JW LIBRARY SIGN LANGUAGE
Njia Rahisi za Kucheza Video
Ishara za Skrini ya Kugusa
Unapotumia kifaa kinachotumika kwa kugusa skrini, tumia ishara ili kucheza video.
Cheza au simamisha video kwa kugusa kwa vidole viwili.
Unaweza kupata video inayofuata kwa kutelezesha kidole kuelekea kushoto. Ili kupata video iliyotangulia, telezesha kuelekea kulia.
Ongeza kasi ya video kwa kutelezesha kuelekea juu. Punguza kasi ya video kwa kutelezesha kuelekea chini.
Vifupisho vya Kibodi
Katika kifaa kinachotumia programu ya Windows kilicho na kibodi, bofya vitufe vifuatavyo unapoonyesha video:
Iliyotangulia |
Mshale wa Kushoto |
Rudi nyuma sekunde 5 |
Ctrl + Mshale wa Kushoto |
Cheza/Simamisha |
Kitufe cha nafasi |
Songa mbele sekunde 15 |
Ctrl + Mshale wa Kulia |
Inayofuata |
Mshale wa Kulia |
Funga video |
Esc |
Kurudia video iliyotangulia |
Page Up |
Kucheza video inayofuata |
Page Down |
Kuongeza kasi ya video |
Ctrl + Mshale wa juu |
Kupunguza kasi ya video |
Ctrl + Mshale wa chini |