaruhusu matumizi ya huduma nyingine zinazotumiwa katika Programu), (c) kuondoa au kubadili alama yoyote ya usajili, majina ya usajili, majina ya huduma, michoro, miundo, nembo, vichwa vya kurasa, alama za kubofya, maandishi, alama za kibiashara, mwonekano wa bidhaa au haki yoyote tunayomiliki kilicho kwenye Programu (kutia ndani alama za “JW” na “JW.ORG”) au alama nyingine zozote za usaijli, (d) kutumia jina, nembo, alama ya usajili au kitu kingine kinachotutambulisha kana kwamba ni binafsi au ya kampuni fulani hivi kwamba mtu anaweza kudhani mtu huyo binafsi au kampuni hiyo ndio inayosambaza Programu yetu, au (e) kutumia kifaa chochote, au programu nyingine ya kompyuta kuingilia utaratibu wowote wa Programu, (f) kusajili, kujaribu kusajili, au kumsaidia mtu mwingine kusajili alama za usajili, nembo, majina tunayomiliki, au kumsaidia mtu mwingine yeyote kusajili alama za usajili, nembo, majina tunayomiliki, na kitu kingine chochote kinachowakilisha bidhaa zetu, haki miliki, au haki yoyote inayomilikiwa na Watchtower, Watch Tower, au shirika lolote linalohusiana nayo; (g) kuondoa, kuficha, au kubadili haki miliki, alama za usajili, au haki yoyote tunayomiliki inayopatikana sehemu yoyote katika Programu, (h) kumpa mtu mwingine, kuhifadhi, au kushughulikia habari za kiafya zilizo chini ya sheria ya HIPAA ya Marekani, au (i) kutumia Programu kwa njia nyingine ambayo haijazungumziwa katika Mkataba huu. Unakubali kutii Masharti ya Huduma ya Google, Google APIs Terms of Service (na kutovunja masharti yoyote kimakusudi).
Ingawa umekubali kutii vizuizi vilivyotajwa hapo juu, unaweza kuomba ruhusa hususa ili kupata habari za kitaalamu kuhusu Programu yetu, ili kuwa na uwezo wa kubadili au kuiboresha, ili kubadili mfumo wa codes, au kutafsiri sehemu ya Programu au Programu yote bila kudhibitiwa na jinsi ilivyo, mifumo yake, au muundo wake, kazi inayofanya, au huduma zinazotolewa. Watchtower itaamua ni nani anayeweza kupewa ruhusa. Ikiwa ungependa kupewa ruhusa hizi hususa, tafadhali wasiliana na Watchtower kwa kutuma barua-pepe DeveloperSupport@jw.org
Ikiwa mmojawapo kati yako na Watchtower hafuati kwa ukaribu masharti yaliyo katika Mkataba huu au kutimiza haki au matakwa yaliyoidhinishwa hapa na msamaha utolewe, hiyo haitapunguza wajibu uliowekwa na Mkataba huu. Msamaha mmoja unapotolewa haimaanishi msamaha mwingine utatolewa baadaye. Ili msamaha wowote kwa sababu ya kutofuata masharti yaliyo katika Mkataba huu utambulike lazima uwe umeandikwa na kuwekwa wazi katika maneno yaliyowasilishwa kwa Watchtower au kwako ikitegemea yule anayesamehewa.
4. MATUMIZI YANAYORUHUSIWA NA YASIYORUHUSIWA YA PROGRAMU NA/AU HABARI ZILIZO KATIKA PROGRAMU.
Unapotii vizuizi vilivyoonyeshwa hapa chini, unaweza kufanya yafuatayo:
● Unaweza kutazama, kupakua, na kuchapisha picha, machapisho ya kielektroni, muziki, maandishi, au video zilizo na haki ya kunakili kutoka katika Programu hii kwa ajili ya matumizi yako binafsi na yasiyo ya kibiashara.
Kushiriki na wengine viunganishi (links) au nakala za machapisho ya kielektroni, video, au programu za sauti ulizopakua kutoka katika Programu hii.
Hupaswi kumruhusu mtu mwingine au wewe mwenyewe:
● Kupachika michoro, machapisho ya kielektroni, alama za usajili, muziki, picha, video, au makala kwenye Intaneti kutoka kwenye Programu hii (iwe ni katika tovuti, kituo cha kushiriki faili au video, au mtandao wa kijamii).
Kusambaza michoro, machapisho ya kielektroni, alama za usajili, muziki, picha, maandishi, video, nembo au alama za usajili kutoka kwenye Programu zikiwa sehemu ya au pamoja na programu yoyote ya kompyuta (kutia ndani kupakia habari hizi katika server kwa matumizi ya programu fulani ya kompyuta).
Kutokeza upya, kuiga, kunakili, kusambaza, au kutumia kwa njia isiyofaa picha zozote, nembo, machapisho ya kielektroni, alama za usajili, muziki, picha, maandishi, video, au chochote kutoka katika Programu hii kwa matumizi ya kibiashara au kupata malipo (hata ikiwa hupati faida).
Kutengeneza programu za kompyuta, vifaa, au mbinu zenye kusudi la kukusanya, kunakili, kupakua, kuchota, kuchukua, au kufyonza habari, HTML, picha, au maandishi kutoka katika Programu hii kwa kusudi la kuzisambaza. (Hii haitii ndani programu za bure zisizo za kibiashara zenye kusudi la kupakua faili za kielektroni kama vile, EPUB, PDF, MP3, AAC, MOBI, na faili za MP4 kutoka katika maeneo ya umma ya tovuti.)
Kuchokonoa Programu hii kwa njia yoyote kama vile njia ya kuifungua au kutumia yaliyomo kupitia mbinu nyingine isipokuwa ile ambayo imeruhusiwa.
Kutumia Programu hii kwa njia yoyote inayosababisha, au inayoweza kusababisha madhara, au kuzuia isipatikane au wengine washindwe kuitumia; au kwa njia yoyote ambayo ni kinyume na sheria, isiyo halali, ya ulaghai, au yenye kudhuru, au kuhusiana na kusudi au utendaji wowote ambao ni kinyume cha sheria, usio halali, wa ulaghai, au kwa kusudi au wenye madhara.
Kutumia Programu hii au habari zozote zilizomo kutia ndani michoro, machapisho ya kielektroni, alama za usajili, muziki, picha, maandishi, au video kwa kusudi lolote linalohusiana na kutangaza biashara.
Kutumia Programu hii kwa shughuli zozote za kibiashara au kuitumia kuuza bidhaa zozote au yafuatayo: madawa au kemikali ambazo matumizi yake husimamiwa na serikali; madawa ya kulevya na ya magendo; silaha; video na audio zinazomilikiwa kinyume cha sheria; maelekezo ya kutengeneza au kupata bidhaa zisizo halali au silaha za kuwashambulia wengine; habari zinazoweza kutumiwa ili kupotosha haki miliki, au alama za usajili wa mali au habari za kitaaluma za wengine; habari zitakazotumiwa kuwadhuru wanadamu au wanyama kinyume cha sheria; ponografia, picha za uchi, huduma za kikahaba, au habari zozote zinazoonekana za watu wazima.
Kutumia Programu hii au habari zinazopatikana ndani yake ili kupotosha au kuchochea wengine kupotosha haki za kisheria za watu (kwa mfano, hili linatia ndani kuvunja sheria ya Digital Millennium Copyright Act kwa kuingilia haki za mali za kitaaluma za wengine).
Kutumia Programu hii kusambaza viunganishi vya virus, worms, Trojan horses, faili zilizochokonolewa, viunganishi vya udanganyifu, au kitu chochote kitakachowadhuru wengine.
Kutumia Programu hii kufanya jambo lolote ambalo tumelitathmini kuwa kinyume cha sheria.
Kutumia Programu hii kutangaza, kutuma, kuonyesha lugha chafu, isiyo na heshima, inayowaharibia sifa wengine, inayodhalilisha, matusi, au vitisho.
Kutumia Programu hii au habari zilizomo kwa kusudi lolote kinyume cha sheria, kuingilia, kuvunja sheria, kumchafulia mtu sifa, au wizi (kwa mfano, phishing, biashara za wizi, au kuiga mwonekano wa tovuti nyingine).
Kutumia Programu hii kuunda, kusambaza, kuhifadhi, au kutegemeza utumaji holela wa barua pepe, kufanyia promosheni, matangazo, au maombi mengine (“spam”).
Kufanya jambo lolote ambalo tunaona ni kuvuruga, kuingilia, kukiuka, au linaloathiri (au tisho la kuvuruga, kuingilia, kukiuka au kuathiri) Programu hii, jinsi tunavyoitumia, au jinsi wengine wanavyoweza kuitumia.
Watchtower haiwajibiki kwa njia yoyote ile kwa niaba ya mtu anayetumia Programu hii kinyume cha sheria na kudhalilisha, kutisha, kuharibia wengine sifa, kutuma jumbe za kuumiza wengine, au zinazokiuka sheria. Au unapokabiliana na hali hizo unapotumia Programu hii.
Ukiwa mtumiaji wa Programu hii, ni lazima (i) usikiuke sheria za shirikisho la Marekani, za nchi yoyote uliopo, na za sehemu unayoishi (ii) shikamana na sheria za haki miliki za muziki, video, michezo, picha, maandishi, na media nyingine unazotumia kibinafsi na pia kutokeza habari katika mfumo wa kielektroni.
5. KUVUNJWA KWA MKATABA. Kibali hiki kitaacha kutumika iwapo kitabatilishwa na wewe au Watchtower. Utanyimwa kutumia programu hii ikiwa hutaweza kushikamana na masharti yaliyomo. Watchtower ina uwezo wa kuvunja Mkataba huu na kukunyima kutumia Programu hii kwa sababu yoyote ile au bila sababu na bila kuwajibika kwako. Mkataba huu utakapovunjwa, tafadhali futa Programu hii kwenye vifaa vyako vyote au sehemu nyingine ya kuhifadhi media. Watchtower haitawajibika kisheria kwa kuvunja Mkataba huu au kukunyima ruhusa ya kutumia Programu hii.
6. HABARI ZA KITIBA
Habari au marejeo yaliyomo katika sehemu hii katika Programu (“Habari za Kitiba”) ni kwa kusudi la kuarifu na si kutoa ushauri wa kitiba, na wala si kwa kusudi la kuchukua mahala pa ushauri wa kitaalamu, uchunguzi au tiba. Habari zinazopatikana za kitiba si mapendekezo ya kuiga inapohusu vipimo vyovyote hususa, madaktari, bidhaa, matibabu, maoni, au habari nyingine zozote zinazotajwa.
Habari za kitiba hazijaandaliwa, hazijakusudiwa, au kupitishwa kisheria kutumiwa kufanya uamuzi wa kitiba unaohusu uhai wa mtu, uchaguzi wa kituo cha tiba, au utaratibu wa matibabu, au hata kwa kusudi lingine lolote. Mara zote wasiliana na daktari au mhudumu wa afya anayestahili ikiwa una maswali yoyote kuhusu tatizo la kiafya au tiba fulani. Programu hii haitabeba lawama au kuwajibika kwa makosa yoyote au mapungufu katika habari zinazopatikana kwenye sehemu hiyo.
7. HATI YA KUKATAA KUBADILISHA HABARI ZILIZOMO. HATUWAJIBIKI UNAPOTUMIA PROGRAMU HII NA MAMBO YALIYOMO. PROGRAMU INAPATIKANA “KAMA ILIVYO,” “KAMA INAVYOPATIKANA,” NA KASORO ZOTE. KWA KADIRI SHERIA INAVYOWEZA KURUHUSU, WATCHTOWER INATANGAZA KUKATAA KUBADILISHA HABARI ZOZOTE ZILIZOMO, UWAKILISHI, NA MASHARTI, IWE YAMETAJWA KWA MOJA KWA MOJA, KWA NJIA ISIYO YA MOJA KWA MOJA, AU KISHERIA, KUTIA NDANI HATI YA KUBADILISHA HABARI, MAJUKUMU, AU MASHARTI YA KIBIASHARA, KUTOINGILIA HAKI ZA WENGINE, UBORA KWA MADHUMUNI FULANI, UTEGEMEO AU UPATIKANAJI, USAHIHI AU UKAMILISHAJI, UBORA, USALAMA, UFAAJI, JITIHADA ZA KIUFUNDI, UKOSEFU WA VIRUS, UKOSEFU WA UZEMBE, AU KWAMBA PROGRAMU HII ITAFUATA MBINU FULANI AU KUWA NA MATOKEO YOYOTE HUSUSA, AU ITAKAYOJITOKEZA AU INAYOHUSIANA NA MATUMIZI YAKO AU YA MTU MWINGINE. WATCHTOWER HAIKUHAKIKISHII KWAMBA HUTAKABILI TATIZO LOLOTE UNAPOTUMIA PROGRAMU HII, KWAMBA UTENDAJI WOTE, AU HUDUMA ZILIZOANDALIWA KATIKA PROGRAMU HII ZITAKIDHI MATARAJIO YAKO, KWAMBA UTENDAJI WA PROGRAMU HII UTAENDELEA BILA TATIZO LOLOTE, AU KWAMBA PROGRAMU HII HAITAKUWA IKIKWAMA, KUPOTEZA HABARI ZAKO, IKISHAMBULIWA, KUDUKULIWA, AU KUKABILI MATATIZO MENGINE YOYOTE YA KIUSALAMA. PIA, WATCHTOWER HAINA WAJIBU WA KUANDAA UTEGEMEZO WOWOTE AU HUDUMA NYINGINE ZOZOTE WALA HAINA WAJIBU ISIPOANDAA UTEGEMEZO AU HUDUMA NYINGINE ZOZOTE ZINAZOHUSIANA NA PROGRAMU HII. UPAKUAJI NA UTUMIAJI WA PROGRAMU YOYOTE ILE HUTOKEZA HATARI, HIVYO, WATCHTOWER INAKUTAHADHARI UHAKIKISHE KWAMBA UNAELEWA HATARI HIZO KABLA YA KUPAKUA, KUSAKINISHA, AU KUITUMIA KWA NJIA NYINGINE YOYOTE. WALA WATCHTOWER WALA SHIRIKA LOLOTE LINALOHUSIANA NA WATCHTOWER WALA WAKURUGENZI, MAOFISA, WAJITOLEAJI, WASHIRIKI, WATOA LESENI, WASAMBAZAJI, WAKANDARASI, MAWAKALA, AU WAWAKILISHAJI (KWA UJUMLA, “MASHIRIKA YANAYOSHIRIKIANA NA WATCHTOWER”) WATAWAJIBIKA KWA AJILI YA HASARA YOYOTE UNAYOPATA AU MTU WA TATU ANAYOWEZA KUPATA KUHUSIANA NA UPAKUAJI, USAKINISHAJI, KUONDOA, KUBADILISHA, AU KUTUMIA KWA NJIA YOYOTE NYINGINE PROGRAMU HII AU HABARI ZOZOTE ZILIZOMO.
8. HATI YA KUKATAA KUWAJIBIKA KISHERIA. KWA KADIRI SHERIA INAVYOWEZA KURUHUSU, WATCHTOWER NA MASHIRIKA YANAYOSHIRIKIANA NA WATCHTOWER HAYATATOA FIDIA KWA SABABU YA ATHARI ZA PEKEE, KIFEDHA, MADHARA, AU FIDIA INAYOAMRIWA NA MAHAKAMA, (KUTIA NDANI FAIDA ZILIZOPOTEA, HABARI ZILIZOPOTEA, HESHIMA YA BIASHARA, AU FAIDA ZILIZOTARAJIWA, FIDIA YA HABARI ZA SIRI ZILIZOPOTEA, YA KUSIMAMISHA BIASHARA, YA KUSHINDWA KUTIMIZA WAJIBU WA BIDHAA HIYO AU WA HALI NJEMA AU UTUNZAJI, YA UZEMBE, NA YA KUPOTEZA PESA AU JAMBO LINGINE LOLOTE) INAYOTOKANA NA AU INAYOTEGEMEA MATUMIZI YAKO YA PROGRAMU HII (AU KWA SABABU UNASHINDWA KUTUMIA PROGRAMU HII NA/AU HABARI ZOZOTE KATIKA PROGRAMU HII) AU INAYOHUSIANA NA MKATABA HUU. MAMBO HAYO YANATIA NDANI KUKATAA KUWAJIBIKA KISHERIA KWA KUTEGEMEA MKATABA, UDHAMINI, UTESI (KUTIA NDANI SABABU YA UZEMBE), FIDIA YA UBORA WA BIDHAA, FIDIA YA BIDHAA, MAKOSA, KUBATILISHWA KWA UDHAMINI, KUBATILISHWA KWA MKATABA, AU HATA IKIWA WATCHTOWER AU MASHIRIKA YOYOTE YANAYOSHIRIKIANA NA WATCHTOWER WAMEJULISHWA KUHUSIANA NA ATHARI HIZO. LICHA YA ATHARI ZOZOTE UNAZOWEZA KUPATA KWA SABABU YOYOTE ILE UNAPOTUMIA PROGRAMU HII (HILO LINATIA NDANI ATHARI AMBAZO ZIMETAJWA NA NYINGINEZO), FIDIA NZIMA INAYOWEZA KUTOLEWA NA WATCHTOWER PAMOJA NA MASHIRIKA YANAYOSHIRIKIANA NA WATCHTOWER HAITAZIDI DOLA KUMI ZA MAREKANI ($10). HATI HII YA KUKATAA KUWAJIBIKA KISHERIA ITATUMIKA HATA IKIWA SEHEMU NYINGINE ZA MKATABA HUU ZIMESHINDWA KUTIMIZA KUSUDI.
9. FIDIA. Utawalipa, linda na kutetea Watchtower pamoja na Mashirika yanayoshirikiana na Watchtower dhidi ya vitisho vyovyote, madai, kesi, mashtaka, na madai na hasara zote, madeni, athari, pesa zilizotumiwa, gharama, kutia ndani kiasi fulani cha pesa kwa ajili ya wakili kutokana na matumizi yako ya Programu hii na/au habari zozote zilizomo, kutia ndani haya na mengineo (a) kuvunja Mkataba huu, hilo linatia ndani unapotumia Programu hii katika njia yoyote ambayo hairuhusiwa kama Mkataba huu unavyosema, (b) uzembe au mwenendo wako mbaya, (c) unapovunja sheria yoyote au taratibu yoyote, (d) uwakilishi na udhamini unaofanya kuhusiana na jambo lolote katika Programu hii na/au habari zilizomo, (e) madai yoyote yanayomhusu mtu wa tatu katika nyanja za programu hii na/au habari zilizomo, au (f) madai yoyote yanayotoka kwa mtu wa tatu kuhusiana na jinsi unavyotumia Programu hii na/au habari zilizomo kwa njia ya moja kwa moja au la.
10. RUHUSA KWA HABARI NA FIDIA. Unatuhakikishia kwamba una haki na/au ruhusa ya kuweka Habari yoyote na zote unapoendelea kutumia Programu hii kupatana na maana ya neno Habari (inavyofafanuliwa hapa chini). “Habari” hurejelea taarifa zote unazotoa inapohusiana na matumizi yako ya Programu hii, hilo linatia ndani mambo kama haya na mengineyo, habari, taarifa, jumbe, faili, picha, video, sauti, na chochote kingine. Unatuhakikishia kwamba Habari unazotoa na jinsi utakavyoitumia hakutaingilia au kuvunja amri ya serikali ya kuruhusu utengenezaji haki miliki, alama ya biashara, au siri ya biashara, au haki za mali za kitaaluma za mtu yeyote wa tatu.
Hivyo unatupa ruhusa ya kudumu, isiyo tenguka, ya ulimwenguni pote, isiyo maalum, na isiyo na malipo ya mwandishi na ruhusu ya kutumia, kufanya, kuhifadhi, kubadili, kunakili, kusambaza, kuwasiliana, kutangaza, kuhamisha, kuonyesha hadharani, kufanya hadharani, kuiga, kubadili, kutafsiri, na kubadili mfumo wa Habari za aina hiyo. Unakubali kututetea sisi na Mashirika yanayohusiana na Watchtower kwa gharama zako mwenyewe dhidi ya kesi zote, mashtaka, na malalamiko yanayoelekezwa kwa mashirika yoyote ya Watchtower yakidai tumevunja amri ya serikali ya kuruhusu utengenezaji, alama ya usajili, au siri ya usajli, au haki nyingine yoyote au uvunjaji wa ruhusa au haki za mali za kitaaluma, kwa kutegemea Habari ulizotoa; na unakubali kufidia na kutetea mashirika ya Watchtower dhidi ya lawama, hasara, madeni, athari, gharama, na pesa zilizotumiwa (kutia ndani kiasi fulani cha pesa kwa ajili ya wakili) inayotokana na uhalifu huo. Unaelewa kwamba wewe binafsi ndiye unayewajibika kwa sababu ya Habari zote unazoweka, unazohamisha, au zinazounganishwa kutoka kwenye Programu hii. Unakubali kwamba hatuoni au kuidhinisha Habari unayoweka lakini tuna haki (na si wajibu) wa kuamua kukataa, kufuta, au kuhamisha Habari yoyote ambayo inakiuka Mkataba huu au kwa sababu nyingine yoyote.
11. KUPAKUA NA KUHAMISHA. Huruhusiwi kutumia au kupakua na kuhamisha-hamisha habari zozote katika Programu hii isipokuwa kwa idhini ya sheria ya Marekani na sheria za mamlaka ambamo Programu hii ilipatikana. Hairuhusiwi hasa, kupakua na kuhamisha-hamisha habari zozote katika Programu hii (a) kwenda nchi zozote zilizowekewa vikwazo na Marekani (b) kwa mtu yeyote ambaye jina lake liko kwenye Orodha ya Raia Waliotengwa Kipekee na Idara ya Hazina ya Marekani au Orodha ya Watu Waliokataliwa ya Idara ya Biashara ya Marekani au Orodha ya Chombo. Unakubali pia kwamba hutatumia Programu hii kwa mambo yoyote yanayokatazwa na Sheria.
12. FARAGHA. Masharti yanayodhibiti matumizi ya habari zako za kibinafsi za utambulisho na habari nyinginezo unazotoa kuhusiana na Programu hii yanafafanuliwa katika Sera ya Faragha ya Programu hii.
13. SHERIA YA UONGOZI; UWASILISHAJI WA MADAI KWA WAKATI. Mkataba huu unaongozwa na kufafanuliwa kwa mujibu wa sheria za Jimbo la New York, kutotia ndani kanuni za uchaguzi-wa-sheria za New York, na madai yote yanayotokana na au yanayohusiana na Mkataba huu, au kutokana na uvunjaji wa Mkataba huu, iwe kwa sababu za kimkataba, kosa la kiraia, au nyingine, yataongozwa pia na sheria za Jimbo la New York, kutotia ndani kanuni za uchaguzi-wa-sheria za New York. Sheria ambayo haitumiki kihususa katika Mkataba huu ni ile inayojulikana kuwa Mapatano ya Umoja wa Mataifa ya Uuzaji wa Bidhaa wa Kimataifa. UNAKUBALI KWAMBA HATA IWE KUNA SHERIA YOYOTE INAYOPINGA, IKIWA UNA DAI, SHTAKA AU HATUA DHIDI YA SHIRIKA LOLOTE LA WATCHTOWER KUTOKANA NA AU KUHUSIANA NA MKATABA HUU, LAZIMA HILO LITOKEZWE NDANI YA MIEZI SITA (6) BAADA YA TAREHE AMBAYO TUKIO LILILOSABABISHA DAI HILO KUTENDEKA AU LILIDAIWA KUTENDEKA.
14. HABARI MBALIMBALI. Mkataba huu, Sera ya Faragha ya Programu hii, na Sifa zake na maagizo yoyote yaliyoandikwa kuhusiana na Programu hii yanayoandaliwa na Watchtower yanafanyiza kwa ujumla mkataba kati yako na Watchtower kwa habari ya Programu hii, na yanachukua mahali pa mawasiliano yote ya hapo awali ya mdomo au ya kuandikwa kwa wakati mmoja, mapendekezo na uwakilishaji mbalimbali kuhusiana na Programu hii au habari zozote nyingine zinazorejelewa na Mkataba huu. Watchtower haitalaumiwa katika Mkataba huu kwa ajili ya kutochukua hatua kwa kadiri ambayo kufanya hivyo kunazuiwa, kunakawishwa, au kunazibwa na mambo ambayo Watchtower haiwezi kudhibiti. Ikiwa kuna sehemu yoyote ya Mkataba huu ambayo inaonwa kuwa bila maana, ya ubatili, kutoweza kutekelezwa, au isiyo halali, sehemu hiyo itabadililshwa na mahakama ili kuwasilisha kwa ukaribu zaidi nia ya Watchtower, na sehemu zote nyingine za Mkataba huu yataendelea kutumika kikamili. Watchtower inaweza kukabidhi au kuhamisha Mkataba huu kwa yoyote kati ya mashirika yake. Watchower isipokuhitaji kuchukua hatua wakati wowote kwa habari ya sehemu fulani ya Mkataba huu, hiyo haitaathiri hata kidogo haki yake ya kutekeleza masharti hayo, pia Watchtower ikisamehe uvunjaji wowote wa masharti yoyote ya Mkataba huu jambo hilo halipaswi kuonwa kuwa itasamehe uvunjaji wowote mwingine wa masharti hayohayo.
Kwa Watumiaji: Nakala hii ni makubaliano yanayotambulika kisheria. Tafadhali soma pia makala yenye kichwa “Kwa nini hairuhusiwi kuweka machapisho ya Mashahidi wa Yehova kwenye tovuti ya kibinafsi au kwenye mitandao ya kijamii?”

