Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

JW LIBRARY

Pakua na Utumie Machapisho​—Windows

Pakua na Utumie Machapisho​—Windows

Kwenye JW Library, unaweza kusoma vitabu, broshua, na trakti, na kutazama video nyingi hata bila kuunganishwa kwenye Intaneti.

Fuata maelekezo yafuatayo ili kupakua na kutumia machapisho:

  • Pakua Chapisho

  • Futa Chapisho

  • Sasisha Chapisho

Pakua Chapisho

Unaweza kupakua machapisho mengi kadiri unavyotaka ili usome na kujifunza unapozima Intaneti.

  • Kwenye sehemu ya juu ya skrini yako, bofya Machapisho na kisha bonyeza Aina ili kupata orodha ya machapisho.

  • Fungua Amri za Programu, kisha bonyeza kitufe cha Lugha ili kupata orodha ya lugha mbalimbali ambazo unaweza kupata machapisho katika lugha hizo. Chagua lugha unayotaka kuona. Lugha unayotumia mara nyingi itakuwa upande wa juu wa orodha hiyo. Pia unaweza kutafuta lugha unayotaka kwa kuandika jina la lugha unayotafuta.

Kuna njia kadhaa za kutafuta machapisho unapotumia JW Library.

Sehemu inayoitwa Aina inaonyesha machapisho katika lugha uliyochagua yakiwa yameorodheshwa kwa aina, kama vile Vitabu, Trakti, au Video. Ukibofya aina fulani ya machapisho utapata uchaguzi wa ziada, kwa mfano ukibofya Mnara wa Mlinzi utapata mpangilio kwa kutegemea mwaka au sehemu ya video itakupa aina mbalimbali za video. Ukibofya sehemu iliyoandikwa Aina Zote itakurudisha kwenye orodha ya machapisho yote.

Sehemu ya Nini Kipya inaonyesha machapisho ambayo yametolewa hivi karibuni katika lugha uliyochagua.

Machapisho ambayo bado hayajapakuliwa yana alama ya wingu. Bofya chapisho ikiwa unataka kulipakua. Chapisho hilo linapomaliza kupakuliwa, alama ya wingu hupotea. Bofya chapisho hilo ili uweze kulisoma.

Sehemu inayoitwa Zilizopakuliwa inaonyesha machapisho yote ambayo umepakua katika lugha yoyote. Unaweza kuyapanga machapisho kwa njia tatu. Kwanza, Unazotumia kwa Ukawaida, pili, Ambazo Hutumii kwa Ukawaida, au tatu, Kubwa Zaidi.

Futa Chapisho

Unaweza kufuta chapisho ikiwa hulihitaji tena au ikiwa unahitaji nafasi zaidi kwenye kifaa chako.

Kwenye sehemu ya juu ya skrini, bofya Machapisho, kisha bonyeza Aina ili kuona orodha ya machapisho. Gusa na ubonyeze kwenye chapisho hilo ili kulichagua. Bofya Futa kwenye Amri za Programu, kisha thibitisha kwamba unataka kufuta chapisho hilo.

Ikiwa unahitaji kupata nafasi zaidi kwenye kifaa chako, unaweza kufuta machapisho usiyotumia kwa ukawaida au machapisho makubwa sana. Bofya Machapisho, kisha bonyeza Zilizopakuliwa, halafu panga orodha hiyo kulingana na Ambazo Hutumii kwa Ukawaida au Kubwa Zaidi. Futa machapisho ambayo huhitaji.

Sasisha Chapisho

Mara kwa mara, machapisho ambayo tayari umepakua hurekebishwa au matoleo mapya kuingizwa.

Chapisho ambalo limerekebishwa huwa na alama ya vishale. Unapobofya chapisho hilo, utaona ujumbe unaosema kwamba chapisho hilo limerekebishwa. Bofya Pakua ili kulisasisha, au ubofye Baadaye ili kuendelea kusoma chapisho ulilopakua tayari.

Ili uone ikiwa chapisho lolote ulilopakua limerekebishwa, bofya Machapisho. Ikiwa kuna machapisho yaliyorekebishwa, sehemu yenye kichwa Sasisha itakuwepo. Ukiibofya utaona orodha ya machapisho yote yanayohitaji kusasishwa. Bofya chapisho moja ili kulisasisha, au ubofye kitufe cha Sasisha Zote ili upakue machapisho yote yaliyorekebishwa.

Sehemu hizo mbalimbali zilipatikana Machi 2015 kwenye JW Library toleo la 1.4, ambalo linafanya kazi vizuri kwenye vifaa vinavyotumia mfumo wa Windows 8.1 au wa karibuni zaidi. Ikiwa huoni mambo haya, tafadhali fuata mwelekezo kwenye makala “Anza Kutumia JW Library ​—Windows,” kwenye Pata Habari za Karibuni Zaidi.