Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Mashahidi wa Yehova Waelimisha Wazazi na Watoto Kuhusu Kutendewa Vibaya Kingono

Mashahidi wa Yehova Waelimisha Wazazi na Watoto Kuhusu Kutendewa Vibaya Kingono

Biblia huwafundisha wazazi kuwapenda, kuwaongoza, na kuwalinda watoto wao na pia kuwaona kuwa zawadi kutoka kwa Mungu. (Zaburi 127:3; Methali 1:8; Waefeso 6:1-4) Hatari mojawapo ambayo wazazi wanapaswa kuwalinda watoto wao kutokana nayo ni kutendewa vibaya kingono.

Kwa miaka mingi, Mashahidi wa Yehova wamechapisha na kugawanya habari zinazoweza kusaidia familia ziwe na mahusiano mazuri. Pia, wamechapisha habari zinazowasaidia wazazi kuwalinda watoto wao wasitendewe vibaya kingono na kuwaelimisha kuhusu watu wanaowavizia ili wafanye ngono nao. Ifuatayo ni orodha ya machapisho yaliyotolewa na Mashahidi wa Yehova yaliyo na miongozo hususa kuhusiana na masuala hayo. Angalia idadi ya nakala na lugha za machapisho yenye habari hizo. *

 • Kichwa: Zinaa ya Maharimu—Uhalifu Uliofichwa

  • Chapisho: Agosti, 1982, toleo la Amkeni!

  • Idadi ya nakala: 7,800,000

  • Idadi ya lugha: 34

 • Kichwa: Msaada kwa Wale Waliotendewa Vibaya Kingono na Watu wa Ukoo

  • Chapisho: Oktoba 1, 1983, toleo la Mnara wa Mlinzi la Kiingereza

  • Idadi ya nakala: 10,050,000

  • Idadi ya lugha: 102

 • Vichwa: Kushika-shika Uchi wa Watoto—Ubaya Unaoshtua Akina Mama Wote; Kushika-shika Uchi wa Watoto—‘Ni Nani Angefanya Jambo Kama Hilo?’; Kushika-shika Uchi wa Watoto—Wewe Unaweza Kulinda Mtoto Wako

  • Chapisho: Desemba, 1985, toleo la Amkeni!

  • Idadi ya nakala: 9,800,000

  • Idadi ya lugha: 54

 • Vichwa: Watu Wasio na Hatia Waliotendewa Vibaya Kingono Utotoni; Madhara Yaliyojificha Yatokanayo na Kutendewa Vibaya Kingono Utotoni

  • Chapisho: Oktoba 8, 1991, toleo la Amkeni! la Kiingereza

  • Idadi ya nakala: 12,980,000

  • Idadi ya lugha: 64

 • Vichwa: Mtoto Wako Yumo Hatarini!; Twaweza Kuwalindaje Watoto Wetu?; Kuzuia Nyumbani

  • Chapisho: Oktoba 8, 1993, toleo la Amkeni!

  • Idadi ya nakala: 13,240,000

  • Idadi ya lugha: 67

 • Kichwa: Walinde Watoto Wako

  • Chapisho: Tangazo la Utumishi la Umma Video Namba 4, ya mwaka wa 2002

  • Idadi ya lugha: 2

 • Kichwa: Jinsi Yesu Alivyolindwa

 • Vichwa: Hatari Inayowahangaisha Wazazi Wote; Jinsi ya Kuwalinda Watoto Wako; Ilinde Familia Yako

  • Chapisho: Oktoba 2007, toleo la Amkeni!

  • Idadi ya nakala: 34,267,000

  • Idadi ya lugha: 81

 • Vichwa: Ninawezaje Kujilinda na Washambuliaji wa Kingono?; Maswali Ambayo Wazazi Huuliza: Je, Nizungumze na Mtoto Wangu Kuhusu Ngono?

 • Kichwa: Wazazi Wanawezaje Kuwafundisha Watoto Wao Kuhusu Ngono?

  • Chapisho: Tovuti ya jw.org; makala iliyotolewa Septemba 5, 2013

  • Idadi ya lugha: 64

Mashahidi wa Yehova wataendelea kuwaelimisha wazazi na watoto wao ili waepuke madhara ya kuviziwa na watu wanaotaka kufanya nao ngono.

^ fu. 3 Tarehe ni za matoleo ya Kiingereza.