Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

TOVUTI YA JW.ORG

Tafuta Habari Katika Lugha ya Ishara

Tafuta Habari Katika Lugha ya Ishara

Habari nyingi za lugha ya ishara zinapatikana katika mfumo wa video. Baadhi ya lugha za ishara zina sehemu fulani ya Tovuti ya jw.org iliyotafsiriwa, kutia ndani ukurasa wa mwanzo. Lugha nyingine za ishara bado hazijatafsiri Tovuti hiyo, lakini vitabu, magazeti na machapisho mengine yanapatikana katika mfumo wa video, na yanapatikana kwenye sehemu ya MACHAPISHO.

Tumia mojawapo ya njia zifuatazo ili upate machapisho katika lugha ya ishara:

 Chagua Lugha Yako ya Ishara

  • Njia ya 1: Bonyeza sehemu ya Chagua Lugha ili utazame orodha kamili ya lugha zinazopatikana kwenye Tovuti ya jw.org.

  • Bonyeza kisanduku cha Onyesha Lugha ya Ishara Pekee ili utazame lugha za ishara tu.

    Au unaweza kuandika jina la lugha ya ishara unayotaka katika kisanduku. Utatazama orodha iliyo na majina yanayofanana na herufi ulizoandika.

  • Njia ya 2: Bonyeza kiunganishi cha “Tazama Video za Lugha ya Ishara” kwenye ukurasa wa mwanzo. Chagua lugha ya ishara katika orodha hiyo.

Ikiwa Tovuti imetafsiriwa katika lugha ya ishara uliyochagua, hiyo itakakuwa lugha ya Tovuti uliyochagua.

Tovuti ya lugha ya ishara hutambuliwa upesi kwa sababu kila sehemu kwenye menyu inaambatana na ishara yake upande wa kushoto. Kila ishara inawakilisha sehemu fulani ya Tovuti.

Katika sehemu ya MACHAPISHO, baadhi ya sehemu kwenye menyu zinatumia maneno yanayotofautiana na yale yanayotumiwa katika lugha zisizo za ishara. Kwa mfano, kwenye Tovuti za lugha ya ishara, sehemu ya MUZIKI inaitwa NYIMBO.

Tumia menyu hizo kufungua habari unazotafuta. Cheza au upakue video za lugha ya ishara.

Nenda Kwenye Sehemu ya MACHAPISHO

 Nenda kwenye MACHAPISHO > MACHAPISHO YALIYOTEULIWA.

Chagua lugha ya ishara unayoipenda kutoka kwenye orodha ya lugha. Kwa kuwa kuna lugha nyingi katika orodha hiyo, unaweza kubonyeza sehemu ya orodha ya lugha, kisha uanze kuandika jina la lugha. Orodha hiyo itaonyesha majina yanayofanana na herufi ulizoandika tu.

Ikiwa lugha ya ishara uliyochagua ina machapisho machache tu, yote yatatokea kwenye ukurasa wa MASHAPISHO YALIYOTEULIWA. Hata hivyo, huwezi kuona machapisho yote kwenye ukurasa wa MASHAPISHO YALIYOTEULIWA katika lugha za ishara zenye machapisho mengi yaliyotafsiriwa. Nenda kwenye ukurasa wa aina ya machapisho (kwa mfano, BIBLIA, MAGAZETI, VITABU NA BROSHUA) ili utazame machapisho ya aina hiyo yanayopatikana katika lugha ya ishara.

Tumia Programu ya JW Library Sign Language

Programu ya JW Library Sign Language inaweza kukufaa ikiwa:

  •   unatumia mara kwa mara video za lugha ya ishara.

  • unaweza kunufaika kwa kuwa na video hizo kwenye kifaa chako cha mkononi wakati hujaunganishwa kwenye Intaneti.

  • programu hiyo inapatikana katika lugha ya ishara unayotumia.

Kwa habari zaidi, nenda kwenye JW Library Sign Language ukurasa wa msaada.