Mashahidi wa Yehova wanajenga majengo mapya yatakayotumiwa kama makao makuu ya ulimwenguni pote katika mji wa Warwick, New York. Kuanzia Mei hadi Agosti 2014, wajenzi walipiga hatua kubwa katika kujenga Jengo la Gereji, Jengo la Ofisi za Usimamizi na Huduma, na majengo C na D ya makazi. Picha zifuatazo zinaonyesha baadhi ya kazi ambazo zilifanywa katika kipindi hicho chenye shughuli nyingi.

Mfano wa majengo yaliyokamilika ya Warwick. Kuanzia kushoto juu kwenda kulia:

  1. Jengo la Gereji

  2. Jengo la Maegesho ya Magari ya Wageni

  3. Jengo la Udumishaji/Maegesho ya Wenyeji

  4. Jengo la Makazi B

  5. Jengo la Makazi D

  6. Jengo la Makazi C

  7. Jengo la Makazi A

  8. Jengo la Ofisi za Usimamizi/Huduma