Mamia ya nakala za kielektroni, sauti na video zinapatikana katika sehemu ya MACHAPISHO katika jw.org. Tumia maelekezo haya kupata chapisho unalotafuta.

 Tafuta Chapisho kwa Kutumia Jina la Chapisho

Ikiwa unafahamu jina au sehemu ya maneno ya jina la chapisho fulani, fuata maelekezo haya kupata chapisho hilo haraka.

Fungua sehemu ya MACHAPISHO > VITABU NA BROSHUA.

  • Bofya katika kisanduku cha Bidhaa Zote kisha andika neno fulani lililo katika jina la chapisho unalotafuta. Kwa mfano, ikiwa unatafuta kitabu Biblia Inafundisha, andika neno “fundisha.” Utafiti wako utakuwa umekusudiwa kuleta machapisho yaliyo na jina lenye neno “fundisha”. Chagua jina la kitabu unachotafuta.

  • Bofya kitufe cha Tafuta.

 Tafuta Toleo la Gazeti

Fungua sehemu ya MACHAPISHO > MAGAZETI.

Ukurasa huu unapofunguka, huonyesha nakala nne za karibuni za Amkeni! na Mnara wa Mlinzi (Toleo la watu wote) na nakala nane za karibuni za Mnara wa Mlinzi toleo la funzo. (Baadhi ya lugha hazina matoleo yote.) Kupata nakala ya gazeti, fuata maelekezo haya:

  • Chagua toleo hususa la gazeti unalotafuta katika mpangilio wa magazeti.

  •   Bofya kitufe cha Tafuta.

Tazama Mbinu Zinazopatikana za Kupakua Machapisho

Machapisho yamepangwa katika njia mbili—Mpangilio Mraba na kwa njia ya Orodha.

Bofya kitufe cha Mpangilio Mraba kufungua mpangilio wa kawaida wa machapisho.

Mpangilio Mraba huonyesha jalada la chapisho, alama ya kupakua, na jina la kila chapisho. Bofya alama ya kupakua (au gusa alama hiyo katika vifaa vya mkononi) kupata mbinu mbalimbali za kupakua chapisho hilo.

Bofya kitufe cha Orodha kubadili mpangilio.

Mpangilio wa Orodha unapofunguka huonyesha mbinu zote za kupakua chapisho.

Baadhi ya machapisho yana matoleo ya ziada kama vile chapa kubwa. Ili kupakua chapisho, bofya toleo hususa kupata mbinu za upakuaji wa toleo hilo (kwa mfano PDF) kisha bofya kiunganishi cha toleo unalotaka kupakua.

 Tafuta Chapisho kwa Kutumia Habari Katika Chapisho

Ikiwa chapisho linapatikana katika mtandao, tumia njia ya Tafuta Kwenye Tovuti kutafuta nakala au sura iliyo na maneno au sentensi hiyo.

Bofya kitufe cha Tafuta. Andika neno au maneno unayotafuta katika kisanduku cha maneno, kisha bofya kitufe cha Tafuta. Ikiwa unafahamu baadhi ya maneno makuu ya chapisho unalotafuta, yaandike yote. Jambo hilo litasaidia kutokeza sura au makala unayotafuta mwanzoni mwa matokeo.

Weka mipaka ya matokeo ya chapisho unalotafuta kwa kufuata maelekezo haya:

  • Bofya Tafuta Zaidi au kiunganishi cha Mbinu Zaidi.

  • Bofya Kipengele na kwenye kichwa chagua Machapisho.

  • Bofya kitufe cha Tafuta.