Sehemu ya Mfuatano wa Vipindi kwenye tv.jw.org ni kama tu televisheni yenye vituo kadhaa vinavyoonyesha vipindi kwa kufuata ratiba hususa. Chagua kipindi kimoja ili uanze kutazama video inayoonyeshwa. Ikiwa ungependa kutazama video kuanzia mwanzo, kuisitisha, kuirudisha nyuma, au kuipeleka mbele, nenda kwenye sehemu ya Video za Karibuni

Fuata maelekezo haya kutazama vipindi vilivyopo:

 Tazama Mfuatano wa Vipindi Kwenye Kompyuta

Bonyeza sehemu ya Mfuatano wa Vipindi. Kipindi chako kitafunguka, na video iliyoko kwenye ratiba itacheza.

 • Ili utazame video kwa ukubwa unaojaza skrini, sogeza kasa juu ya video, halafu bonyeza sehemu ya Jaza Skrini.

 • Kupunguza ukubwa wa video ili usijaze skrini, bonyeza kitufe kilichoandikwa Esc kwenye kibodi au usogeze kasa juu ya video na ubonyeze sehemu ya Ukubwa wa kawaida.

 • Kubadili ubora wa picha, sogeza kasa juu ya video, halafu juu ya sehemu ya Mipangilio ya Video. Chagua ubora wa picha unaopenda. (Taarifa: Huenda isiwezekane kufanya hivi katika vipekuzi vyote.)

  Taarifa: Nambari ya juu inaonyesha picha nzuri zaidi, na hilo linamaanisha unahitaji intaneti yenye kasi zaidi. Chagua nambari inayopatana na uwezo wa intaneti yako na ukubwa wa kiwambo chako. (Kwa habari zaidi, ona Badili Mpangilio wa Kompyuta au Kifaa Chako.)

 • Ili kuongeza au kupunguza sauti, sogeza kasa juu ya video, kisha kwenye kitufe cha Sauti. Inua kistari ili kuongeza sauti au ushushe kistari ili kupunguza sauti.

Bofya Cheza Kuanzia Mwanzo ili utoke kwenye mfuatano wa vipindi na utazame video hiyo chini ya sehemu Video za Karibuni.

Dokezo: Nenda kwenye Mpangilio wa Mtumiaji ili uchague ni kipindi gani kitakachokuwa kikifunguka kila mara unapobofya Mfuatano wa Vipindi.

Unapotazama mfuatano fulani wa vipindi kwa muda mrefu bila kubadili kituo, ujumbe utajitokeza na kuuliza ikiwa bado unatazama. Sababu ni kwamba pesa zinatumika ili kurusha kila video, kwa hiyo hatungependa kuendelea kurusha kipindi fulani ikiwa hakuna anayetazama. Ikiwa bado unatazama, bofya OK na utaendelea kutazama mfuatano huo wa vipindi.

 Tazama Mfuatano wa Vipindi Kwenye Kifaa cha Mkononi

Taarifa: Kuna tofauti ndogo katika utendaji wa vifaa vya mkononi kwa kuwa vina skrini zenye ukubwa unaotofautiana na vinaendeshwa kwa programu tofauti-tofauti. Tumetaja baadhi ya tofauti hizo katika maagizo yaliyo hapa chini.

Katika vifaa vikubwa, kama vile tablet, bofya Mfuatano wa Vipindi. Kituo ulichokipangilia kitaanza kucheza.

Katika vifaa vidogo vya mkononi, kama vile simu ya smartphone, bofya kitufe cha Menyu. Bofya Mfuatano wa Vipindi ili kipindi ulichokipangilia kianze kucheza, au bofya kishale kinachoelekeza Chini kilicho upande wa kulia wa Mfuatano wa Vipindi na uchague kituo kimoja kati ya mfuatano wa vipindi.

Bofya Cheza ili uanzishe video.

 • Bofya video mara mbili ikiwa ungependa kuitazama kwenye skrini yote, au ubofye video na kubofya kitufe kilichoandikwa Jaza Skrini.

  Taarifa: Unapotazama video kwa kujaza skrini, vitufe mbalimbali (vya kusitisha, kucheza, kusogeza mbele, kurudisha nyuma) vinaweza kujitokeza lakini huenda visiwe vimewezeshwa.

 • iOS: Ili video isiendelee kujaza skrini yote, bofya video yenyewe, kisha ubofye kitufe cha Skrini ya Kawaida au cha Kwisha.

  Android: Ili video isiendelee kujaza skrini yote, bofya video yenyewe, kisha ubofye kitufe cha Android cha Nyuma.

  Windows Mobile: Ili video isiendelee kujaza skrini yote, bofya kitufe cha Nyuma katika kifaa chako.

 • Ili kubadili ubora wa video, bofya video yenyewe kisha kitufe cha Mpangilio wa Video. Chagua nambari yenye ukubwa unaotaka. (Taarifa: Jambo hili haliwezekani katika vifaa vyote vya mkononi.)

  Taarifa: Nambari ya juu inaonyesha picha nzuri zaidi, na hilo linamaanisha unahitaji intaneti yenye kasi zaidi. Chagua nambari inayopatana na uwezo wa intaneti yako na ukubwa wa skrini yako. (Kwa habari zaidi, ona Badili Mpangilio wa Kompyuta au Kifaa Chako.)

Ili uone ni video gani itakavyofuata, bofya Ratiba ya Vipindi. Katika kifaa kidogo cha mkononi, lazima usogeze maandishi ili uone yanayofuata.

Bofya Cheza Kuanzia Mwanzo ili utoke kwenye mfuatano wa vipindi na utazame video hiyo chini ya sehemu Video za Karibuni.

Dokezo: Nenda kwenye Mpangilio ili uchague ni kipindi gani kitakachokuwa kikifunguka kila mara unapobofya Mfuatano wa Vipindi.

 Badili Kituo Kwenye Kompyuta au Tablet

Video inapocheza katika skrini ya kawaida (si skrini kubwa), orodha ya vituo vilivyopo itaonekana chini ya video hiyo. Bofya kituo kimoja ili uanze kukitazama.

Kwenye kompyuta au tablet, vituo huonekana chini ya skrini. Kipindi kinachocheza huwa na mstari wa bluu juu yake.

Bofya kishale kinachoelekeza Kushoto au Kulia ili uone vituo vingine. Bofya kichwa cha kituo hicho ili uanze kukitazama.

Unapotumia kompyuta, video katika kituo kilichochaguliwa huanza kucheza mara moja. Kwenye vifaa vya iOS na Android, unapaswa kubofya Cheza ili uanze kucheza video hiyo.

 Badili Kituo Kwenye Simu ya Kisasa

Video inapocheza katika skrini ya kawaida (si skrini kubwa), orodha ya vituo vilivyopo itaonekana chini ya video hiyo. Bofya kituo kimoja ili uanze kukitazama.

Katika simu aina ya smartphone, mfuatano wa vipindi huonekana katika orodha iliyopangwa kuanzia juu kwenda chini. Kituo kinachocheza huwa na mstari wa bluu juu yake. Bofya kishale kinachoelekeza Chini kilicho upande wa kulia wa jina la kituo hicho ili uone jina la kipindi kinachoendelea. Angalia orodha yake ili uone vipindi vinavyofuata, urefu wake, na wakati ambapo vitaanza.

Bofya kishale cha Juu ili kufunga orodha ya kituo hicho.

Bofya jina la kituo ili ukifungue, kisha bofya Cheza ili uanze kucheza video iliyoonyeshwa.

 Soma Ratiba ya Vipindi

Kwenye kompyuta au tablet, Ratiba ya Vipindi inapatikana unapotumia katika skrini ya kawaida (si skrini kubwa). Ikiwa unatumia simu aina ya smartphone, ona sehemu yenye kichwa Badili Kituo Kwenye Simu ya Kisasa.

Bofya Orodha ya Vipindi ili uone orodha ya vituo vyote na vipindi vinavyoonyeshwa katika kila kituo.

Kila kituo kimepangwa katika safu yake. Video inayocheza imepangwa kwanza katika safu. Vipindi vitakavyofuata, urefu wake, na wakati ambapo vitaanza, vimeorodheshwa kwa mfuatano.

Bofya kishale kinachoelekeza Kushoto au Kulia ili uone vituo vyote. Bofya kituo unachotaka na ratiba ya vipindi itajifunga na kituo ulichotaka kitafunguka.

Taarifa: Saa zilizoonyeshwa kwenye Ratiba ya Vipindi zinalingana na za eneo lako (yaani, saa inayoonyeshwa katika kompyuta au kifaa unachotumia). Hilo linamaanisha kwamba watazamaji wa kituo kilekile hawatakuwa wakitazama video ileile wakati uleule. Kwa mfano, ikiwa unatazama video fulani saa 1:00 jioni, mtu anayetazama kituo hicho akiwa upande wa mashariki alishatazama video hiyo saa moja kabla yako, wakati saa za eneo anamoishi zilipokuwa saa 1:00 jioni. Mtu anayetazama kituo hicho akiwa upande wa magharibi atatazama video hiyo saa moja baadaye, wakati saa za eneo anamoishi zitakapokuwa saa 1:00 jioni.

Bofya Ratiba ya Vipindi tena ili uifunge na uendelee kutazama video uliyochagua.