Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Awamu ya 6 ya Picha za Warwick (Machi hadi Agosti 2016)

Awamu ya 6 ya Picha za Warwick (Machi hadi Agosti 2016)

Katika mfululizo huu wa picha, ona maendeleo yaliyofanywa kwenye ujenzi wa makao makuu mapya ya Mashahidi wa Yehova na jinsi wajitoleaji walivyosaidia katika kazi hiyo ya ujenzi kuanzia mwezi wa Machi hadi Agosti 2016.

Picha ya eneo lote la ujenzi la Warwick lililokamilika. Kuanzia kushoto juu kwenda kulia:

  1. Jengo la Gereji

  2. Jengo la Maegesho ya Magari ya Wageni

  3. Jengo la Udumishaji na Maegesho ya Wenyeji

  4. Jengo la Makazi B

  5. Jengo la Makazi D

  6. Jengo la Makazi C

  7. Jengo la Makazi A

  8. Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Machi 16, 2016​—Eneo la ujenzi la Warwick

Wafanyakazi wakishusha mti aina ya mwaloni na maple katika eneo linalopandwa miti. Zaidi ya miti 1,400 imepandwa kwenye eneo la ujenzi la Warwick.

Machi 23, 2016​—Jengo la Gereji

Wafanyakazi wa Warwick wakiwa kwenye Mlo wa Jioni wa Bwana. Jumla ya watu 384 walihudhuria tukio hilo ambalo hufanywa kila mwaka na Mashahidi wa Yehova duniani pote.

Aprili 15, 2016​—Eneo la ujenzi la Warwick

Seremala wakiweka madirisha kwenye nyumba iliyo kwenye lango. Wafanyakazi watakaokuwa hapo langoni watakaribisha wageni, watatoa ulinzi, na kuongoza magari yanayoingia na kutoka kwenye eneo.

Aprili 19, 2016​—Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Baba na mwana wake wanakifanya kazi pamoja kutandaza mazulia kwenye kijia katika ghorofa ya pili. Vipande vya zulia vinawekwa hasa kwenye maeneo yanayotumiwa na watu wengi, kwa kuwa ni rahisi kubadili kipande kilichoharibika cha zulia kuliko kubadili zulia lote.

Aprili 27, 2016​—Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Seremala wakigawanya ofisi kwa vifaa vinavyoweza kuhamishika. Kugawanya ofisi kwa njia hiyo kunaruhusu idara mbalimbali zibadili ukubwa wa ofisi ikihitajika kufanya hivyo.

Mei 10, 2016​—Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Mfanyakazi akitayarisha eneo ili ligawanywe na kuwekwa vyoo. Eneo hili lililoko karibu na mapokezi litakuwa na vyoo kwa ajili ya wageni.

Mei 26, 2016​—Eneo la ujenzi la Warwick

Wakiwa katika mazoezi, Wafanyakazi wa Idara ya Huduma ya Dharura wajitayarisha kuzima moto. Kwa kujitayarisha kukabiliana na hali kama hizo, wazima-moto hawa wataweza kuokoa wafanyakazi na majengo ya Warwick, na pia kupunguza kazi inayofanywa na makampuni ya huduma za dharura katika eneo hilo.

Mei 30, 2016​—Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Mhudumu akiwasaidia wafanyakazi wa Warwick waliokusanyika kwenye chumba cha kulia chakula kupata mahali pa kuketi muda mfupi kabla ya kuanza kwa programu ya Ibada ya Asubuhi iliyounganishwa kwa mara ya kwanza katika eneo hilo.

Mei 31, 2016​—Jengo la Udumishaji na Maegesho ya Wenyeji

Seremala akitumia kifaa kinachotoa mwangaza kuweka moja kati ya ishara zaidi ya 2,500 ambayo itawaelekeza wenyeji na wageni.

Juni 1, 2016​—Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Fundi akiweka vishikilio vya kwenye ngazi zinazotoka eneo la mapokezi mpaka kwenye ukumbi. Blanketi la kuzuia moto ambalo linaonekana kwenye picha linatumika kulinda maeneo ambayo ujenzi umekamilika ili yasiharibike.

Juni 9, 2016​—Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Mfanyakazi wa Idara ya Ukuta na Paa akikamilisha ujenzi wa ukuta katika eneo la “Imani Yenye Matendo,” ambalo ni moja kati ya maeneo matatu ya maonyesho yatakayotembelewa na wageni bila kuongozwa na mtu mwingine. Muundo wa maeneo hayo ya maonyesho unakazia kichwa cha kila onyesho.

Juni 16, 2016​—Jengo la Gereji

Wafanyakazi wakinyunyiza kemikali ya kushindilia zege. Hatua hii ya kushindilia husaidia kufunika kabisa sakafu na hivyo kuifanya idumu, iweze kuzuia vumbi na alama za magurudumu na kufanya iwe rahisi kuidumisha.

Juni 29, 2016​—Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Mafundi seremala wakiweka paa linaloangaza juu ya njia ya kuingia eneo la mapokezi. Paa hilo linalopenyeza nuru litapitisha mwanga hafifu kwenye njia hiyo kuu ya kuelekea mapokezi.

Juni 29, 2016​—Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Mume na mke wake wakiweka vigae kwenye eneo la mwingilio wa maonyesho ya wageni yenye kichwa “Biblia na Jina la Mungu.”

Julai 6, 2016​—Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Seremala akiweka moja kati ya viti 1,018 kwenye ukumbi. Ukumbi huu utatumiwa kwa ajili ya Funzo la Mnara wa Mlinzi na programu nyingine za kiroho za familia ya Betheli.

Julai 9, 2016​—Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Kwenye eneo la mapokezi, seremala, mafundi umeme, na wafanyakazi wengine wakiweka ishara iliyopambwa kwa taa ya kuwakaribisha wageni.

Julai 13, 2016​—Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Washiriki wawili wa kikundi cha Wasaidizi wa Ujenzi wakiweka maji kwenye eneo la mapokezi kwa ajili ya wafanyakazi. Wafanyakazi wa ujenzi walikumbushwa kwa ukawaida kunywa maji mara kwa mara hasa wakati wa majira ya joto.

Julai 19, 2016​—Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Seremala akimalizia ujenzi wa vifaa vitakavyotumiwa kuhifadhi Biblia adimu katika eneo la maonyesho yenye kichwa “Biblia na Jina la Mungu.” Eneo hilo la maonyesho litatia ndani picha zinazozunguka zinazoonyesha Biblia nyingine na vitu vingine vya kale vinavyohusiana na Biblia.

Julai 22, 2016​—Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Seremala akisaidiwa na picha inayoonyeshwa kwa kutumia projekta anabandika kipande kinachowakilisha nchi ya Australia na visiwa vya Kusini-Mashariki mwa Asia kwenye ramani katika eneo la mapokezi. Jina Mashahidi wa Yehova limeandikwa kwenye ukuta huo katika lugha 700 hivi.

Julai 23, 2016​—Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Washiriki wa familia ya Betheli wakiwa kwenye kipindi cha kujifunza mambo ya msingi. Vipindi hivi vimeandaliwa kwa ajili ya kuwakaribisha, kuwafunza, na kuwaonya Wanabetheli wa watakaoishi Warwick kuhusu hatari za kiusalama ambazo bado zipo kwenye eneo hilo la ujenzi.

Agosti 17, 2016​—Studio ya JW Broadcasting

Wafanyakazi wakiweka kifaa cha kutoa mwanga pamoja na vifaa vya kukitegemeza juu ya dawati la msemaji wa JW Broadcasting. Vifaa vingi vya studio vilihamishwa kutoka kwenye studio ya zamani ya Brooklyn.

Agosti 24, 2016​—Eneo la ujenzi la Warwick

Fundi wa umeme akiweka ishara mpya iliyopambwa na taa (LED) kwenye eneo la lango kuu la kuingia. Kufikia Septemba 1, idara nyingi za makao makuu ya ulimwenguni pote zilikuwa zikifanya kazi Warwick.