Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Awamu ya 2 ya Picha za Wallkill (Novemba 2014 Hadi Novemba 2015)

Awamu ya 2 ya Picha za Wallkill (Novemba 2014 Hadi Novemba 2015)

Mashahidi wa Yehova walifanya kazi ya kupanua na kuboresha majengo yao yaliyoko Wallkill, New York. Katika picha hizi, ona jinsi mradi huo ulivyoendelea kuanzia Novemba 2014 hadi Novemba 2015.

Picha za majengo ya Wallkill kufikia Oktoba 15, 2015.

  1. Kiwanda cha Kuchapishia

  2. Jengo la Kwanza la Ofisi

  3. Jengo la Makazi E

  4. Chumba cha Kulia Chakula

  5. Dobi

  6. Jengo la Pili la Ofisi

  7. Jengo la Makazi D

Desemba 4, 2014​—Jengo la Pili la Ofisi

Mwingilio wa jengo jipya la ofisi ukitayarishwa kwa ajili ya kutengeneza barabara ya wale wanaotembea. Sehemu ya chini upande wa kushoto wa barabara hiyo inapashwa joto ili kufanya sakafu isiteleze wakati wa baridi kali. Jengo hilo litakuwa kwa ajili ya Ofisi ya Betheli, Ofisi za Halmashauri ya Tawi, na Idara ya Utumishi.

Desemba 5, 2014​—Jengo la Makazi D

Mfanyakazi akitumia mashine kufanya matayarisho kwenye sehemu inayotarajiwa kuwekwa sakafu. Mashine hiyo imeunganishwa na kifaa cha kufyonza vumbi.

Januari 9, 2015​—Jengo la Makazi E

Chumba kilichojengwa kwa muundo wa nusu duara kwa ajili ya mapokezi ya wageni na Wanabetheli zaidi ya 200 wanaoishi kwenye jengo la Makazi E. Ukarabati wa jengo hili ulitia ndani kuwekwa kwa madirisha yanayoingiza mwanga wa kutosha na mfumo mpya wa king’ora cha moto.

Februari 9, 2015​—Kiwanda cha Kuchapishia

Fundi akiunganisha nyaya za vifaa vya mawasiliano kwenye jengo jipya la Mafunzo ya Ufundi. Jengo hili limejengwa kwa ajili ya kuwapatia ujuzi wafanyakazi katika mambo kama vile ufundi wa mabomba, kudumisha vifaa vya umeme, na usalama.

Februari 17, 2015​—Kiwanda cha Kuchapishia

Fundi wa umeme akiweka taa za LED katika jengo jipya la Idara ya Mafunzo ya Ufundi.

Machi 2, 2015​—Jengo la Kwanza la Ofisi

Mfanyakazi akichunguza nafasi zilizopo kati ya mabomba ya kupitisha nyaya za umeme. Eneo hili limekarabatiwa kwa ajili ya idara mbalimbali za ofisi ya tawi zilizohamishiwa kutoka Brooklyn.

Machi 3, 2015​—Jengo la Makazi D

Fundi wa mabomba akichomelea mabomba ambayo yatatumiwa kusambaza maji ya moto kwenye makazi.

Machi 31, 2015​—Jengo la Makazi D

Wafanyakazi wakiweka vitu vya kuzuia maji yasiingie kwenye dirisha. Madirisha 298 yanayoingiza mwanga mwingi yamewekwa kwenye jengo hili. Madirisha haya yanapunguza gharama ya umeme katika kipindi cha kiangazi na masika.

Aprili 17, 2015​—Jengo la Kwanza la Ofisi

Mafundi wakitumia mawe yaliyotumiwa kujenga majengo miaka ya 1970 kujenga upya ukuta wa maegesho, ulioko kati ya Jengo la Kwanza la Ofisi na Jengo la Makazi E.

Aprili 17, 2015​—Jengo la Kwanza la Ofisi

Fundi akitayarisha ukuta kwa ajili ya kupaka rangi. Jengo hili lilikarabatiwa kwa ajili ya idara ya Hesabu, Kompyuta, na Ununuzi.

Juni 8, 2015​—Jengo la Makazi D

Fundi wa umeme akivuta waya kwenye paa ili kuunganisha na nyaya za kuzuia radi. Kwa kuwa nyaya hizo zimekusudiwa kuzuia radi, zinapeleka umeme ardhini kutoka kwenye radi ili kuzuia uharibifu wa majengo.

Juni 8, 2015​—Jengo la Makazi D

Wakati wa mradi wa kupanua eneo la Wallkill, mazingira ya eneo hilo yalitunzwa vizuri kutia ndani miti mingi kama inavyoonekana kwenye picha hii. Mnara wa maji ulioko upande wa kushoto, ambao una tangi lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita 150,000, ni kifaa muhimu sana cha usambazaji wa maji, vifaa vya kuzima moto, na mfumo wa kuzima moto ulioko kwenye eneo la Wallkill.

Juni 25, 2015​—Jengo la Kwanza la Ofisi

Fundi seremala akiweka baadhi ya vipande 1,800 vya mbao kwa ajili ya ukuta wa nyuma. Vipande hivi vya mbao ambavyo vina ukubwa mbalimbali vinapunguza mwangwi.

Julai 9, 2015​—Jengo la Pili la Ofisi

Charles Reed amekuwa akitumikia Betheli tangu mwaka 1958. Ndugu Reed alisaidia kubuni ramani na kuweka zege kwenye kiwanda cha kuchapishia kilichokuwa Betheli ya Brooklyn ambacho kilikuwa kikichapa machapisho kwa ajili ya Marekani na nchi nyingine nyingi. Wakati wa mradi wa kupanua majengo ya Wallkill, Ndugu Reed alifanya kazi katika timu ya kupima ubora.

Agosti 17, 2015​—Jengo la Kwanza la Ofisi

Wafanyakazi wakibeba viti vipya na kuvipeleka ukumbini. Ukumbi uliokarabatiwa unatosha kuwekwa viti kwa ajili ya watu 812.

Septemba 21, 2015​—Jengo la Kwanza la Ofisi

Ukarabati wa ukumbi ulitia ndani kuwekwa kwa skrini za video na vifaa vya kufanya sauti isikike vizuri ukumbini.

Oktoba 12, 2015​—Jengo la Makazi D

Kituo cha wauguzi kikijengwa kwenye sehemu ya kuwatunzia wagonjwa iliyokarabatiwa. Ili kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa, njia za kuingilia zilipanuliwa na bafu ziliongezwa ukubwa.

Oktoba 15, 2015​—Eneo la Wallkill

Picha ya majengo ya Wallkill, ambayo yanakadiriwa kuwa na vyumba vya kulala washiriki wa familia ya Betheli 2,000. Sehemu kubwa ya mradi wa upanuzi​—uliohusisha eneo la zaidi ya mita za mraba 102,000 ya majengo mapya au yaliyokarabatiwa​—ilikamilika kufikia Novemba 30, 2015.