Hamia kwenye habari

OKTOBA 7, 2019
MAMBO MAPYA

JW.ORG Kwenye Amazon Alexa na Google Assistant

JW.ORG Kwenye Amazon Alexa na Google Assistant

Kama ilivyotangazwa kwenye mkutano wa kila mwaka wa Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania mnamo Oktoba 5, 2019, sasa unaweza kucheza habari zilizochaguliwa kwenye jw.org ukitumia programu za Amazon Alexa au Google Assistant. Sauti zinazoweza kutambuliwa zinatia ndani lugha ya Kifaransa, Kihispania, Kiingereza, Kiitaliano, na Kijerumani.

Ili kupata habari zaidi kuhusu jinsi ya kutumia mfumo wa sauti kucheza habari zilizo kwenye jw.org, soma makala zifuatazo “Tumia JW.ORG Skill Kwenye Amazon Alexa au “Tumia JW.ORG Action Kwenye Google Assistant.”