Kurasa zote na sehemu zote zinazoweza kufunguka kwenye skrini ya kompyuta kubwa zinaweza kufunguka pia kwenye simu ya kisasa au tablet. Hata hivyo, menyu na kurasa zimepangwa kwa njia tofauti kwa ajili ya vifaa vidogo vya kubeba mkononi ili iwe rahisi zaidi kusoma. Madokezo yaliyo katika makala hii yatakusaidia kutafuta machapisho unayohitaji kwenye Tovuti ya jw.org.

 Tumia Menyu za Vifaa vya Mkononi

Kwenye skrini sehemu za msingi sikuzote zinaonekana upande wa juu wa skrini na menyu ya pili huonyeshwa upande wa kushoto wa skrini.

Hata hivyo, kwenye viwambo vidogo vya simu, menyu zote huonekana upande mmoja. Pia, menyu hazionekani ikiwa hazitumiwi ili kuruhusu mtazamaji aone vizuri habari kwenye kiwambo.

 • Bonyeza Menyu ili kuficha au kuonyesha menyu iliyopo. Bonyeza sehemu unayotaka katika menyu ili kufungua ukurasa unaotaka.

 • Bonyeza Ongeza Orodha ili kuona menyu ya pili ndani ya sehemu hiyo. Bonyeza jina la menyu ili kufungua ukurasa unaotaka.

 • Bonyeza Ficha Orodha ili kuficha menyu ya pili ya sehemu hiyo.

 • Bonyeza JW.ORG ili kurudi mwanzo.

 • Bonyeza Lugha ili uone orodha ya lugha zinazopatikana.

 • Bonyeza Tafuta ili kupata habari kwa kutumia Tafuta kwenye Tovuti.

 Rambaza Makala au Sura za Chapisho

Katika mfumo wa kujaza skrini, sikuzote jedwali ya yaliyomo huonekana unaposoma chapisho au sura ya chapisho. Hata hivyo, kwa kawaida kwenye kiwambo kidogo cha simu jedwali haionekani.

 • Bonyeza Onyesha Orodha ili kuona jedwali ya yaliyomo. Bonyeza kichwa ili kuona yaliyomo kwenye makala au sura ya chapisho.

 • Bonyeza Iliyotangulia ili kuona makala au sura iliyotangulia.

 • Bonyeza Inayofuata ili uone makala au sura itakayofuata.

 • Bonyeza Ficha Orodha ili usione jedwali ya yaliyomo na kuendelea kusoma makala au sura uliofungua.

 Rambaza Biblia Mtandaoni

Nenda kwenye MACHAPISHO > BIBLIA na ubonyeze Soma Mtandaoni. Au, bonyeza kiunganishi cha Soma Biblia Mtandaoni kwenye ukurasa wa kwanza.

Kwenye Kistari cha Kurambaza Biblia, chagua kitabu cha Biblia na sura kutoka kwenye orodha ya vitabu na ubonyeze Go.

Unapoteremka chini kwenye orodha ya sura ya vitab, Kistari cha Kurambaza Biblia kinabaki kwenye Kistari cha Menyu ili iwe rahisi kwako kurambaza sura nyingine.

 • Bonyeza Ondoa ili kuondoa Kistari cha Biblia kutoka kwenye Kistari cha Menyu. Hilo huwezesha kuwa na nafasi ya kutosha kwenye kiwambo chako ili kuona andiko la Biblia. ili kuchagua sura tofauti, unahitaji kuteremka chini au juu kwenye ukurasa unaosoma.

 • Bonyeza Hifadhi ili kuhifadhi Kistari cha Kurambaza kwenye Kistari cha Menyu.

 • Bonyeza Onyesha Orodha ili kuona jedwali ya yaliyomo katika Biblia, kutia ndani na habari za utangulizi na nyongeza.

 • Bonyeza Iliyotangulia ili kuona sura iliyotangulia.

 • Bonyeza Inayofuata ili kuona sura itakayofuata.

 • Bonyeza Ficha Orodha ili kuficha jedwali ya yaliyomo.

 Sikiliza Rekodi ya Makala

Ikiwa rekodi ya sauti inapatikana ya makala unayosoma, Kistari cha Rekodi kitaonekana.

 • BonyezaCheza ili kucheza rekodi ya sauti.

 • Bonyeza Sitisha ili kusitisha rekodi ya sauti. Bonyeza Cheza ili kuendelea kucheza rekodi ya sauti.

 • Kokota kishale mbele au nyuma ili kusikiliza sehemu tofauti kwenye rekodi ya sauti.

Ukianza kusikiliza rekodi ya sauti kisha ushuke chini kwenye makala, Kistari cha Rekodi kinabaki kikiwa kimehifadhiwa kwenye Kistari cha Menyu. Hilo linakuwezesha kusitisha na kuanza tena kucheza rekodi ya sauti bila kupoteza mahali ulipofika kusoma kwenye makala.