JULAI 4, 2018
MAMBO MAPYA
Sehemu ya Maandishi Haitapatikana Katika Baadhi ya Video za JW Broadcasting Zinazorushwa Kupitia Roku
Sehemu ya Cheza Pamoja na Maandishi haitapatikana kwa muda katika baadhi ya video za JW Broadcasting zinazorushwa kupitia Roku, na itachukua miezi michache ili maandishi katika video yaweze kupatikana. Sehemu ya maandishi ya video za JW Broadcasting zinazorushwa kupitia Amazon Fire TV na Apple TV haitaathiriwa na badiliko hili.
Ikiwa watumiaji wa Roku wanataka kutazama video za JW Broadcasting pamoja na maandishi wanaweza kutumia tovuti ya JW Broadcasting kama njia mbadala ya kupata video zenye maandishi. Ili kuonyesha maandishi katika tovuti, bofya kisanduku cha Onyesha maandishi ikiwa yanapatikana kwenye sehemu ya Mipangilio katika skrini.

