Kiswahili
Habari Njema Kulingana na Yesu
https://cms-imgp.jw-cdn.org/img/p/1011760/univ/art/1011760_univ_sqr_xl.jpg

Habari Njema Kulingana na Yesu​—Mhutasari wa Mfululizo Wote

MFULULIZO WA VIDEO


Kionjo

Nembo ya lugha.

Inapatikana Katika Lugha Zaidi ya 500

Video hizi zinawasaidia watu ulimwenguni pote kujifunza mafundisho ya Yesu katika lugha yao wenyewe

Nembo ya Biblia.

Hati Ni Biblia

Mazungumzo yametolewa moja kwa moja kwenye Injili ya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana

Nembo ya Utafiti.

Utafiti Wenye Kina

Miaka mingi ya utafiti imetumika kuhakikisha habari zote ni sahihi kadiri iwezekanavyo


Drama

Drama zinapatikana pia zikiwa na maelezo ya video ili kuwasaidia vipofu na watu wenye uwezo mdogo wa kuona.

DRAMA YA 1

Yosefu na Maria walipewa pendeleo la kumlea Yesu, mtoto aliyekuwa tofauti na wengine wote.

DRAMA YA 2

Yohana Mbatizaji anatangaza kutokea kwa Masihi. Yesu anaanza huduma yake.

DRAMA YA 3

Yesu anamfundisha Nikodemo, mwanamke Msamaria, na watu wa Nazareti. Baadhi wanamkubali, wengine wanamkataa.

DRAMA YA 4

Yesu anawaponya wagonjwa, anawafukuza roho waovu, anafanya wanafunzi, na kuchagua mitume wake 12.

DRAMA YA 5

Baada ya kuponya umati mkubwa, Yesu anatoa Mahubiri ya Mlimani—hotuba yake maarufu zaidi.

DRAMA YA 6

Yesu anamfufua mwana wa mjane, anafundisha kwa kutumia mifano rahisi, na kufichua nia za wale wanaomsikiliza.

Drama Nyingine Zitapatikana Hivi Karibuni

Drama mpya zitatolewa kila mwaka mpaka mfululizo huu wenye drama 18 unapokamilika. Drama zifuatazo zitatolewa Mei 2027.


Mafundisho ya Yesu Yanawezaje Kuboresha Maisha Yako?

Mashahidi wa Yehova watafurahi kukusaidia ujifunze mengi zaidi kumhusu Yesu na jinsi mashauri yake yanavyoweza kukusaidia kuwa na maisha yenye furaha zaidi sasa. Angalia sehemu mbalimbali za jw.org ili ujifunze mengi zaidi, au uombe kujifunza Biblia bila malipo ukiongozwa na mwalimu.

Huenda Ukapenda Pia

MAJIBU YA MASWALI YA BIBLIA

Ukweli Kumhusu Yesu

Pata majibu ya maswali yako kumhusu Yesu moja kwa moja katika Neno la Mungu.

MAJIBU YA MASWALI YA BIBLIA

Kwa Nini Yesu Anaitwa Mwana wa Mungu?

Ikiwa Mungu hakumzaa Yesu kihalisi kama wanadamu wanavyozaa watoto, inawezekanaje kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?

MAJIBU YA MASWALI YA BIBLIA

Je, Unabii wa Kimasihi Unathibitisha Kwamba Yesu Alikuwa Ndiye Masihi?

Je, mtu zaidi ya mmoja angeweza kutimiza unabii wa Kimasihi?

MAFUNDISHO MUHIMU YA BIBLIA

Kwa Nini Yesu Alikufa?

Huenda unajua kwamba alikufa kwa sababu ya dhambi zetu? Lakini dhabihu ya mtu mmoja inawezaje kuwanufaisha mamilioni ya watu?