Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Mashahidi wa Yehova Wametunukiwa Tuzo ya Utunzaji wa Mazingira

Mashahidi wa Yehova Wametunukiwa Tuzo ya Utunzaji wa Mazingira

Viwanda vinavyosimamiwa na Mashahidi wa Yehova nchini Mexico, vilitunukiwa cheti cha kuhifadhi mazingira yakiwa safi kwa mwaka wa saba mfululizo.

Mnamo Septemba 26, 2012, serikali ya Mexico iliwapa Mashahidi wa Yehova cheti rasmi cha usafi kwa sababu ya “jitihada zao za kusafisha na kutunza mazingira.”

Programu ya kutunza mazingira ni mpango ambao umekusudiwa kukuza maendeleo ya viwanda bila kuharibu mazingira. Kila mwaka, Mashahidi wa Yehova wanashiriki katika mpango huo, hata ingawa wao si shirika la kibiashara. Msemaji wa kiwanda cha Mashahidi wa Yehova nchini Mexico alisema hivi: “Ili kupewa cheti cha utunzaji mzuri wa mazingira, inatupasa tuhakikishe kwamba namna kiwanda kilivyojengwa lazima kiwe na mabomba ya kutoa taka nje, na ujenzi huo ukidhi viwango vya kimazingira vilivyowekwa na serikali katika mambo saba muhimu: hewa, maji, mahali pa kutupa taka jijini, mahali pa kutupa takataka ambazo ni hatari zaidi kiafya, usalama, tuna nishati ya umeme, na tuwe na mafunzo ya kutunza mazingira. Viwanda haviko chini ya wajibu wa kujiandikisha katika mpango huu. Hata hivyo, sisi tumejiunga katika mpango huu kwa hiari.”

Mashahidi wa Yehova ulimwenguni pote wanajitahidi kufanya kadiri ya uwezo wao kuhakikisha kwamba wanatunza vizuri mazingira ya dunia yetu.