Sehemu ya Cheza Video Mfululizo inafanana na vipindi vinavyoonyeshwa kwenye vituo vingine vya televisheni. Ikiwa unataka kucheza video (yaani, kutazama tena, kusimamisha kwa muda, kurudisha nyuma na kupeleka mbele), nenda kwenye sehemu ya Chagua Video.

(Taarifa: Mwonekano wa kibonyezo cha kubadili vipindi unaoonyeshwa kwenye miongozo hii unaweza usifanane na kibonyezo chako.)

Fuata maagizo haya ili uweze kutazama vipindi vya JW Broadcasting kwenye Amazon Fire TV:

 Tazama Mfululizo wa Vipindi

Chagua sehemu ya Cheza Video Mfululizo katika ukurasa wa mwanzo ili uone orodha ya vipindi.

Bonyeza kwenda Juu au Chini kwenye kibonyezo cha kutafuta vipindi cha Amazon Fire TV ili kuchagua vipindi. Upande wa kushoto wa skrini unaonyesha ratiba ya video ambazo zitachezwa kwenye kipindi ulichochagua. Bonyeza kitufe cha Chagua upate kipindi ulichochagua.

 Chagua Kipindi Tofauti

Ili kuchagua kipindi tofauti unapotazama mfululizo unaweza kufanya hivi:

  • Bonyeza kitufe cha Nyuma ili urudi kwenye orodha ya vipindi.

  • Peleka Juu au Chini ili utafute kipindi.

  • Bonyeza kitufe cha Chagua ili kuchagua kipindi.