Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

TOVUTI YA JW.ORG

Tazama Video Kwenye JW.ORG

Tazama Video Kwenye JW.ORG

Tazama video moja au zote zilizo katika mkusanyo. Tua, rudisha nyuma, au peleka mbele.

 Tafuta na Cheza Video

Fungua sehemu ya MAKTABA > VIDEO ili kuona video zote zilizopo, kutia ndani zilizoandaliwa katika studio yetu ya JW Broadcasting.

Chagua sehemu ya video.

Kila kipengele kinawakilisha mkusanyiko wa video. Ili kuona video nyingi zaidi katika mkusanyiko, nenda kushoto au kulia katika mkusanyiko au bofya Ona Zote.

Tazama au shiriki video kwa kutumia njia moja kati ya njia zilizoorodheshwa hapa:

 • Bofya Cheza kwenye kifaa.

 • Bofya Pakua ili kuhifadhi video kwenye kompyuta au kifaa chako kingine. (Taarifa: Baadhi ya vifaa vya mkononi vitahitaji kutumia programu nyingine ili kupakua faili hizo. Ikiwa una programu ya JW Library kwenye simu yako, tunapendekeza uitumie kupakua video ambazo utatazama bila kuunganisha intaneti.)

 • Bofya Shiriki ili kumtumia mtu kiunganishi cha video hiyo. Ili kujua mengi zaidi, ona “Shiriki kiunganishi cha Makala, Video au Chapisho.”

 • Ili kutazama video katika lugha tofauti, chagua lugha unayotaka kutoka kwenye orodha yenye kichwa Lugha iliyo pembeni mwa kichwa cha video.

 Cheza Video Zote Zilizo Katika Kipengele Kimoja au Katika Mkusanyiko

Bofya kitufe Changanya katika ukurasa wenye mkusanyiko huo ili kucheza video zote katika kipengele bila kufuata mpangilio.

Kuna njia mbili za kutazama video zote katika mkusanyiko wa kipengele kimoja:

 • Bofya kitufe Cheza Zote kilicho katika mkusanyiko wa video ili kucheza video zote kama zilivyoorodheshwa.

 • Bofya kitufe Changanya kilicho katika mkusanyiko ili kucheza video zote bila mpangilio.

Taarifa: Kila video katika mkusanyiko itachezwa mara moja na mwishowe itasimama.

 Cheza, Tua, Peleka Mbele, na Rudisha Nyuma

Unaweza kufanya hivyo kwa:

 • Kubofya kitufe cha Jaza Skrini ili kukuza video na ionekane kwenye skrini nzima au inaweza kurudisha video kuwa ndogo ikiwa ilikuwa imejaza skrini.

 • Bofya Tua ili video isimame.

 • Bofya Cheza ili video iendelee kucheza.

 • Kokota Kishale mbele au nyumba ili kupeleka video mbele au kuirudisha nyuma.

 • Bofya kitufe cha Sauti na kukokota kishale ili kuongeza au kupunguza sauti. Ikiwa unatumia simu, unaweza kutumia kitufe cha sauti cha simu yako.

 Badilisha mipangilio ya video

Bofya Mipangilio na uchague kiwango ubora wa mwonekano wa video. (Taarifa: Si virambaza vyote vina mpango huu.)

Namba hizi humaanisha nini? Kadiri namba inavyozidi kuongezeka, na ubora wa video pia huongezeka, nayo itahitaji intaneti yenye kasi zaidi. Chagua kiwango ambacho kulingana na kasi ya intaneti yako, ukubwa wa skrini na kiasi cha pesa ulichopangia kutumia ili kulipia huduma ya intaneti.

Orodha inayofafanua viwango hivyo:

Kiwango

Maelezo

240p

Ubora wa chini sana. Ni nzuri kwa ajili ya simu ndogo za mkononi.

360p

Ubora wa chini. Ni nzuri kwa ajili ya simu ndogo za mkononi.

480p

Ubora wa hali ya kati. Ni nzuri kwa ajili ya tablet, skrini ya kompyuta na ya televisheni zenye ubora wa hali ya kati.

720p

Ubora wa hali ya juu (HD). Ni nzuri kwa ajili ya skrini ya kompyuta yenye ukubwa wa angalau 1024 x 768 au kwenye HDTV yenye ukubwa wa angalau 1280 x 720.

Kwa nini ni muhimu kubadilisha kiwango cha video? Ikiwa intaneti yako haina kasi na unagundua kwamba video inatua yenyewe, ni afadhali kutumia kiwango cha chini zaidi. Tumia kiwango cha juu zaidi ambacho kinafaa kompyuta au kifaa chako. Unaweza kutumia kiwango cha chini pia ikiwa unataka kupunguza gharama za kununua intaneti.

Bofya kitufe cha Maandishi ya Video ili yatokee au ili kuyatoa, yatafuatana na lugha unayotumia kutazama video.

Taarifa: Si video zote zenye maandishi ya video.