Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

JW BROADCASTING

Tazama Mfululizo wa Video Kwenye Apple TV

Tazama Mfululizo wa Video Kwenye Apple TV

Sehemu ya Cheza Video Mfululizo inafanana na vipindi vinavyoonyeshwa kwenye vituo vingine vya televisheni. Ikiwa unataka kucheza video (yaani, kutazama tena, kusimamisha kwa muda, kurudisha nyuma na kupeleka mbele), fungua sehemu ya Chagua Video.

(Taarifa: Mwonekano wa kibonyezo cha kubadili vipindi unaoonyeshwa kwenye miongozo hii unaweza usifanane na kibonyezo chako.)

Chagua Cheza Video Mfululizo katika ukurasa wa mwanzo ili ufungue orodha ya vipindi.

Fuata maagizo haya ili upate vipindi kwenye JW Broadcasting vinayopatikana kupitia Apple TV:

 Tazama Vipindi vya Video Mfululizo

Telezesha kwenye kibonyezo chako (Siri remote) kwenda Juu au Chini ili ufungue orodha ya vipindi. Upande wa kushoto wa skrini yako kutaonyeshwa ratiba ya video zitakazopatikana kwenye kipindi kilichowekewa alama. Bofya kibonyezo chako ili utazame kipindi kilichowekwa alama.

Chagua Kipindi Tofauti

 Ili uchague kipindi tofauti huku ukitazama mfululizo wa video fanya yafuatayo:

  • Bofya kitufe cha Menyu ili kurudi kwenye orodha ya vipindi.

  • Telezesha kwenda Juu au Chini ili utafute kipindi unachotaka.

  • Bonyeza kipindi ulichochagua.