Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Sera ya Kulinda Taarifa Binafsi

Sera ya Kulinda Taarifa Binafsi

Tengenezo la Mashahidi wa Yehova linaheshimu haki ya faragha ya kila mtu kulingana na kanuni zinazopatikana katika Biblia. Linatambua umuhimu wa kuwa na mawasiliano yaliyo wazi na ya unyoofu pamoja na umuhimu wa kukusanya taarifa za binafsi na zilizo nyeti ili kushughulikia mahitaji ya Mashahidi wa Yehova na kutimiza utendaji wake wa kidini na huduma inayotoa bila malipo, na pia umuhimu wa kutunza siri na kuhakikisha kwamba taarifa binafsi zinalindwa ipasavyo. (Methali 15:22; 25:9) Utunzaji wa siri ni jambo muhimu sana kwetu.​—Methali 20:19.

Nchi mbalimbali zimepitisha Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi ili kuhakikisha kwamba haki ya faragha ya kila mtu inalindwa. Tengenezo la Mashahidi wa Yehova lina historia ndefu ya kuheshimu haki za faragha na kutunza siri, hata kabla ya kupitishwa kwa sheria hizo za kulinda taarifa binafsi. Tengenezo la Mashahidi wa Yehova litaendelea kulinda taarifa binafsi kama tu lilivyokuwa likifanya kwa miaka mingi ila kwa sasa sera hiyo ya ulinzi wa taarifa binafsi inapatikana katika hati hii.

Upana wa Matumizi

Sera hii inatumiwa na tengenezo zima la Mashahidi wa Yehova. Tengenezo hili linawakilishwa na ofisi za tawi zilizopo ulimwenguni pote.

Ulinzi wa Taarifa

Tengenezo la Mashahidi wa Yehova linashughulikia taarifa za binafsi kwa kufuata kanuni zifuatazo:

 1. Taarifa binafsi zinatumiwa kwa haki na kisheria.

 2. Taarifa binafsi zitakusanywa, na kutumiwa zinapohitajika tu kwa madhumuni ya kutimiza utendaji wa dini wa Mashahidi wa Yehova na kushughulikia michango.

 3. Taarifa binafsi zitakuwa sahihi na ambazo hazijapitwa na wakati. Kosa lolote litasahihishwa mara tu linapogunduliwa na tengenezo.

 4. Taarifa binafsi zitatunzwa na tengenezo kwa kadiri zinavyohitajika ili zitumiwe kwa kusudi linalofaa.

 5. Haki za wenye taarifa (data subjects) zitaangaliwa kwa uzito.

 6. Hatua za kiufundi na mipango itafanywa ili kuzuia usambazaji wa taarifa binafsi bila idhini au kinyume cha sheria. Taarifa zote binafsi zinahifadhiwa kwenye kompyuta zenye nywila na zinazotumiwa tu na watu wenye idhini ya kufanya hivyo. Ofisi zenye kompyuta hizo hufungwa baada ya saa za kazi na walioidhinishwa tu ndio wenye ruhusa ya kuingia kwenye ofisi hizo.

 7. Taarifa binafsi hazitatolewa kutoka ofisi moja ya tawi kwenda nyingine ila tu ikiwa ni lazima kufanya hivyo kwa ajili ya kutimiza utendaji wa dini au inapohusu michango ya hiari ya tengenezo la Mashahidi wa Yehova, mambo ambayo kimsingi Mashahidi wa Yehova wameyakubali kwa kukubali kwa hiari kuwa na kujitambulisha kuwa Mashahidi wa Yehova.

Haki za Mwenye Taarifa

 1. Haki ya mwenye taarifa inayolinda taarifa zake za kibinafsi na zilizo nyeti na ya kusahihishwa au kufutwa kwa taarifa hizo itatolewa kulingana na utendaji wa Mashahidi wa Yehova unaopatikana kwenye sera hii.

 2. Mtu yeyote atakayetoa ombi linalohusu sehemu hii ni lazima atoe uthibitisho wa kutosha unaomtambulisha.

 3. Ikiwa mwenye taarifa atatoa ombi la kusahihishwa, au kufutwa kwa taarifa zake binafsi au zilizo nyeti, tengenezo litashughulikia ombi lake kwa njia ya haki likizingatia pande zote mbili, yaani, faida za mwenye taarifa za kupewa au kusahihisha au kufuta taarifa na faida za kimsingi za tengenezo, kutia ndani ikiwa kukubali ombi hilo kutahatarisha haki ya uhuru wa dini na utendaji wa tengenezo.

 4. Tengenezo lingependa kuweka taarifa za kudumu za mtu zinazoonyesha kwamba yeye ni Shahidi wa Yehova. Kufuta taarifa ya aina hiyo kutaingilia utendaji wa tengenezo na imani ya dini.

Haki ya Kukata Rufaa

Ikiwa mtu anaamini kwamba haki zake zimeingiliwa, anaweza kukata rufaa kwa kuiandikia Halmashauri ya Tawi kupitia barua ya kibinafsi. Barua inapaswa itumwe ndani ya majuma mawili ya kutokea kwa tukio ambalo ni msingi wa rufaa hiyo.