Hamia kwenye habari

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

Sera ya Faragha na Vidakuzi

Sera ya Faragha na Vidakuzi

Tengenezo la Mashahidi wa Yehova linaheshimu haki ya faragha ya kila mtu. Ili kupata habari kuhusu Sera ya Kulinda Taarifa Binafsi ya tengenezo letu ulimwenguni pote, tafadhali bofya hapa.

Sera ya Kulinda Taarifa Binafsi inaeleza jinsi tengenezo la Mashahidi wa Yehova linavyoshughulikia taarifa binafsi. Isitoshe, miongozo hususa kwa ajili ya tovuti hii imeandaliwa na inapatikana kwenye mafungu yafuatayo.

Tovuti hii ni mali ya Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc. (“Watchtower”), ni shirika lisilo la kibiashara lililopo jijini New York linalotegemeza utendaji wa Mashahidi wa Yehova na elimu yao ya Biblia. Baadhi ya seva zinazotegemeza tovuti yetu zinapatikana Marekani.

Taarifa za Kibinafsi

Taarifa za kibinafsi zinazoingizwa katika tovuti hii hutumiwa tu kwa kusudi lililotajwa kwa mtumiaji wakati wa kuiwasilisha habari yenyewe.

Hatutoi taarifa zozote za kibinafsi kwa mtu yeyote isipokuwa iwe inahitajika kufanya hivyo ili kuandaa huduma iliyoombwa na mtumiaji na kabla ya kutumia habari hizo tunamjulisha habari kamili mtumiaji au tunaamini vya kutosha kwamba habari hizo zinahitajika ili kutekeleza sheria au matakwa fulani au ili kugundua na kuzuia ulaghai, au kwa sababu za kiusalama, au za kiufundi. Kwa kutumia tovuti hii unakubali tutoe habari zako za kibinafsi kwa makusudi hayo tu. Habari zozote za kibinafsi zinazowasilishwa hazitauzwa, wala kutolewa kwa kubadilishana na nyingine, au kukodishwa katika hali yoyote ile.

Taarifa kwa Mtu wa Tatu. Nyakati nyingine tovuti itatumia viunganishi vinavyoelekeza kwenye tovuti nyingine (third-party vendor) itakayotoa huduma fulani kwa niaba yetu (kwa mfano, inapohusu ujazaji wa fomu mtandoani). Utagundua kwamba umeingia kwenye tovuti nyingine kwa sababu mwonekano wa tovuti hiyo utakuwa tofauti na anwani ya tovuti itabadilika. Wakati tunapomchagua mtu wa tatu wa kutoa huduma, na mara kwa mara baada ya hapo, tunachunguza sera zao za faragha na za kulinda taarifa kibinafsi ili kuhakikisha kwamba zina viwango vinavyofanana na vile tunavyotumia katika sera zetu. Ikiwa una maswali yoyote kuhusu sera ya mtu wa tatu wa kutoa huduma, tafadhali soma sera yao inayopatikana kwenye tovuti yao.

Usalama

Tunahakikisha kwamba taarifa zako za kibinafsi zipo salama. Tunalinda taarifa zako za binafsi kwa kutumia mifumo ya kiteknolojia, kama, teknolojia ya Transport Layer Security (TLS). Tunatumia mifumo ya kompyuta inayotumiwa na watu wachache inayotunzwa kwenye majengo yanayolindwa kielektroniki, kwa kutumia watu na mikakati hususa iliyowekwa ili kulinda usiri na usalama wa taarifa binafsi zinazotufikia.

Anwani ya Barua-pepe

Anwani ya barua-pepe unayotumia unapounda akaunti katika tovuti hii itatumiwa kuwasiliana nawe kuhusiana na akaunti yako. Kwa mfano, ukisahau jina lako la mtumiaji au nywila (nenosiri) yako na kuomba usaidizi kuhusu jinsi ya kuingia kwenye tovuti, utaandaliwa msaada kupitia ujumbe utakaotumwa kwenye anwani ya barua-pepe uliyoingiza habari fupi kukuhusu.

Michango

Ukitoa mchango wa pesa mtandaoni, tutahitaji jina lako na anwani au namba ya simu. Michango inayotolewa kupitia kadi za benki, hushughulikiwa na kampuni za kutoa huduma mtandaoni zinazotegemeka za kuhamisha pesa na zina sera za ulinzi na usalama wa taarifa binafsi zinazotambulika duniani pote. Sisi hatutunzi wala kuona taarifa zilizo kwenye kadi yako ya benki, namba ya akaunti yako ya benki, au taarifa nyingine za akaunti yako utakazotuma kwa kampuni hizo zinazotoa huduma ya kuhamisha pesa. Anayepokea mchango atahifadhi rekodi ya kupokea pesa hizo kwa angalau miaka kumi. Rekodi hiyo inatia ndani rekodi ya tarehe ambayo mchango ulitolewa, kiasi kilichotolewa, na njia iliyotumiwa. Hivyo, tutaweza kwenda sambamba na msharti ya uhasibu na kujibu maswali yoyote kutoka kwako kwa kipindi hicho. Hatutawasiliana na wewe ili kuomba michango zaidi.

Taarifa Nyingine

Unaweza kutoa taarifa zako za kibinafsi (kama jina lako, anwani ya posta, na namba ya simu) ukiwa na kusudi lingine tofauti na kutoa mchango au kufungua akaunti (kama unapotoa ombi la kujifunza Biblia bila malipo). Tunakusanya, kuhifadhi, na kutumia taarifa hizo kwa njia uliyokusudia wakati ulipozitoa na kuzitunza kwa muda wote ambao zitahitajika.

Vidakuzi na Teknolojia Sawa

Habari nyingine zinakusanywa kwa njia ya moja kwa moja unapotembelea tovuti yetu. Tunakusanya taarifa hizo kupitia “vidakuzi,” “web beacons,” au teknolojia zinazofanana na hizo. Matumizi ya neno kidakuzi (cookie) katika sera hii ya faragha ni pana na inatia ndani teknolojia sawa kama ile ya “local storage.”

Vidakuzi. Kama tu ilivyo unapotembelea tovuti nyingine, unapotembelea tovuti yetu pia, kiasi kidogo cha taarifa zinazojulikana kama “vidakuzi” huhifadhiwa katika simu, tablet, au kompyuta yako. Kuna aina mbalimbali za vidakuzi vinavyofanya kazi tofauti-tofauti na kwa ujumla vinaboresha jinsi unavyotumia tovuti. Tunatumia vidakuzi kujua ikiwa uliwahi kutembelea tovuti yetu au kuweka kumbukumbu ya mapendezi yako unayochagua unapotumia tovuti yetu. Kwa mfano, lugha unayochagua kutumia inaweza kuhifadhiwa kwenye kidakuzi ili uitumie utakapotembelea tena tovuti yetu. Vidakuzi hivyo havitatumiwa kibiashara.

Vidakuzi vinavyotumiwa katika tovuti hii vinaweza kugawanya katika makundi matatu:

  1. Vidakuzi Muhimu​—Hivi vinakuwezesha kutumia sehemu fulani za tovuti, kama vile kuingia kwenye akaunti au kuwasilisha fomu kwenye tovuti. Bila vidakuzi hivi, usingeweza kupata huduma muhimu, kama vile kutoa mchango kwa njia ya mtandao. Vidakuzi hivi pia vinakuruhusu kupata huduma hususa unazoomba unapotumia tovuti. Vidakuzi hivi havihifadhi taarifa zako za kibinafsi ambazo zinaweza kutumiwa kwenye mambo ya kibiashara au kujulisha wengine tovuti ulizotembelea.

  2. Vidakuzi vya Utendaji​—Hivi husaidia tovuti kukumbuka mambo unayoingiza (kwa mfano jina, lugha, au mahali ulipo) na vinaboresha utendaji wa sehemu mbalimbali za tovuti.

  3. Vidakuzi vya Uchanganuzi​—Hivi vinakusanya taarifa za jinsi wanaotembelea tovuti wanavyoitumia, kwa mfano ni mara ngapi tovuti imetembelewa au ni kwa muda gani waliitumia. Taarifa hizo hukusanywa tu ili kuboresha utendaji wa tovuti.

Baadhi ya vidakuzi ni vya mtu wa kwanza, navyo vinawekwa na tovuti yetu. Vingine ni vidakuzi vya mtu wa tatu, navyo huwekwa na watu wengine. Sisi tunatumia tu vidakuzi vya mtu wa kwanza isipokuwa tu inapohusu Google reCAPTCHA tunatumia kidakuzi cha mtu wa tatu. Google reCAPTCHA inatumiwa kutujulisha ikiwa tovuti inatumiwa na mtu moja kwa moja au na programu ya kompyuta, ili kudhibiti barua-pepe zenye madhara (spam). Tafadhali ona Sera ya Faragha ya Google kwenyehttps://www.google.com/intl/en/policies/privacy/.

Web Beacons. Kurasa fulani katika tovuti yetu huenda zikawa na faili ndogo za kielektroni zinazojulikana kama web beacons zinazotuwezesha kurekodi utendaji katika tovuti, kama vile kufunguliwa kwa ukurasa fulani. Web beacons zinatumiwa kurekodi matumizi ya tovuti hii na kukagua ubora wake.

Matumizi ya anwani ya IP. Anwani ya IP ni mfululizo wa namba kadhaa zinazotambulisha kompyuta yako unapokuwa mtandaoni. Tunaitumia anwani yako ya IP na kivinjari chako kutusaidia kuchunguza utendaji wa tovuti, kugundua matatizo yanayotokea na kuboresha huduma tunayokupatia.

Uchaguzi Wako. Karibu aina zote za vivinjari hukuruhusu kuzuia utendaji wa vidakuzi au kukutaarifu kabla ya kukihifadhi katika kifaa chako. Tafadhali rejelea miongozo ya kivinjari chako kujifunza jinsi ya kufanya hivyo. Hata hivyo, tafadhali zingatia kwamba bila kuwa na vidakuzi hutaweza kutumia vizuri baadhi ya sehemu zinazopatikana katika tovuti yetu.

HatiJava (Active Scripting au JavaScript)

Hati hutumiwa na tovuti kuboresha utendaji wa tovuti. Kutumia ufundi wa hati huwezesha tovuti kurejesha habari zilizoombwa haraka zaidi kwa mtumiaji. Hati haitumiwi kamwe na tovuti kusakinisha programu kwenye kompyuta ya mtumiaji wala kukusanya habari kutoka kwa mtumiaji pasipo idhini..

Lazima HatiJava iwezeshwe katika kipekuzi ili sehemu fulani za tovuti zifanye kazi ifaavyo. Vivinjari vingi humruhusu mtumiaji kuwezesha au kulemaza hati hizo katika tovuti hususa. Soma habari kuhusu kipekuzi ili upate kujua jinsi ya kuwezesha hati katika tovuti teule.

Haki Yako

Matumizi yako ya tovuti hii, kutia ndani kupakua machapisho, video, au rekodi zozote za sauti ni bila malipo. Huhitaji kufungua akaunti, kutoa mchango, au kutoa taarifa zozote za binafsi ili unufaike na habari zilizopo katika tovuti hii. Hata hivyo, ikiwa kwa hiari yako mwenyewe utachagua kufungua akaunti, kutoa mchango, au kujaza ombi la kujifunza Biblia bila malipo, au kutoa taarifa za kibinafsi kwa kusudi lingine lolote, basi unakubaliana na Sera hii ya Faragha na Vidakuzi; na kuhifadhiwa kwa taarifa zako katika seva nchini Marekani; na ukusanywaji, utumiaji, uhamishaji, na kuhifadhiwa kwa taarifa zako binafsi na Watchtower na mashirika yanayotoa utegemezo kwa Mashahidi wa Yehova katika nchi mbalimbali inapohitajika, ili kutekeleza ombi lako. Taarifa itakusanywa kwa njia inayotegemea kusudi lake la kutolewa. Kwa mfano, ukitoa mchango kupitia shirika la kisheria katika nchi fulani, basi jina, anwani au simu yako itatatumwa kwa shiriki hilo kama utakavyokuwa umejulishwa wakati unapotoa mchango huo. Mfano mwingine ni unapotoa ombi la kujifunza Biblia, katika kisa hiki jina, anwani au simu yako itatatumwa ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova itakayotekeleza ombi lako.

Ikiwa hutaweza kutoa taarifa binafsi zinazohitajika ili kufungua akaunti, kutoa mchango, au kunufaika kwa njia nyingine yoyote inayohitaji taarifa za binafsi, hatutaweza kutekeleza ombi lako.

Ikihitajika kubadili Sera ya Faragha na Vidakuzi, tutatangaza mabadiliko hayo katika gombo hili ili sikuzote ujue taarifa tunazokusanya na jinsi tunavyozitumia.

Kwa mujibu wa sheria, huenda ukawa na haki nyingine za matumizi ya taarifa zako za kibinafsi. Haki hizo zinaweza kutia ndani haki ya kupata, kusahihisha au kuondoa taarifa zako binafsi ulizowasilisha katika tovuti. Ikiwa sheria ya nchi yako inatia ndani haki hizo, unaweza kuwasiliana nasi hapa. Ikiwa ombi lako la habari zaidi kuhusu matumizi ya taarifa zako binafsi linahusu utoaji mchango, tafadhali wasiliana na yule atakayepokea mchango huo. Taarifa za atakayepokea mchango utazipata katika hatua mojawapo unapotoa mchango huo na katika stakabadhi ya mchango.