Kiswahili
Kimbunga Rai Chaipiga Filipino
https://cms-imgp.jw-cdn.org/img/p/702021421/univ/art/702021421_univ_sqr_xl.jpg

DESEMBA 22, 2021
FILIPINO

Kimbunga Rai Chaipiga Filipino

Kimbunga Rai Chaipiga Filipino

Desemba 16 hadi 18, 2021, Kimbunga Rai (kinachojulikana nchini Filipino kama Odette) kilipiga maeneo mbalimbali ya Filipino. Kilipopiga kwa mara ya kwanza katika Kisiwa cha Siargao, Filipino, kilikuwa na upepo wenye kuendelea uliovuma kwa kilomita 195 kwa saa. Mikoa ya Mindano Kaskazini, Luzon Kusini, na Visayas vilikabili uharibifu mkubwa.

Athari kwa Ndugu na Dada Zetu

  • Kwa kusikitisha, wahubiri 4 walikufa

  • Mhubiri mmoja bado hajulikani alipo

  • Ndugu na dada 12 walijeruhiwa

  • Zaidi ya wahubiri 2,000 wamelazimika kuhama makazi yao

  • Nyumba 246 ziliharibiwa kabisa

  • Nyumba 327 zilipata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 1,174 zilipata uharibifu mdogo

  • Majumba 43 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Halmashauri 6 za Kutoa Msaada zimeanzishwa ili kusimamia kazi ya kutoa msaada

  • Wazee wa eneo hilo wanawafanyia ziara za uchungaji wale walioathiriwa, kutia ndani wale waliowapoteza wapendwa wao

  • Jitihada zote za kutoa msaada zinafanywa kulingana na miongozo ya usalama ya kujilinda dhidi ya COVID-19

Chini ya mwongozo wa wazee, ndugu na dada katika maeneo ambayo hayakuathiriwa walitoa chakula na mavazi kwa ajili ya wahubiri walioathiriwa na kimbunga hicho. Vifurushi vya chakula kutoka Jiji la Davao vilisambazwa mara moja kwa familia zilizokuwa na uhitaji katika Jiji la Surigao.

Tunasikitika kusikia kwamba baadhi ya ndugu na dada zetu wapendwa walikufa katika janga hilo. Tunapoendelea kuvumilia “nyakati [hizi] za hatari zilizo ngumu kushughulika nazo,” na tuendelee kumtegemea Yehova ili atupe faraja na kutuimarisha.​—2 Timotheo 3:1.