• Matoleo ya zamani ya JW Lugha yalizima sauti ya programu hiyo mtu alipozima sauti ya mwito kwenye kifaa. Tafadhali sasisha JW Lugha kwenye kifaa chako ili kuhakikisha kwamba una toleo la karibuni zaidi.

  • Angalia ikiwa umezima sauti kwenye kifaa chako. Ikiwa umefanya hivyo, ongeza sauti.

  • Hakikisha kwamba umeongeza sauti kwenye kifaa chako.