Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Je, Ninyi Ni Dhehebu la Marekani?

Je, Ninyi Ni Dhehebu la Marekani?

Makao yetu makuu yako Marekani. Hata hivyo, sisi si dhehebu la Marekani kwa sababu zifuatazo:

  • Watu hufafanua dhehebu kuwa kikundi ambacho kimetokana na dini kubwa. Mashahidi wa Yehova hawakutokana na dini nyingine. Badala yake, tunaamini kwamba tumerudisha Ukristo uliokuwepo katika karne ya kwanza.

  • Mashahidi wa Yehova wanapatikana katika zaidi ya nchi 230. Haidhuru tunaishi wapi, uaminifu wetu ni kwa Yehova Mungu na Yesu Kristo, si kwa serikali ya Marekani au kwa serikali nyingine yoyote ya kibinadamu.—Yohana 15:19; 17:15, 16.

  • Mafundisho yetu yote yanategemea Biblia, si maandishi ya kiongozi fulani wa kidini nchini Marekani.1 Wathesalonike 2:13.

  • Tunamfuata Yesu Kristo, wala si kiongozi yeyote mwanadamu.Mathayo 23:8-10.