Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

JW BROADCASTING

Tazama Mfuatano wa Vipindi Kupitia Roku

Tazama Mfuatano wa Vipindi Kupitia Roku

Sehemu ya Mfuatano wa Vipindi kwenye JW Broadcasting inafanana na ya televisheni iliyo na vituo tofauti vinavyoonyesha vipindi mbalimbali. Ikiwa unataka kudhibiti video (kutazama tena, kuisitisha, kuirudisha nyuma, au kuisogeza mbele), nenda kwenye sehemu ya Video za Karibuni.

(Taarifa: Picha za kifaa cha televisheni cha kubadili vituo kutoka mbali, au kibonyezo, cha Roku 3 zimeonyeshwa. Huenda kisifanane na kibonyezo chako.)

Fuata maagizo haya ili ufurahie kutazama vipindi kwenye JW Broadcasting kupitia Roku:

 Tazama Mfuatano wa Vipindi

Bonyeza Mfuatano wa Vipindi kwenye ukurasa wa mwanzo wa JW Broadcasting ili utazame orodha ya vipindi.

Ukitumia vishale vya kukuelekeza Kushoto na Kulia kwa kutumia kibonyezo cha Roku, unaweza kutafuta kipindi unachotaka. Kipindi ulichochagua kitajitokeza katikati ya kiwambo chako na mbali na picha utaona pia kichwa na ufafanuzi mfupi. Bonyeza kitufe kilichoandikwa OK ili uchague kipindi hicho.

Video inapofunguka, menyu ya vipindi itaonyesha kichwa kikuu cha kituo ulichochagua pamoja na majina ya video tatu zinazofuata.

Dokezo: Video ikifunguka na unataka kuondoa orodha ya vipindi, bonyeza kishale cha Kushoto kwenye kibonyezo cha Roku.

 Badili Kipindi Unachotazama

Unapotazama kipindi fulani, kuna njia mbili za kubadili kituo:

  • Rudi kwenye orodha ya vipindi

    Bonyeza kishale cha Kushoto au Nyuma ili urudi kwenye orodha ya vipindi. Tumia vishale vinavyoelekeza Kushoto na Kulia ili utafute kipindi unachotaka kutazama. Bonyeza kitufe kilichoandikwa OK ili kuchagua kipindi.

  • Hamia kwenye kituo kingine

    Unapotazama kipindi fulani, bonyeza kishale cha Juu au Chini ili kuhamia kwenye kituo kinachotangulia au kinachofuata. Video inapofunguka, menyu ya kituo hicho itaonyesha jina la kituo hicho na jina la video hiyo. Bofya kishale cha Juu au Chini ili kuhama kwenda kwenye kituo kingine au usubiri video imalize kufunguka.

 Tumia Menyu ya Vipindi

Unapotazama kipindi fulani, bonyeza kishale cha Kulia ili upate menyu ya vipindi.

Mbali na jina la kituo na orodha ya mfuatano wa video katika kituo hicho, menyu hiyo itakuruhusu kufanya mambo mengine mawili: Cheza Kuanzia Mwanzo na Onyesha Maelezo Mafupi. Tumia kishale kinachoelekeza Juu au Chini ili kuchagua unachotaka. Bonyeza kitufe kilichoandikwa OK ili kuchagua unachotaka.

  • Cheza Kuanzia Mwanzo: Chagua kufanya hivi ili utazame video hii chini ya sehemu ya Video za Karibuni. Ukiwa hapo unaweza kucheza video hiyo kuanzia mwanzo, uisitishe, uirudishe nyuma, au uisogeze mbele.

  • Onyesha Maelezo Mafupi: Chagua kufanya hivi ili uweze kuona maelezo mafupi ya video unayotazama. Unaweza kufanya hivyo kwa ajili ya video zote zilizo chini ya sehemu ya Mfuatano wa Vipindi au Video za Karibuni. Ili kuondoa maandishi, rudi kwenye menyu hiyo na uchague Ondoa Maelezo Mafupi. (Taarifa: Unaweza kufanya hivyo ikiwa tu maandishi ya video unayotazama yanapatikana.)

Ili kufunga menyu ya vipindi, bofya kishale kinachoelekeza Kushoto, Kulia, au Nyuma.