Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Awamu ya 4 ya Picha za Warwick (Mei Hadi Agosti 2015)

Awamu ya 4 ya Picha za Warwick (Mei Hadi Agosti 2015)

Katika mfululizo huu wa picha, ona maendeleo yaliyofanywa kwenye ujenzi wa makao makuu mapya ya Mashahidi wa Yehova na jinsi wajitoleaji walivyosaidia katika kazi hiyo ya ujenzi kuanzia mwezi wa Mei hadi Agosti 2015.

Picha ya eneo lote la ujenzi la Warwick litakapokamilika. Kuanzia kushoto juu kwenda kulia:

  1. Jengo la Gereji

  2. Jengo la Maegesho ya Magari ya Wageni

  3. Jengo la Udumishaji na Maegesho ya Wenyeji

  4. Jengo la Makazi B

  5. Jengo la Makazi D

  6. Jengo la Makazi C

  7. Jengo la Makazi A

  8. Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Mei 6, 2015—Eneo la ujenzi la Warwick

Mfanyakazi akijitayarisha kushusha kifaa cha kuzuia takataka kwenye Ziwa Sterling Forest (Blue Lake). Kifaa hicho kitazuia takataka kubwa zisipite.

Mei 6, 2015—Jengo la Udumishaji na Maegesho ya Wenyeji

Wafanyakazi wakijenga ukuta wa kingo kwenye eneo lilio juu ya Jengo la Udumishaji. Mbinu hiyo wanayotumia ni rahisi zaidi.

Mei 15, 2015—Eneo la ujenzi la Warwick

Mpiga-picha akipiga picha kwenye eneo la ujenzi. Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova huangalia picha kila wiki ili kujua maendeleo ya mradi.

Mei 30, 2015—Eneo la Tuxedo

Wajitoleaji wawili kutoka kusini mwa California wamefika ili kufanya kazi katika Idara ya Mabomba. Wao ni miongoni mwa mamia ya wafanyakazi waliofika Mei 30, 2015 eneo la Tuxedo, linalotegemeza ujenzi wa Warwick. Agosti 1, kulikuwa na kilele kipya cha wajitoleaji wapya waliofika ili kusaidia kazi ya ujenzi.

Juni 9, 2015—Jengo la Makazi B

Mwanakandarasi akitumia kreni kuinua na kusimamisha ukuta. Jengo la Makazi B lilikuwa jengo la mwisho kuwekwa kuta na madirisha.

Juni 16, 2015—Jengo la Makazi C na D

Daraja linalounganisha Jengo la Makazi C na D likiwekwa na wanakandarasi.

Juni 25, 2015—Jengo la Makazi C

Wafanyakazi wakitandaza nyasi upande wa magharibi mwa eneo la ujenzi la Warwick.

Julai 2, 2015—Eneo la ujenzi la Warwick

Wafanyakazi wakirekebisha mfereji wa kupunguza maji ya bwawa. Mfereji huo ulijengwa miaka ya 1950. Marekebisho hayo yanafanywa kwa sababu ya dhoruba kali zaidi na mvua kubwa inayokumba eneo hilo kwa sasa. Hivyo mfereji huo utasaidia kuzuia uharibifu unaotokana na mafuriko kwenye eneo la ujenzi la Warwick na maeneo ya jirani.

Julai 15, 2015—Jengo la Makazi A

Ili kupunguza msongamano katika eneo la ujenzi, kazi zinazofanywa ndani kama vile kupanga rangi na kufunika mabomba, zilifanywa usiku. Mamia ya wafanyakazi wa kikosi cha pili walipangiwa kufanya kazi kuanzia saa 9:00 mchana hadi saa 8:00 usiku.

Julai 20, 2015—Jengo la Makazi D

Mfanyakazi akimzoeza mwenzake kazi ya kufunika mabomba ili kuzuia maji kuganda wakati wa baridi kali.

Julai 21, 2015—Jengo la Makazi B

Mfanyakazi akipaka rangi daraja linalounganisha Jengo la Makazi B na Jengo la Udumishaji.

Julai 27, 2015—Eneo la Tuxedo

Wafanyakazi wakisubiri kwenye eneo la kuegesha magari, kusafirishwa mpaka Warwick. Mabasi kadhaa huwapeleka wafanyakazi kwenye eneo la kazi na kuwarudisha.

Julai 27, 2015—Eneo la Tuxedo

Wafanyakazi watatu wa Warwick wakinyolewa nywele. Zaidi ya watu 400 hunyolewa kila wiki kwenye vyumba vya kunyolea nywele vilivyoko Tuxedo, Warwick, na kwenye bohari iliyoko Montgomery.

Agosti 3, 2015—Eneo la ujenzi la Warwick

Sehemu za kuweka zege ikiandaliwa katika eneo la uzalishaji wa nishati ya mvuke kutoka ardhini. Kwa kutumia visima 120 vyenye kina chenye urefu wa meta 150 , mfumo huo utasaidia kuleta joto wakati wa majira ya baridi na kuleta baridi wakati wa kiangazi. Nishati ya mvuke unaotoka ardhini inapunguza gharama na pia ni matumizi mazuri ya mazingira katika eneo la Warwick.

Agosti 7, 2015—Montgomery, New York

Vifaa vya kazi vikiletwa na kukusanywa kwa ajili ya kazi maalumu kwenye eneo la ujenzi la Warwick.

Agosti 14, 2015—Eneo la Tuxedo Park, New York

Wafanyakazi wawili wa Warwick (wa pili na watatu kutoka kulia) wakifurahia mlo pamoja na familia inayoishi eneo hilo. Familia nyingi za Mashahidi wa Yehova zimejitolea kuwakaribisha wajitoleaji wanaofanya kazi ya ujenzi kuishi katika nyumba zao.

Agosti 17, 2015—Jengo la Udumishaji na Maegesho ya Wenyeji

Mfanyakazi akipima urefu kwa kutumia darubini maalumu.

Agosti 20, 2015—Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Kazi ya kuweka vioo kwenye eneo la mapokezi kwa ajili ya wageni wanaokuja kutembelea eneo hilo, tayari imekamilika.

Agosti 26, 2015—Eneo la ujenzi la Warwick

Kati ya Mei na Agosti, kuta na paa zilikamilishwa kuwekwa kwenye Jengo la Makazi B, ambalo ni jengo la makazi la mwisho kukamilishwa. Madaraja ya wanaotembea kwa miguu yanayounganisha majengo mbalimbali yaliwekwa, na baada ya hapo wafanyakazi walianza kazi ya kutengeneza mandhari.

Pata Kujua Mengi Zaidi

NI NANI WANAOFANYA MAPENZI YA YEHOVA LEO?

Mashahidi wa Yehova Ni Watu wa Aina Gani?

Unawafahamu Mashahidi wangapi wa Yehova? Unajua nini hasa kutuhusu?