Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW LIBRARY SIGN LANGUAGE

Sakinisha JW Library Sign Language Ikiwa Huwezi Kuipakua kwenye (App Store) Ukitumia Kifaa cha Android

Sakinisha JW Library Sign Language Ikiwa Huwezi Kuipakua kwenye (App Store) Ukitumia Kifaa cha Android

Ikiwa huwezi kusakinisha JW Library Sign Language kwenye kifaa chako cha Android kutoka kwenye app store, kama vile Google Play Store au Amazon Appstore, unaweza kuisakinisha kwa kutumia JW Library Sign Language Android package (APK).

Ili kusakinisha JW Library Sign Language APK, utahitaji kukiruhusu kifaa chako kiweze “kusakinisha programu zisizojulikana” au “kuruhusu programu kutoka vyanzo visivyojulikana ziwekwe.” Ili kujua jinsi ya kufanya hivyo, soma kitabu cha mwongozo cha kifaa chako cha Android.

Fuata hatua hizi ili kupakua na kusakinisha JW Library Sign Language APK:

  1. Bofya kitufe cha Pakua kilicho kwenye ukurasa huu, kisha uhifadhi programu ya APK uliyopakua kwenye kifaa chako.

  2. Tafuta programu hiyo ya APK katika kifaa chako, kisha ibofye ili usakinishe JW Library Sign Language.

Baada ya kusakinisha JW Library Sign Language APK, angalia mara kwa mara ikiwa kuna toleo jipya la programu hiyo. Ili kufanya hivyo, fuata hatua zifuatazo:

  1. Fungua ukurasa wa Mipangilio kwenye JW Library Sign Language ili kujua toleo unalotumia.

  2. Ikiwa namba ya toleo unalotumia ni tofauti na namba iliyo hapo chini kwenye kifaa chako, Pakua na sakinisha faili ya APK kwa kufuata hatua zilizotajwa hapo juu.

Version: 5.0 (224138)