Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

JW BROADCASTING

Badili Mipangilio Kwenye Kompyuta, Tablet, au Simu ya Kisasa

Badili Mipangilio Kwenye Kompyuta, Tablet, au Simu ya Kisasa

Kwenye skrini ya Mipangilio unaweza kupangilia kituo cha tv.jw.org kulingana na mapendezi yako.

Bonyeza Mipangilio. Fuata hatua zifuatazo:

Taarifa: Mipangilio hii inakubalika kwenye vipekuzi au vifaa vya mkononi vinavyotegemezwa. Ukifuta habari zote kwenye kipekuzi chako, mipangilio yako huenda ikarudi katika mfumo wa awali uliokuwapo mwanzoni kabisa.

 Chagua Ubora wa Picha Unaopendelea

  • Bonyeza na uchague sehemu yenye ubora wa picha unaopendelea.

  • Bonyeza Tunza ili uhifadhi mipangilio yako.

Namba hizi zinamaanisha ninii? Namba zilizopo kwenye orodha hii zinawakilisha urefu wa fremu ya video, na zinakusaidia kujua ubora wa picha. Namba kubwa inawakilisha ubora mkubwa zaidi wa picha, unaohitaji intaneti ya kasi zaidi.

Jedwali lifuatalo linaelezea kila ubora wa picha:

Ubora wa Picha

Ufafanuzi

240p

Ubora wa chini kabisa. Tumia kwenye vifaa vya mkononi vyenye skrini ndogo.

360p

Ubora wa chini. Tumia kwenye vifaa vya mkononi vyenye skrini ndogo.

480p

Yenye ubora wa kadiri. Tumia kwenye tablet, kompyuta, na skrini za televisheni zenye ubora kama huo.

720p

Ubora wa hali ya juu (HD). Inafanya kazi vizuri kwenye kompyuta yenye skrini yenye ubora wa angalau 1024x768, au HDTV yenye ubora wa 1280x720.

1080p

Ubora wa hali ya juu kabisa (HD). Inafanya kazi vizuri kwenye kompyuta yenye skrini yenye ubora wa angalau 1080 pixels, au HDTV yenye ubora wa 1920x1080.

Kwa nini ubadili ubora wa picha? Ikiwa intaneti yako inafanya kazi taratibu, na video inatua mara kwa mara, huenda ukahitaji kutumia ubora wa picha wa chini zaidi. Tumia kiwango cha ubora wa picha unaofanya kazi vizuri kwenye kompyuta au kifaa chako. Pia unaweza kutumia ubora wa picha wa chini zaidi ili kupunguza gharama za pesa kwenye matumizi ya intaneti .

Mpangilio huu unatumiwaje? Kituo cha TV.JW.ORG hakitumii ubora wa picha wa juu zaidi kuliko ule uliochagua au kwenye kifaa chako. (See Tazama mfuatano wa vipindi kwenye tv.jw.org.)

Ukichagua mpangilio wa Kawaida,kituo cha tv.jw.org kitakuchagulia ubora wa picha unaolingana na ukubwa wa skrini ya kompyuta au kifaa chako.

 Amua Kuweka au Kutoweka Maelezo Mafupi

Baadhi ya video zilizopo zina maelezo mafupi. Maelezo hayo yanatumia lugha ileile inayosikika kwenye video hizo.

  • Ikiwa ungependa kuaona maelezo hayo, weka alama kwenye kisanduku cha Onyesha Maelezo Mafupi Yanapopatikana.

  • Ondoa alama kwenye kisanduku ikiwa hauhitaji maelezo mafupi.

  • Bonyeza Tunza ili utunze mipangilio yako.

Taarifa: Mipangilio hii ni kwa video zenye maelezo mafupi, zilizopo aidha kwenye Mfuatano wa Vipindi au Video za Karibuni.

 Chagua Mfuatano wa Vipindi Unaopendelea

Mfumo uliopo utaweka kumbukumbu ya kipindi cha mwisho ulichotazama halafu wakati mwingine ukichgua Mfuatano wa Vipindi .kipindi hicho hicho kitafunguka.

Hata hivyo, huenda ungependa kipindi kilekile kionekane kila unpochagua Mfuatano wa Vipindi kwenye kifaa chako. Kwa mfano, ikiwa wewe ni mzazi, huenda ungependa tablet inayotumiwa na watoto wako, ianze moja kwa moja na kipindi cha Watoto.

  • Ili uanze kutazama Mfuatano wa Vipindi uleule kila mara, nenda kwenye Mipangilio na uchague jina la kipindi.

  • Ili kurudi kwenye mpangilio wa awali, chagua Anza na kipindi changu cha mwisho kutazama.

  • Bonyeza Tunza ili utunze mipangilio yako.