Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

TOVUTI YA JW.ORG

Tafuta Habari Katika Lugha Nyingine

Tafuta Habari Katika Lugha Nyingine

Ikiwa unajifunza lugha, au ungependa kutumia Tovuti ya jw.org kumwonyesha habari fulani mtu anayeongea lugha nyingine, tumia mojawapo ya njia tatu zinazoelezwa hapa chini ili kutafuta lugha unayopenda.

 Badili Lugha Katika Tovuti

Bonyeza sehemu ya Chagua Lugha ili uone orodha kamili ya lugha zinazopatikana kwenye Tovuti ya jw.org.

Kila lugha katika orodha hiyo ina mojawapo ya ishara zifuatazo upande wa kushoto wa jina la lugha:

 • Tovuti yenyewe, au sehemu fulani ya Tovuti, imetafsiriwa katika lugha hiyo. Bonyeza jina la lugha ili uifanye iwe lugha ya Tovuti.

 • Tovuti haijatafsiriwa katika lugha hiyo, lakini kuna machapisho unayoweza kupakua katika lugha hiyo. Bonyeza jina la lugha hiyo ili utazame machapisho yanayopatikana katika lugha hiyo.

 • Hii ni lugha ya ishara.

  Ikiwa sehemu fulani ya Tovuti ya jw.org imetafsiriwa katika lugha ya ishara unayochagua, hiyo ndiyo itakayokuwa lugha ya Tovuti.

  Ikiwa Tovuti ya jw.org haijatafsiriwa katika lugha ya ishara unayochagua, utaona orodha ya machapisho yanayopatikana katika lugha hiyo ya ishara.

Kwa kuwa kuna mamia ya lugha katika orodha hiyo, tumia mojawapo ya njia zifuatazo ili upate kwa urahisi lugha unayopenda:

 • Chagua lugha unayoipenda: Lugha nne ulizochagua karibuni kwenye Tovuti zitatokea juu kwenye orodha ya lugha.

 • Andika jina la lugha: Andika herufi chache za jina la lugha, iwe ni katika lugha yako au lugha unayotafuta. Kwa mfano, ikiwa unatumia Tovuti katika lugha ya Kiingereza na unataka kubadilisha iwe katika Kijerumani, unaweza kuandika “German” au “Deutsch.” Kadiri unavyoandika herufi, orodha ya lugha itaonyesha tu majina ya lugha yanayofanana na herufi ulizoandika.

 Tazama Ukurasa wa Tovuti Katika Lugha Nyingine

Njia ya 1: Tumia njia hii kwenye kurasa zilizo na sehemu ya Soma Katika.

Fungua makala unayotaka kusoma au kumwonyesha mtu mwingine. Kisha chagua lugha katika sehemu ya Soma Katika ili uisome katika lugha hiyo. (Ikiwa lugha unayotafuta haipatikani katika orodha ya Soma Katika, hilo linamaanisha kwamba makala hiyo haijatafsiriwa katika lugha unayotafuta.)

Dokezo: Katika orodha ya Soma Katika, ishara ya rekodi za sauti upande wa kushoto wa jina la lugha huonyesha kwamba makala hiyo inapatikana pia katika mfumo wa sauti katika lugha hiyo.

Ukifungua makala katika lugha nyingine kwa kutumia orodha ya Soma Katika, ni makala hiyo tu itakayofunguka katika lugha uliyochagua. Sehemu nyingine ya Tovuti itabaki katika lugha uliyofungua mwanzoni.

Njia ya 2: Ikiwa makala unayosoma haina orodha ya Soma Katika, tumia sehemu ya Chagua Lugha ili ubadilishe Tovuti iwe katika lugha unayopenda. Ikiwa makala unayosoma inapatikana katika lugha uliyochagua, itafunguka. La sivyo, utaelekezwa kwenye ukurasa wa mwanzo wa Tovuti katika lugha uliyochagua.

 Tafuta Chapisho Katika Lugha Nyingine

Nenda kwenye MACHAPISHO > BIDHAA ZILIZOTEULIWA. Chagua lugha katika orodha ya lugha na ubonyeze Tafuta.

Tumia mojawapo ya njia zifuatazo kutafuta lugha nyingine kwa njia rahisi zaidi:

 • Chagua lugha unayoipenda zaidi: Lugha nne ulizochagua karibuni zaidi zitatokea juu kwenye orodha hiyo.

 • Andika jina la lugha: Andika herufi chache za jina la lugha, iwe ni katika lugha yako au lugha unayotafuta. Kwa mfano, ikiwa unatumia Tovuti katika lugha ya Kiingereza na unataka kubadilisha iwe katika Kijerumani, unaweza kuandika “German” au “Deutsch.” Kadiri unavyoandika herufi, orodha ya lugha itaonyesha tu majina ya lugha yanayofanana na herufi ulizoandika.

Ikiwa kuna machapisho mengi katika lugha uliyochagua, ukurasa wa BIDHAA ZILIZOTEULIWA utaonyesha bidhaa chache tu. Ili utafute machapisho zaidi katika lugha uliyochagua, nenda kwenye mojawapo ya kurasa za aina ya chapisho (kwa mfano, VITABU NA BROSHUA au MAGAZETI) ili upate orodha ya machapisho ya aina hiyo yanayopatikana katika lugha uliyochagua.

Ikiwa machapisho hayo hayapatikani katika lugha uliyochagua, ukurasa utaonyesha viunganishi vya machapisho yanayopatikana.