Ona video zinazopatikana

Ona habari zilizo ndani

WIMBO 75

Miye Huyu! Unitume!

Miye Huyu! Unitume!

(Isaya 6:8)

  1. 1. Watu wako nachafua

    Kabisa jina ya Mungu.

    Na wengine wanasema

    Ya kama “hakuna Mungu.”

    Nani atamutetea

    Na kumuimbia sifa?

    (REFREE 1)

    Miye huyu, unitume!

    Nitakuimbia sifa.

    Kwangu ni pendeleo sana

    Kufanya kazi yako.

  2. 2. Leo watu wanasema

    Yehova anakawia,

    Tena hawamuogope;

    Wanaabudu sanamu.

    Ni nani atawaonya

    Kuhusu vita ya Mungu?

    (REFREE 2)

    Miye huyu, unitume!

    Nitawaonya wabaya.

    Kwangu ni pendeleo sana

    Kufanya kazi yako.

  3. 3. Wapole wako nalia

    Kwa sababu ya mabaya.

    Wako natafuta kweli

    Yenye kuleta amani.

    Nani atawafariji?

    Nani atawafundisha?

    (REFREE 3)

    Miye huyu, unitume!

    Nitafundisha wapole.

    Kwangu ni pendeleo sana

    Kufanya kazi yako.

(Ona pia Zb. 10:4; Eze. 9:4.)