Hamia kwenye habari

JW LIBRARY LUGHA YA ISHARA

Mambo Mbalimbali Kuhusu JW Library Lugha ya Ishara

Mambo Mbalimbali Kuhusu JW Library Lugha ya Ishara

JW Library Lugha ya Ishara ni programu rasmi ya Mashahidi wa Yehova. Inaweza kupakua, kupanga, na kucheza video za lugha ya ishara zilizo kwenye Tovuti ya jw.org/sw.

Tazama video ya Biblia ya lugha ya ishara pamoja na machapisho mengine ya lugha ya ishara. Pakua machapisho hayo kwa kutumia kifaa chako cha mkononi ili uweze kuyatazama wakati wowote. Furahia picha maridadi, kurasa zilizo rahisi kufungua, na rahisi kutumia.

 

Rahisi Kutumia

Unaweza kutazama kitabu kimoja-kimoja cha Biblia ya Tafsiri ya Ulimwengu Mpya kwenye ukurasa wenye Biblia. Pia, unaweza kutazama Maandiko ambayo hayajatafsiriwa kwenye Tafsiri ya Ulimwengu Mpya lakini ambayo ni sehemu ya machapisho mengine ya lugha ya ishara. Ukurasa wenye Maktaba unaonyesha pia machapisho mengine na sinema zinazopatikana kwenye Tovuti ya jw.org.

 

Tafuta kwa Urahisi Maandiko Yaliyorejelewa

Unapotazama video, bonyeza sehemu ya Biblia. Video itasitishwa na andiko lililorejelewa litaonekana. Rudi kwenye ukurasa wa Maktaba ili uendelee kutazama video hiyo.

Pakua Video kwa Njia Rahisi

Video ambazo hujapakua zitaonekana zikiwa na rangi hafifu. Bonyeza video ili uipakue kutoka jw.org. Bonyeza kitufe cha Pakua Zote ili upakue video zote katika ukurasa huo. Bonyeza video kwa muda mrefu (usiachie haraka) ili ufute video kutoka kwenye kifaa chako.

 

Chagua Njia ya Kuhifadhi Video

Chagua aidha kupakua video zinazochukua nafasi kubwa (zenye-ubora-wa-juu) au zinazochukua nafasi ndogo (zenye-ubora-wa-chini). Ikiwa kifaa chako kina sehemu ya kuingiza kadi ya SD, unaweza kuchagua aidha kuhifadhi video zako katika kifaa chako au katika kadi ya SD.

 

Programu ya Kuchezea Video Iliyo Rahisi Kutumia

Tumia njia hizi rahisi ili kuongoza video:

  • Bonyeza kwa kidole mara mbili: Cheza au simamisha video.

  • Papasa kwenda kushoto: Nenda kwenye alama ya kuongozea video inayofuata.

  • Papasa kwenda kulia: Rudi kwenye alama ya kuongozea video uliyoipita.

  • Papasa kwenda juu: Ongeza mwendo wa kucheza video. (Haifanyi kazi katika vifaa vya Android.)

  • Papasa kwenda chini: Punguza mwendo wa video. (Haifanyi kazi katika vifaa vya Android.)

  • Bonyeza mara moja: Ficha au onyesha alama za kuelekezea video.

Msaada

Ikiwa una swali lolote kuhusiana na programu ya JW Library Lugha ya Ishara, unaweza kuomba msaada kwa rafiki yako anayejua jinsi ya kuitumia. Ikiwa hawezi, tafadhali wasiliana na ofisi ya tawi iliyo karibu.