Mashahidi wa Yehova wanajenga majengo mapya na kurekebisha majengo ya zamani ya ofisi ya tawi ya nchini Filipino iliyopo Quezon City. Kwa kuwa sasa machapisho kwa ajili ya Filipino huchapishwa katika ofisi ya tawi ya Japani, jengo lililotumiwa zamani kwa kazi ya uchapishaji nchini Filipino limebadilishwa na kuwa ofisi za Idara za Utafsiri, Kompyuta, Usanifu-Majengo na Ujenzi, Udumishaji, na Usafirishaji. Picha hizi zinaonyesha ujenzi na ukarabati mbalimbali uliofanywa katika jengo hilo na majengo mengine kuanzia Februari 2014 hadi Mei 2015. Mradi huo umekusudiwa kukamilika Oktoba 2016.

Picha ya jengo lote la ofisi ya tawi ya Filipino litakapokamilika. Majengo yanayojengwa au kukarabatiwa yanatia ndani:

  • Jengo la 4 (Makazi)

  • Jengo la 5 (Studio, Idara ya Utumishi)

  • Jengo la 6 (Bustani, Gereji, Uchomeleaji)

  • Jengo la 7 (Kompyuta, Usanifu-Majengo na Ujenzi, Udumishaji, Usafirishaji, Utafsiri)