JULAI 8, 2019
MAMBO MAPYA
Tafsiri ya Ulimwengu Mpya Imetolewa Katika Kichina Cha Mandarini
Toleo lililorekebishwa la Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ya maandiko matakatifu lilitolewa katika lugha ya Kichina cha Mandarini (ya kitamaduni) na Kichina cha Mandarini (kilichorahisishwa) tarehe 5 Julai, 2019, katika jiji la Taoyuan City, Taiwan. Tafsiri ya Ulimwengu Mpya imetafsiriwa ikiwa nzima au kwa sehemu katika lugha 180, kutia ndani lugha 24 zilizorekebishwa kulingana na toleo la 2013.

