Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW LIBRARY SIGN LANGUAGE

Sakinisha JW Library Sign Language Ikiwa Huwezi Kuipakua Kwenye (App Store) Ukitumia Kifaa cha Windows

Sakinisha JW Library Sign Language Ikiwa Huwezi Kuipakua Kwenye (App Store) Ukitumia Kifaa cha Windows

Ikiwa huwezi kusakinisha JW Library Sign Language kwenye kifaa cha Windows kutoka kwenye Microsoft Store, unaweza kuisakinisha kwa kutumia faili za kusakinisha za JW Library Sign Language Windows.

Huenda ukahitaji kubadili mipangilio ya kifaa chako ili iruhusu kifaa chako kusakinisha programu kutoka kwa vyanzo vingine. Nenda kwenye Mipangilio (Settings) kisha fungua sehemu yenye mipangilio kutoka kwa watengenezaji (developers). Kisha, bonyeza chaguo linaloruhusu kusakinisha programu kutoka kwenye chanzo chochote au vyanzo vingine. Zingatia: Ikitegemea toleo la windows unalotumia, huenda chaguo hilo likawa na maneno kama vile“Developer Mode” au “Sideload apps.”

Pakua na usakinishe faili za kusakinisha za JW Library Sign Language:

  1. Bofya kitufe cha Pakua katika ukurasa huu ili kuhifadhi faili za kusakinisha kwenye diski ya kompyuta.

  2. Bofya kitufe cha kulia kwenye kipanya chako ili ufungue faili ya zip.

  3. Fungua folda, tumia kitufe cha kulia cha kipanya chako kubofya kwenye faili ya Install.ps1, kisha bofya Run with PowerShell.

  4. Thibitisha kwamba cheti cha kusaini kimesakinishwa ikiwa kinahitajika.

  5. Baada ya kumaliza kusakinisha ujumbe wa uthibitisho utatokea.

Mara kwa mara angalia ikiwa kuna toleo jipya la programu ya JW Library Sign Language.

  1. Fungua ukurasa wa Mipangilio kwenye JW Library Sign Language ili kuona kifaa chako kina toleo gani la programu hiyo.

  2. Ikiwa namba ya toleo inayoonyeshwa kwenye Mipangilio ni tofauti na namba iliyo hapa chini, pakua na kusakinisha programu ya JW Library Sign Language kwa kufuata hatua zilizotajwa hapo juu.

Version: 5.0.84 (224139)