Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Mkaguzi wa Usalama Awapongeza Mashahidi

Mkaguzi wa Usalama Awapongeza Mashahidi

Mkaguzi mmoja wa usalama wa serikali alipotembelea ujenzi wa Jumba moja la Ufalme katika kitongoji kimoja huko Sydney, Australia, alisema hivi: “Kwa muda mrefu sana, sijatembelea eneo la ujenzi linalozingatia usalama kama hilo.

Mkaguzi huyo aliandika hivi: “Eneo hilo lilisimamiwa kwa njia nzuri sana. . . . [Lilikuwa] safi sana na nadhifu na kulikuwa na sehemu ya kuingilia na kutokea, nyaya zote za umeme zilikuwa zimeshikiliwa ukutani kwa kulabu za plastiki, [na] vifaa vya kuzima moto [vilikuwa] mahali vinapoweza kufikiwa kwa urahisi na haraka . . . Kila mtu katika eneo hilo la ujenzi alikuwa amevalia shati lenye mikono mirefu, suruali ndefu, kofia ngumu na miwani ya kukinga macho. . . . Wafanyakazi kwenye ujenzi huo walikuwa wenye urafiki sana.

Msimamizi wa ujenzi huo, Victor Otter, alisema, “Mashahidi huona usalama kuwa jambo muhimu sana. Tunapofanya kazi kwa kuzingatia usalama, tunaonyesha maoni ya Mungu kuhusu uhai na tunafanya kazi kwa upatano na furaha. Baada ya kufanya kazi ngumu siku nzima, mimi huenda nyumbani nikiwa ninatabasamu.

Jumba hilo la Ufalme linaloweza kutoshea watu 127 lilikamilishwa Aprili 2012.