Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW LIBRARY SIGN LANGUAGE

Tumia Orodha

Tumia Orodha

Pangilia video katika orodha kwa ajili ya mikutano, funzo la kibinafsi, au utumishi.

 Kuongeza video kwenye orodha

 1. Fungua video, kisha bonyeza, Kuongeza Kwenye Orodha.

 2. Chagua kisehemu ambacho ungependa kuongeza, yaani, kisehemu hususa cha video kama vile mstari moja katika Biblia.

 3. Bonyeza Maliza.

 4. Chagua orodha ya video iliyopo, au bonyeza Tengeneza Orodha kisha uweke jina kwa ajili ya orodha mpya.

ZINGATIA: Ili kuongeza video nzima kwenye orodha, bonyeza Ongeza kwenye video kisha ubonyeze Kuongeza Kwenye Orodha.

  Punguza urefu wa video

Tumia kitufe cha Kupunguza Urefu wa Video ili kuchagua kisehemu cha video katika orodha. Unapocheza video zilizo katika orodha, ni visehemu tu ulivyopunguza urefu vitakavyocheza.

 1. Fungua video kwenye orodha.

 2. Bonyeza kitufe cha Kupunguza Urefu wa Video.

 3. Vuta vishikizo vya upande wa kushoto na upande wa kulia ili kupunguza urefu wa video.

 4. Bonyeza kitufe cha Cheza ili kuona video iliyopunguzwa urefu itakavyokuwa.

 5. Bonyeza kitufe cha Maliza ili kuhifadhi marekebisho uliyofanya kwenye video.

ZINGATIA: Video zilizopunguzwa urefu zitaonyeshwa kwa mstari wa rangi ya chungwa chini ya picha ya video hiyo.

 Pangilia orodha yako unavyotaka

Kubadili Jina

Ili kubadili jina katika orodha, bonyeza kitufe cha Kubadili Jina.

Ili kubadili jina la video kwenye orodha, bonyeza kitufe cha Ongeza kisha ubonyeze kitufe cha Kubadili Jina ili ubadili jina la video. Kumbuka kwamba video inabadilishwa tu katika orodha uliyochagua.

Kubadili Mpangilio

Sogeza video kwenye orodha kwa kuigusa na kushikilia video hiyo unapoivuta kuipeleka mahali papya.

Kupangua Makundi

Unapounganisha visehemu kadhaa vinavyokaribiana katika video (kwa mfano mistari inayofuatana katika sura ya Biblia), vitaunganishwa kama kundi moja kwenye orodha. Ili kutengeneza kikundi tofauti kwenye orodha kwa ajili ya kila kisehemu, bonyeza kitufe cha Ongeza na uchague Kupangua Makundi.

Umalizio

Unaweza kuchagua hatua inayofuata kwa kila video katika orodha inapomaliza kucheza. Unapocheza video iliyo katika orodha, hatua uliyochagua itaamua ni jambo gani kati ya haya ambalo litafanyika video inapomaliza kucheza:

 • Endelea: Cheza video inayofuata.

 • Acha Kucheza: Rudi kwenye orodha.

 • Simamisha: Simamisha kwenye sehemu ya mwisho ya video.

 • Rudia: Cheza video hiyo tena.