Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW LIBRARY

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi​—JW Library (iOS)

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi​—JW Library (iOS)

JW Library inaweza kutumiwa katika vifaa vifuatavyo vya Apple:

  • iPad 2 au mpya zaidi (zenye mfumo wa iOS 9.0 au wa karibuni zaidi)

  • iPhone 4 au mpya zaidi (zenye mfumo wa iOS 9.0 au wa karibuni zaidi)

  • iPod touch kizazi cha 5 (zenye mfumo wa iOS 9.0 au wa karibuni zaidi)

 

Lugha mpya huongezwa pindi kwa pindi. Ili uone orodha ya lugha ambazo chapisho unalotaka linapatikana, bonyeza kitufe cha Lugha.

Rangi hizo zinalingana na mpangilio wa vikundi vinane vinavyofafanuliwa kwenye Swali la 19 katika kijitabu Utangulizi wa Neno la Mungu.

 

JW Library inafanya kazi kwa njia ileile katika vifaa vyote. Lakini, sehemu fulani na matoleo mapya ya programu hutolewa wakati tofauti-tofauti kwa ajili ya matumizi katika kila kifaa.

 

Hapana. Ikiwa utaondoa programu ya JW Library na kuisakinisha tena upya, kumbukumbu ya alama za ukurasa na mistari uliyopiga itapotea. Lakini, ikiwa umefuta au kuondoa chapisho fulani na kisha ukalipakua tena, alama za ukurasa na sehemu ulizokuwa umepigia mistari zitapatikana tena.

 

Hapana. Kwa wakati huu, alama za kukumbuka ukurasa na sehemu ulizopigia mistari zitapatikana tu katika kifaa ulichofanya hivyo.

 

Tatizo: Baada ya kusasisha programu ya JW Library ili kupata toleo la hivi karibuni, huenda ukapata ujumbe unaosema kwamba mambo makuu uliyoandika na alama ulizoweka zimepotea. Huwezi kuona mambo makuu uliyoandika, vibandiko, alama, machapisho unayotumia kila mara na alama za kukumbuka kurasa.

Suluhisho: Toleo la hivi karibuni la programu hiyo inaweza kutatua tatizo hilo. Sakinisha toleo lenye nambari kubwa zaidi, na ufuate maelekezo yaliyo kwenye skrini ili kurudisha mambo yako makuu na alama.

 

Rafiki anayefahamu programu ya JW Library anaweza kukusaidia. Ikiwa hawezi, tafadhali wasiliana na ofisi ya tawi iliyo karibu.