Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

JW BROADCASTING

Tazama Video ya Karibuni Kwenye TV.JW.ORG

Tazama Video ya Karibuni Kwenye TV.JW.ORG

Video za Karibuni inakupa nafasi ya kutazama video za tv.jw.org wakati wowote. Tua, rudisha nyuma, peleka mbele. Tazama video moja au video zote katika mkusanyiko. Bonyeza Video za Karibuni ili kuona mkusanyiko wa video unaopatikana. Fuata hatua zifuatazo ili kupata na kutazama video:

 Tazama Video ya Karibuni

Unapochagua Video za Karibuni, ishara inatokea upande wa juu wa skrini inayoonyesha video hiyo. Ishara hiyo inabadilika kila baada ya sekunde chache ili kuonyesha video tofauti. Baadhi ya video hizo ni mpya. Nyingine zinaweza kuonyeshwa ikiwa zinahusiana na mikutano yetu ya kila juma.

Bonyeza ishara ili kuchagua video iliyoonyeshwa hapo. Skrini itafunguka yenye habari kuhusu video hiyo, kichwa, ni kuhusu nini, na ni ndefu kadiri gani.

Bonyeza Cheza ili uanze kucheza video hiyo. (Taarifa: Unahitaji kubonyeza Cheza kwenye iOS na simu za Android ili video hiyo icheze.)

 Tafutiza Video

Mkusanyiko unaonyeshwa chini ya ishara ya kuonyesha Video za Karibuni. Kila mkusanyiko unaonyeshwa na ishara na kichwa cha mkusanyiko. Baadhi ya video zinapatikana ndani ya mikusanyiko kadhaa. Kwa mfano, video Mwana Mpotevu Arudi inaweza kupatikana chini ya vichwa Sinema, Familia, na Matineja.

Shuka chini ili uone mikusanyiko yote.

Bonyeza ishara ya mkusanyiko mmoja au kichwa ili kuchagua mkusanyiko unaotaka. Ishara iliyo upande wa juu ya skrini inaonyesha kichwa cha mkusanyiko uliopo na aina zilizopo. Chini ya ishara hiyo utapata mkusanyiko wa video ndani ya mkusanyiko huo.

Kompyuta au tablet: Bonyeza Kishale Kushoto au Kishale Kulia ili uone video zaidi ndani ya mkusanyiko.

Simu za kisasa: Huonyesha video ya kwanza katika mkusanyiko. Ili kuona video zaidi, bonyeza Ona Zaidi.

Bonyeza ishara ya video au kichwa cha video ili kuchagua. Ishara iliyo upande wa juu wa skrini inaonyesha kichwa cha video, ni ya aina gani, na ni ndefu kadiri gani.

Bonyeza Cheza ili kucheza video hiyo. (Taarifa: Unahitaji kubonyeza Cheza kwenye iOS na simu za Android ili kucheza video hiyo.)

 • Dokezo: Badala ya kucheza video moja, unaweza kubonyeza Cheza Zote chini ya mkusanyiko wa video ili kucheza video zote katika mkusanyiko huo.

  Taarifa: Video itaacha kucheza itakapokamilisha kucheza mkusanyiko wote.

 • Katika Cheza Zote, bonyeza Hatua Nyuma kwenda kwenye video iliyotangulia.

 • Katika Cheza Zote, bonyeza Hatua Mbele ili ucheze video iliyo mbele katika mkusanyiko huo.

 Tua, Sogeza mbele, rudisha nyuma Video

Katika sehemu ya Video za Karibuni, unaweza kudhibiti video kwa kufanya mambo yafuatayo:

 • Kompyuta: Ili kutazama video kwenye skrini nzima, elekeza kishale juu ya skrini na ubonyeze Jaza Skrini.

  Tablet or au simu ya kisasa: Ili kutazama video kwenye skrini nzima, fungua video kisha bonyeza Jaza Skrini.

 • Kompyuta: Ili kutazama video katika mfumo wa kawaida, bonyeza Ondoka, au uelekeze kishale juu ya video na ubonyeze Kawaida.

  iOS: Ili kutazama video katika mfumo wa kawaida, fungua video kisha ubonyeze Kawaida.

  Simu za Android: Ili kutazama video katika mfumo wa kawaida, fungua video kisha ubonyeze Nyuma kwenye kifaa chako cha mkononi.

  Simu aina ya Windows: Ili kutazama video katika mfumo wa kawaida, bonyeza Nyuma kwenye kifaa chako cha mkononi.

 • Bonyeza Tua ili video itue.

 • Bonyeza Cheza ili kuendelea kucheza.

 • Ili kusogeza hatua mbele kwenye video, onyesha kishale mbele au nyuma.

 • Kompyuta: Ili kubadili jinsi video unayotazama inavyoonekana, elekeza kishale juu ya skrini, kisha juu ya Mipangilio ya Video, kisha uchague mwonekano upendao. (Taarifa: Mpangilio huu hautegemezwi na vipekuzi vyote.)

  Taarifa: Mipangilio imepangwa kulingana na namba. Namba ya juu zaidi inamaanisha ubora wa video, ambayo itahitaji Intaneti kwa wingi zaidi. Chagua inayofanya kazi vizuri kulingana na kipimo chako cha intaneti na ubora wa skrini yako. (Kwa habari zaidi, onaBadili Mpangilio wa Kompyuta Yako au Kifaa Chako.)

  Simu za kisasa au Tablet: Ili kubadili mwonekano wa video, fungua video, kisha ubonyeze Mipangilio ya Video, kisha uchague upendavyo kutoka kwenye orodha hiyo. (Taarifa: Mipangilio hii haipatikani kwenye vifaa vyote vya mkononi.)

 • Kompyuta: Ili kubadili sauti, elekeza kishale juu ya video, kisha juu ya Sauti. Kokota kishale juu au chini ili kuongeza au kupunguza sauti.

  Tablet au simu za kisasa: Ili kubadili sauti, bofya vitufe vya kupunguza na kuongeza sauti kwenye kifaa chako.