Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

“Kwa Kweli Ninyi Ni Mfano Mzuri!”

“Kwa Kweli Ninyi Ni Mfano Mzuri!”

MASHAHIDI WA YEHOVA katika mji wa Saponara, Sicily, walipokea tuzo kwa sababu ya kazi yao ya kutoa msaada baada ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko.

Novemba 22, 2011, mafuriko yenye kuleta uharibifu yalikumba baadhi ya miji na vijiji katika mkoa wa Messina. Jioni hiyo, katika mji wa Saponara, maporomoko ya ardhi yaliwaua watu watatu—mtoto mmoja na watu wazima wawili.

Siku zilizofuata msiba huo, Mashahidi wa Yehova walipanga vikundi vya wafanyakazi wa kujitolea na kuwapa vifaa vya kuondoa matope na vifusi katika maeneo yaliyoharibiwa vibaya.

Vikundi hivyo vilishirikiana pamoja na wenye mamlaka na vilitoa msaada mahali ambapo kulikuwa na uhitaji mkubwa. Waliendelea kufanya kazi hata baada ya hali ya dharura kwisha. Mashahidi 50 hadi 80 walishiriki, na baadhi yao ambao walitoka umbali wa zaidi ya kilomita 97.

Wakazi wengi wa eneo lililokumbwa na msiba huo wa asili walionyesha shukrani zao kwa Mashahidi. Meya wa eneo hilo alisikika akisema hivi mara kadhaa: “Kwa kweli ninyi ni mfano mzuri!

Miezi mitano baadaye, kwa niaba ya manispaa ya mji huo, diwani wa Saponara, Fabio Vinci, alilipa kutaniko la Mashahidi wa Yehova la eneo hilo tuzo.